WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Monday, June 20, 2016

MUWE WAMOJA KAMA SISI TULIVYO:


June 20

Yohana 17: 1-5

Tafakari yetu ya leo inatukumbusha ombi ambalo Yesu, aliwaombea mitume wake wawe na umoja kama wao walivyo katika ufalme wa mbinguni. Yesu aliwakumbusha mitume wake bila kujali khali zao, wametoka wapi; wana nini wanapaswa kuwa wamoja. Tafakari yetu inatukumbusha kuwa watu wa mungu  wametoka kutoka makabila yote; lugha zote;mataifa yote;katika khali tofauti za uchumi. Ndio maana Yesu aliwaombea wafuasi wake wawe na Umoja kama wao walivyo. Tunatoka katika mazingira tofauti lakini wote ni zao lake yeye; tunajitenga na kuchukiana kwa sababu za tofauti zetu na mazingira ambayo tunajijengea miongoni mwetu; mungu anataka sisi kushirikiana pamoja kwa upendo wote;

Tafakri yetu leo inatumumbusha kuwa tunatakiwa kufikiria katika akili zetu kuwa  mimi ndio natakiwa kuwa sababu ya umoja wetu; natakiwa nititoe kwako, niwe nawe na nishiriki nawe katika yale yote ambayo yameelezwa katika  amri ile kuu ya upendo; kuwa Mkristo wa kweli na sio wa kuhudhuria katika makanisa ni kuishi amri hii ya upendo kwa vitendo; na tukiishi kwa vitendo ndipo tutatekeleza maana ya kuwa Mfuasi wa kristo; tukumbuke kuwa zawadi zote ambazo Mungu ametupa sisi, zawadi za Muda, zawadi ya Nguvu, afya njema Mungu ametujalia sisi lakini anataka zawadi hizi tuzitumie kwa manufaa ya wengine pia; heshima ambayo sisi tunatamani kuwa nayo ndio iwe hsehima hiyo hiyo ambayo tunapaswa tuionyeshe na kwa wengine; tunapaswa kushauriana; inatupasa kutiana moyo; yatupasa kushirikiana kwa Yesu alivyotenda kwetu; Yesu daima anataka sisi tuwe chumvi ambayo inaleta radha nzuri katika chakula. Wafilipi 2:2 ijalizeni furaha yangu, ili mwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, nia moja. 

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa Jamii yetu leo kuwa ukweli sio kitu ambacho kinapewa thamani ya kweli; Mungu katika mafundisho yake ukweli mmeweka kuwa msingi wa kila kitu; tukiangalia zaburi ya 51:6 Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni; Nawe utanijulisha hekima kwa siri, au Zaburi ya 86:11 Ee Bwana, unifundishe njia yako; Nitakwenda katika kweli yako; Moyo wangu na ufurahi kulicha jina lako; Wafilipi Ufunuo 21: 27 Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.

Yesu alituombea tuwe na umoja akijua kuwa palipo na umoja ukweli hutawala na amani itadumu, na palipo na ukweli na umoja unyenyekevu utatawala uwazi wa mambo ya msingi yahusuyo amani yatafanyika, na mashauriano mema yatafanyika kwa upendo mkubwa; ndio maana yesu alitaka tuwe wamoja tukiwa wamoja tutashirikiana kwa ukaribu zaidi. Tutapendana na hata pale ambapo hatutakubaliana tutamaliza tofauti zetu kwa upendo na hekima ya kweli. Yesu anatufundisha kuwa Maisha ya Mkristo ni mchanganyiko wa vitu viwili yaani machungu na furaha; katika machungu maisha yanakuwa yamegubikwa na mambo mengi ambayo yamejaa masikitiko, taabu na mateso kwa baadhi ya yetu na wengine wakifurahi maisha yalijaa furaha na starehe. Tukisoma Warumi 8:28 inatukumbusha kuwa Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. Hivyo sisi sote pamoja na taabu zetu na furaha zetu Mungu ametuita tuwe pamoja naye, Ndio maana yesu alituombea tuwe wa moja katika umoja wetu tutaweza kusaidiana katika kyakabili maisha katika khali yeyote ile;

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa katika umoja wetu hakuna magumu. Bali neema ya Mungu ndio silaha ya kweli katika kupambana na majaribu yeyote yale. 2 Wakorinto 12:9-10  inatukumbusha kuwa Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu. Pasipo na umoja ni karibisho la udhaifu; bali tukiishia katiaka umoja tunajenga nguvu ya ushindi. Ombi la Yesu aliloomba juu wa wafuasi wake lilikuwa la maana na msingi mkubwa akitambua kuwa mitume wake walikuwa ni watu wenye uwakilishi tofauti, utu tofuti na walikuwa wamekulia katika mazingira Tofauti, walikuwa wengine ni wapole, waaminifu, wengine ambao walikuwa tayari kwa shari; hivyo ombi lake juu yetu likuwa ni msingi mkubwa;

Yohana 17; 20-26 inavyotukumbusha Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli.  Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakao niamini kwa sababu ya neno lao.  Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.  Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja.  Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.  Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami po pote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu.  Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua; lakini mimi nalikujua, na hao wamejua ya kuwa ndiwe uliyenituma.  Nami naliwajulisha jina lako, tena nitawajulisha hilo; ili pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, nami niwe ndani yao. Umoja ni silaha muhimu sana katika imani yetu.

Hii ndio tafakari yetu ya leo Amina

Emmanuel Turuka


No comments:

Post a Comment