WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Tuesday, June 21, 2016

JE YATUPASA KUISHI KWA MASHAKA?



June 21

Matthew 11:2-3

Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa kama nina amini na kwa nina wasiwasi? Tukiangalia katika mazingira tofauti tofauti simulizi katika vitabu vya  Ayubu, Mhubiri, maombolezo, zaburi na Habakuki vyote katia mazingira tofatuti vimegusia dhana ya mashaka kwa hisia kuwa Mungu alikuwa amewaacha katika shida zao; Katika mazingira ya maisha ya kuwa Mfuasi wa Kristo ni wazi kuwa dhana ya kuwa na mashaka ni jambo la kawaida; tukumbuke kuwa hata imani ili iweze kuimarika yatupasa kuwa mashaka ili kukomaza imani hiyo; kama wataalamu wengi walivyopata ongea kuwa kama utakuwa na wasiwasi basi utakuwa umefika katika mahali ambapo pa mwisho kabisa katika imani na mahali hapo ni mbinguni.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa mashaka /wasiwasi tunaweza vielezea katika makundi makuu matatu; kuna wasiwasi ambayo inaletwa na wasomi ambao wao mashaka yao wanayaelekeza nje ya imani yetu, wakiuliza Mungu kweli yuko? Je bibilia ni neno la Mungu? Kweli yesu ni mwana wa Mungu? Ni kweli kuwa Yesu alifufuka? Kundi la pili la wenye mashaka ni wale ambao ni washiriki katika makanisa yetu; ambao wanajiuliza kama kweli wao ni wakristo kweli? Je kweli wananamini? Kwa nini bado najisikia mdhambi? Kwa nini inachukua muda mrefu kwangu kufanikiwa kupona, au shida yangu kutatuliwa. Na kundi la tatu wale ambao mashaka yao yanalengwa na swali kwa nini? Kwa nini mototo wangu alikufa? Kwa nini ndoa yangu imevunyika? Kwa nini sipati Mume? Kwa nini marafiki zangu wananisaliti; Mungu alikuwa wapi wakati Mjomba wangu aliponibaka? Haya ni maswali machache kati ya mengi; tunachokiona hapa ni mwingiliana wa imani na maumivu ambayo yanapatikana katika maisha na kuleta mashaka na tatizo ni pale sasa majibu hayapatikani hata wale wahusika ambao wako ndani ya kanisa ambao walitakiwa kusaidia kuondoa mashaka haya nao wanamua kudharau na kuto kutoa msada wa ufafanuzi mzuri ambao unamjenga mtu kiimani zaidi na kuweza kuondoa mashaka ya namna hii. Kwa kushindwa kuyapatia ufumbuzi maswali kama haya ndio mashaka ya kiimani au mashaka ya kiroho huanza kujitokeza na watu wananza kukimbia kanisa.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa watu wengi wanafikiri kuwa kuwa na mashaka ni kukosa imani; lakini kwa ujumla wake sio kweli isipokuwa kama wewe huamini hivyo huna imani; kwa asiye amini ni tendo la makusudi na lililo kusudiwa; lakini kuwa na mashaka ni  kuwa na mashaka ya ndani ya nafsi yako; mshaka yanasemehewa na mungu hatuazibu sisi tunapo jiuliza maswali mengi kuhusu yeye; tuwakumbuke Ayubu na Daudi mara kadhaa walikuwa wanajiuliza maswali mengi kuhusu Mungu lakini hata hawakuwalaani; Uwezo wa mungu ni wa ajabu kutatua mashaka yetu na maswali yote yenye mashaka juu yake; watu wengi wanafikiri jinsi tunavyo jiuliza maswali mengi kuhusu Mungu kwamba hatuna imani la hasha tukumbuke kuwa bila kuwa na mashaka imani yetu haitakuwa inavyotakiwa.

Tafakari yetu inaendelea kufafanua kuhusu mashaka kwa kuangalia mfano kutoka Mathayo 11:2-3 Naye Yohana aliposikia huko gerezani matendo yake Kristo, alituma wanafunzi wake, kumwuliza,  Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine? Hili ni swali lenye nguvu sana; cha kujiuliza hapa masha ya Yohana Mbatizaji yanatokea wapi; kumbuku kuwa yeye wenyewe huko nyuma alishakiri kumjua Kristo kama masiha; ukisoma Yohana 1: Yohana akawajibu akisema, Mimi nabatiza kwa maji. Katikati yenu amesimama yeye msiyemjua ninyi. Ndiye yule ajaye nyuma yangu, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya kiatu chake.  Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!  Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Yuaja mtu nyuma yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu.  Wala mimi sikumjua; lakini kusudi adhihirishwe kwa Israeli ndiyo maana mimi nalikuja nikibatiza kwa maji....  Nami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa huyu ni Mwana wa Mungu.

Akamtazama Yesu akitembea, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu!  Kwa maelezo haya toka injili ya Yohana: Yohana Mbatizaji alikuwa anamjua Yesu kuwa ni nani; lakini swali la kujiuliza ni hili kwa nini mtu ambaye alimfahamu sana Yesu aliishika kuwa na Mashaka na mafundisho yake? Lakini tukumbuke kuwa watu wenye mashaka ndio wanaokuwa watu wenye imani kubwa sana.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa Mungu yuko tayari  kutatua mashaka yote; kuondoa woga; na kukujibu maswali yote ambayo unafikiria kuwa hayana majibu; anatawala mbingu na dunia bila msaada; tujue kuwa mashaka yetu kamwe hayamletei hasiara yeyote; yeye ni Mungu wetu sote katika khali yeyote ile; tunachopaswa kufanya ni kuishi na kutekeleza majukumu yetu kwa Imani tumkumbuke Noha alipokuwa akijenga safina alitenda kwa Imani; Abrahamu alipo acha ur na kwenda Chaldees alifanya kwa imani bila mashaka; Abrahamu alipotakiwa kumtolea sadaka Isaki alifanya kwa Imani bila mashaka; tunakumbuka Kisa cha Musa na  alipotembea na wana wa Israeli katika ya Bahari ya shamu kwa imani na sio mashaka; mwangalie samweli alipotupwa katikati ya samba alikuwa na imani zaidi na sio mashaka. Hivyo pamoja na mashaka yetu bali tunatakiwa kutanguliza imani zaidi na kutenda kwa imani na sio mashaka;

Hii ndio tafakari yetu ya leo – Amina-


Emmanuel Turuka

No comments:

Post a Comment