WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Saturday, June 18, 2016

NAWATUMA - MKIKARIBISHWA INGIENI

June 18


Tafakari ya leo tujikumbushe jinsi Yesu alipowatuma wale sabini na wawili na kuwaagiza kuwa Mathayo 10:8-23  Afadhali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.  

Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia.  Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.  

Msichukue dhahabu, wala fedha, wala mapesa mishipini mwenu;  wala mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala viatu, wala fimbo; maana mtenda kazi astahili posho lake.  Na mji wo wote au kijiji cho chote mtakachoingia, tafuteni ni nani humo aliye mtu mwaminifu; mkae kwake hata mtakapotoka.  

Nanyi mkiingia katika nyumba isalimuni.  Na nyumba ile ikistahili, amani yenu na iifikilie; la, kwamba haistahili, amani yenu na iwarudie ninyi.  Na mtu asipowakaribisha wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule, kung'uteni mavumbi ya miguuni mwenu.  

Amin, nawaambia, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma na Gomora kustahimili adhabu ya siku ya hukumu, kuliko mji ule.  Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.  

Jihadharini na wanadamu; kwa maana watawapeleka mabarazani, na katika masinagogi yao watawapiga;  nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa.  Lakini hapo watakapowapeleka, 

msifikiri-fikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema.  Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu.  Na ndugu atamsaliti nduguye ili auawe, na baba atamsaliti mwana, na wana watawainukia wazazi wao, na kuwafisha. 

 Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.  Lakini watakapowafukuza katika mji huu, kimbilieni mwingine; kwa maana ni kweli nawaambia, Hamtaimaliza miji ya Israeli, hata ajapo Mwana wa Adamu. 

No comments:

Post a Comment