WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Monday, June 13, 2016

YATUPASA KUANGALIA KABLA YA KURUKA




June 13

Yakobo 1:19

Tafakari yetu leo inatukumbusha kuchukua taadhari kabla hatujechukua hatua yeyote muhimu ambayo inayahusisha maisha yetu kwa ujumla; kwani kama hatutachukua taadhari tutaishia kupata maumivu na sio faraja ambayo kama tunaitegemea katika maisha yetu;  Taadhari hii tukiifuata inavyopasa itatusaidia katika  katika maisha yetu ya kila siku na maandalizi yetu na mungu. Mfano wa kawaida tu ni kuwa kama tunachukua taadhari na kupata nafasi ya kusikiliza  nini watu wengine wanatuambia na tukawapa nafasi ya kutosha watatusimulia mambo mengi kuhusuwao wenyewe; lakini kama tutakwa wavumilivu, na wasikivu zaidi watakusimulia mambo ya ndani zaidi ambayo hata hukutarajia kuyasikia. Na hivyo pengine ukapata nafasi ya kumsaidia mtu zaidi, kwa sababu tu umechukua taadhari, hujekurupuka kumkatisha katika maelezo ya shida yake, hivyo umemwelewa sana na unakuwa umepata nafasi nzuri ya kumsaidia.

Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa tusipokuwa makini kila kitu tukifanyacho au tunachokifikiria kinaweza kuwa na mwisho mbaya; hata vitu ambavyo tayari vimetayarishwa kwa ajili ya matumizi au kutusaidia sisi wenyewe; Kama vitu au mawazo yetu hatutaytumia kwa namna inayofaa. Mwamba mdogo tu katikati ya bahari unaweza kusababisha madhara makubwa kama Nahodha akuwa makini wakati alipokuwa akiangali na kuendesha chombo chake; hivyo yatupasa kuwa makini tukikumbuka kuwa kila kitu hata kama ni kidogo bado vina umuhimu mkubwa sana. Kwa hiyo yatupasa kuchukua taadhari katika kufanya maamuzi yetu kwani kila kitu ni muhimu. Hivyo yatupasa kuwa makini kama 1Petro 5:8 anavyo tufundisha Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze. 

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa lazima tutumie busara na hekima katika maamuzi yetu kama kitabu cha mithali14:15 kinavyofundisha Mjinga huamini kila neno; Bali mwenye busara huangalia sana aendavyo. Kwa kutafakari na kuchukua taadhari kabla ya kufanya maamuzi ni jambo la hekima kubwa; hekima hiyo ndio tunayoihitaji sana katika masia yetu ya kila siku; Busara na hekima yetu itatufanya sisi kuwa na msimamo na kufanya maamuzi sahihi kama Paulo alivyosema katika waraka wake kwa Waefeso 4:14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. 

Tafakari inatuonya kuacha kuwa wazembe na wazivu katika kuchambua. Kufuatilia, kuangalia na kusikiliza ili mawazo na matendo yetu yaweze kulingana na faida ambayo tunaisubiria kwa hamu kubwa , na sio kukurupuka na kujikuta tukiishia kwenye korongo kwa kushindwa kuangalia na kupima hitaji linalohitajika kabla ya kufanya maamuzi. Tumejaliwa elimu na maarifa katika kutekeleza majukumu yetu; bibili ni chanzo kizuri sana cha maarifa na kina dhana zote nzuri za kutusaidia kuweza kuruka bila kupata athari yeyote ile; au kusikiliza bila kupata hasiri; lakini mwenyezi Mungu bado ametuachia maamuzi ya kufanya mambo yetu kwa busara na hekima bado yako juu yetu; ni wakati sasa umefika wa kubadilika na kutumia busara na taatdari katika maamuzi yetu yote;

Hii ndio tafakari yetu ya Leo Amina


Emmanuel Turuka

No comments:

Post a Comment