WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Wednesday, June 15, 2016

NITUME MIMI BWANA


June 16

Isaya  6:8

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa katika maisha yetu sasa je tu sisi tuko tayari kama Isaya alivyo mwambia Mungu  Kisha nikaisikia sauti ya Bwana, akisema, Nimtume nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu? Ndipo niliposema, Mimi hapa, nitume mimi. Mungu alikuwa anatafuta mtu ambaye atakuwa mwakilishi wake, karani wake ambaye atakuwa ataweza kutawanya ujumbe wake kwa mataifa. Ujumbe wa amani , ujumbe wa matumaini, ujumbe wa upendo; bila wasiwasi na kusita Isaya alimwambia Mungu Mimi hapa nitume; isaya kwa kukubali aliweza kuona nguvu ya ajabu ya mungu  na utataktifu wa Mungu; aliweza kuzisafisha kabisa dhambi zake na kumfanya aweze kwenda kokote na kuhubiri neno la Mungu. Kumbuka lile kaa la moto ambalo liligusa midomo ya Isaya, midomo ya Isaya ilikuwa yenye dhambi hivyo kwa kaa la moto la kimungu lilisafisha dhambi zilizokuwa katika midomo yake ili aweze sasa kutangaza ukweli wa Mungu.

Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa Mungu bado anataka mimi na wewe leo tuwe miongoni mwa wale ambao amewaita na kama ilivyokuwa kwa isaya basi tusisite au kuwa na mashaka ya kukubali wito huo; tunatakiwa leo hii kuweka imani yetu kwa Yesu tukishukuru kuwa kwa damu yake sisi tumesafisha na kuondolewa dhambi zetu; Lazima tuendelee kutafakari kuwa tunatakiwa kumrudia Mungu, na kufuata sheria zake na sio kuendelea kuishi kwa namna na jinsi ambavyo tunaona sisi inatupendeza kwa kuendelea kufanya hivyo tutatengwa na Baraka na upendo wa Mungu; Gharama ya kufanya mambo kwa namna ambayo sisi tunataka ni kubwa sana. Tunamwitaji Mungu na Mungu anatuhitaji sisi ili tuweze kutangaza neno lake na kufikisha ujumbe wa upendo kwa mataifa. Tukumbuke  bila nguvu ya Mungu maisha yetu yatendelea kujaa ushetani wa ajabu na wa kutisha.

Tafakari yetu ya leo inatukumbusha kuwa kwa kupitia Malaki 3:6 Kwa kuwa mimi, Bwana, sina kigeugeu; ndio maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo. Mungu yuko vile vile kama Isaya alivyomwona. Bahati mbaya wengi wetu hatujewahi kupata maono kama alivyoshuhudia  Isaya. Hatujemwona Mungu lakini kama tutakubali wito wake wa kutangaza neno lake tutamwona Mungu katika karamu ya mwisho. Mungu anakuita leo kwani anajua kuwa kuna watu wengi ambao wanatamani kusikia neno lake liletalo faraja lakini wewe na mimi bado hatujeitikia wito wa Mungu na kusema MIMI HAPA; NITUME MIMI: NITUME BWANA.

Tafakari yetu tuhitimishe kwa maneno haya Isaya 6:4-8 Ndipo niliposema, Ole wangu! Kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, Bwana wa majeshi. Kisha mmoja wa maserafi wale akaruka akanikaribia; naye alikuwa na kaa la moto mkononi mwake, ambalo alikuwa amelitwaa kwa makoleo toka juu ya madhabahu;  akanigusa kinywa changu kwa kaa hilo, akaniambia, Tazama, hili limekugusa midomo yako, na uovu wako umeondolewa, na dhambi yako imefunikwa.  Kisha nikaisikia sauti ya Bwana, akisema, Nimtume nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu? Ndipo niliposema, Mimi hapa, nitume mimi. 

Hii ndiyo Tafakari yetu ya Leo  Amina

Emmanuel Turuka

No comments:

Post a Comment