SIKU 1: JANUARY 1, 2019
Waebrania 11:1,3
Warumi 10:17
Kheri ya Mwaka mpya 2019: Leo naomba kuwakaribisha katika mwendelezo wa siku nyingine 365 ambapo tutaangalia Akisi ya Imani katika maisha yetu kama wakristo;
Imani ndio msingi wa kwanza wa mkristo
Imani ina umuhimu mkubwa katika maisha Yetu ya kiroho kama mkristo
Imani ni muhimu sana katika kuimarisha sheria ya Mungu. Na kwa upande mwingine Kufuata amri za Mungu ndiyo njia bora ya kujenga imani yetu
Mtitiriko wake ni kuwa Tunapoishi kulingana na amri hizo, tunaona wazi zaidi kwamba zina mwongozo wenye upendo ambao ni kielelezo cha imani:
Mtume Paulo katika Waebrania 11:1,3 anasema kuwa Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Jambo la pili imani huhusisha usikivu kama Paulo anavyotukumbusha katika
Warumi 10:17, chanzo cha imani ni kusikia. Imani katika Kristo inakuja kwa kusikia:
Je unapenda kusikia Habari Za kristo au Habari za shetani:
Tunakumbuka tukisoma Mwanzo 3:1-8 jinsi nguvu ya kusikia ilivyo haribu nguvu na baraka zote walizopata
Adam na Hawa katika bustani ya Edeni.
Huu ni utangulizi tu katika Safari yetu ya Akisi ya Imani kwa mwaka huu 2019:
Kama utakuwa na nafasi Karibu sana nitaweza kukutumia mfululizo huu:
Na kama hutakuwa na nafasi katika Safari hii ya kiroho:
Nawatakieni kheri na fanaka kwa kuvuka salama mkiwa na afya njema;
Emmanuel Turuka
Kalamazoo MI
2019
No comments:
Post a Comment