WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Saturday, June 11, 2016

TAABU NA MAUMIVU YANATUFUNDISHA SISI CHOCHOTE?


June 11

2 wakorinto 12: 7-10


Tafakari ya leo tunaangalia jinsi maumivu katika maisha yetu kama yanakuwa na fundisho lolote au yanaishia tu kuwa maumivu ambayo yanafanya maisha yetu kuwa magumu na ya kusikitisha. Tunajifunza kutoka kwa Mtume Paulo jinsi ambavyo alivyokuwa akikumbana na maumivu wakati alipokuwa akihubiri neno la Mungu kwa mataifa tukisoma waraka wa 2 Wakorinto 11:25-27 Paulo anatukumbusha kuwa Taabu na maumivu hatuwezi kuyakwepa katika kutafuta uzima wa milele na maisha bora ya baadae; Mara tatu nalipigwa kwa bakora; mara moja nalipigwa kwa mawe; mara tatu nalivunjikiwa jahazi; kuchwa kucha nimepata kukaa kilindini;  katika kusafiri mara nyingi; hatari za mito; hatari za wanyang'anyi; hatari kwa taifa langu; hatari kwa mataifa mengine; hatari za mjini; hatari za jangwani; hatari za baharini; hatari kwa ndugu za uongo;  katika taabu na masumbufu; katika kukesha mara nyingi; katika njaa na kiu; katika kufunga mara nyingi; katika baridi na kuwa uchi. Hivi vyote hatuwezi kuvikwepa;

Tafakari yetu leo inatukumbusha hata ndani ya familia zetu tabu na maumivu tunakabiliana nazo; lakini tunatakiwa hizo changamoto tuweze kuzikabili vizuri na kuzishinda kwa ufanisi kwa kuzingatia neno la Mungu; katika familia zetu tunakabiliwa na maumivu yatokanayo na magonjwa; maumivu yatokanayo na maisha kama maisha ya ndoa; khali ngumu ya maisha kutokana na umasikini; kama Mtume Paulo alivyomwomba Mungu amwondolee maumivu na Taabu ili aweze kufanya kazi ya uchungaji zaidi lakini Mungu alimjibu kwa namna tofauti kwani kutokana na taabu na maumivu watu wengi waliokolewa na kumrudia Mungu. Yesu alipata Tabu na maaumivu aliposulubiwa msalabani.

Tafakari yetu ya leo kama ilivyokuwa kwa Mtume Paulo tulio wengi hatuoni dhumuni la taabu na muumivu mwanzoni; tunatakiwa tuombe neema ya kutambua taabu na maumivu yetu kupitia jicho la mungu toka mwanzo ili tuweze kusherekea utukufu wa Mungu kwa dhumuni ambalo ameliweka katika shida zetu; Tunatakiwa kuimarisha imani yetu kwani Imani inamchango mkubwa sana katika taabu na maumivu; tunatakiwa kumwomba Mungu atuonyeshe dhumuni la taabu na maumivu, na kutuimarisha ili kutuwezesha kuzikabili hizo changamoto zote;

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa Maumivu na taabu yana nguvu sana kama Paulo alivyosema neema yangu inatosha katika madhaifu na mapungufu yetu. Hivyo tunatakiwa keweka neema ya Mungu mbele na ili tuone dhumuni la maaumivu na taabu ili tupate nafuu; Mauumivu na Taabu ni kama taa za taadhari ambazo zinaashiria kuwa kuna jambo linaweza kutokea kama hatutakuwa makini katika maisha yetu; hatutakiwi kudharau taa hizo hivyo haitupasi kudharau maumivu na shida zetu bali tutafute neema ya Mungu katika kujua sababu ya Maumivu na tabu zetu kwa utukufu wa Mungu;

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa wakati mwingine maumivu na taabu huwa ni chachu za mabadiliko ambayo Mungu hutaka sisi tuyapitie; tukumbuke kuwa Mungu ni Yule Yule; Mungu hataki watu tupate taabu na maumivu lakini wakti mwingine anafanya katika kutujengea nidhamu; kutufundisha na kutuongoza sisi tupite katika njia ambayo ni sahihi; sio kuwa Mungu ana hasira au hatupendi bali anatupenda sana na kutujali; Tatizo letu sisi hatuko tayari kubadilika hata katika Maumivu na Taabu zetu.

Tafakari yetu inatunyoshea kidole kuwa sasa ni wakati wa kubadilika na kusisma imara ili kujiepusha na maumivu na taabu;
Hii ndio tafakari yetu ya Leo – Amina

Emmanuel Turuka









No comments:

Post a Comment