WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Tuesday, June 28, 2016

JE MAOMBI YETU TUNAYAOMBA KATIKA NJIA SAHIHI?



June 28

Yohana 16:24


Tafakri ya leo tujukumbushe umuhimu wa kufanya maombi ipasavyo ili tuweze kupata kile ambacho kweli tunakihitaji kwa wakati muafaka;  Tunatakiwa kukubali kuwa  Mungu anajibu maombi yetu lakini pengine jibu lake linakuwa hapana wakati sisi tulikuwa tumetegemea ndio; Tukumbuke kuwa hata jibu likiwa hapana ni kwa ajili ya faida yetu sisi kama binadamu ambao hatuna upeo wa kuweza kuona yale ambayo yako mbele yetu; Jukumu letu la msingi wakati tukiwa tunafanya maombi tunatakiwa tuwe  watu tuliojaa uaminivu na ukweli na tujue kuwa ambaye anatawala maombi yetu ni mmoja tu ndiye yeye ambaye ni Alpha na Omega; yeye ndio anayetufanya tuyaelewe maisha yetu; tuyakubali na mwisho ndiye anayeleta uzima. Je tunapoomba maombi yetu tunaomba katika njia sahihi na lengo sahihi; Yakobo 4:3 anatukumbusha Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu. Tukumbuke kuwa lengo kubwa sala kwanza ni kumshukuru na kumwabudu Mungu kwa wema na utukufu wake. Je tunapomwomba Mungu tunakuwa tayari tumekiri makosa yetu na kuomba msamaha?

Tafakari yetu inaendelea kutufundisha kuwa mkono wa Mungu sio mfupi katika kutuokoa au sikio lake ni bofu kusikia, tatizo ni dhambi zetu ambazo zinakuwa zinatutenganisha sisi nayeye hata asisikie shida na maombi yetu kwa wakati kwani anatusubiri sisi kwanza tujitambue kuwa tuna dhambi nasi tuweze kukiri dhambi zetu na kasha kuomba msamaha kabala ya kuomba ili tupate msadda wa shida zetu. Isaya 59: 1-2 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.  Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong'ona ubaya. Ezekiel 14:3 Mwanadamu, watu hawa wametwaa vinyago vyao na kuvitia mioyoni mwao, nao wameweka kwazo la uovu wao mbele ya nyuso zao. Je! Ni laiki yangu niulizwe na wao katika neno lo lote? 

Katika Tafakari yetu leo tukumbuke kuwa ni jambo la muhimu sana kudumisha uhusiano wetu mzuri wakati wote; kwa kufanya hivyo tutaweza kushinda majaribu ya Shetani ambaye anasababisha maombi yetu yasipokelewe; Laki kama tutadumisha  na kujielekeza kwa Mungu tutaweza kushinda kama Injili ya Yohana 15:7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. Tatizo maisha yetu bado tunayaishi katika ulimwengu wa dhambi na kiburi huku tukitegemea Mungu asikilize shida zetu na kutubariki. Je Mungu anaweza kumbariki Mwenye dhambi ambaye hajitambui na hayuko tayari kujuta dhambi zake? 1 Yohana 3:21-22 Wapenzi, mioyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu;  na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.  Tukumbke kuwa hatuwezi kumzihaki Mungu Wagalatia 6:7 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.

Zaburi ya 66:17-20  inatukumbusha kuwa Nalimwita kwa kinywa changu, Na sifa kuu zilikuwa chini ya ulimi wangu. Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu, Bwana asingesikia.  Hakika Mungu amesikia; Ameisikiliza sauti ya maombi yangu.  Na ahimidiwe Mungu asiyeyakataa maombi yangu, Wala kuniondolea fadhili zake. Mara nyingi sana Maombi yetu hayapati kibali mbele ya macho ya Mungu kwa sababu tunadhambi ambazo zinatakiwa tuziungame na tuache kuishi katika dhambi ili sala na maombi yetu yapate kibali cha Mungu. Tukitimiza hayo Mungu anaweza jibu maombi yetu kwa kadiri na namna ambayo sisi tumemwomba; lakini jibu lake llinaweza lisije kaulingana na kalenda ya mwombaji, anaweza hata tumia njia ya kuchelewesha kidogo ili kutufundisha sisi subira,unyenyekevu na upole. Kusubiri ni fadhila moja kubwa sana katika maombi yetu.

Tafakari yetu vile vile inatukumbusha kuwa tunaye mpatanishi ambaye anatuombea kwa Baba na hivyo ni wajibu wetu kuomba kupitia yeye Mathayo 7:7-8 inavyotukimbusha Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. Ili tufanikiwe katika hili tusijenge tabia ya kumaliza ombi letu kwa kutaja tu jina Yesu mwisho wa maombi yetu; bali tunatakiwa kuishi maisha ya utakatifu ili sala zetu zipate kibali; lazima tuishi katika mapenzi ya Mungu. Jambo nyingine lakuzingatia ili maombi yetu yapate kibali cha Mungu ni kuhakikisha kuwa kwa wale wote wako kwenye ndoa wajue kuwa mahusuiano yao mazuri na utii miongoni mwao ni kibali kikubwa katika usikivu wa maombi yetu; 1 Petro 3:7 Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.

Tumalizie tafakari yetu kwa kukumbuka tujijengee tabia ya ushindi kwa kuzingatia matendo yetu mema, maisha bora yanyompendeza Mungu; Kutimiza wajibu wetu ipasavyo katika jamii tukiendelea kuamini kuwa Mungu ndiye mwenye mamlaka na ndiye mwenye mamlaka na pekee ndiye jibu la shida zetu kama Mtume Paulo 2 Wakorinto 12:8-10 aliposema Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke. Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.  Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu. Mungu anatupenda sana na daima anajibu kwa wakati wake ambao ndio wakati muafaka ambao unapita uelewa wa akili zetu.

Hii ndio tafakari yetu ya leo. Amina


Emmanuel Turuka

No comments:

Post a Comment