JANUARY 3. 2019
IMANI NA MASHAKA VINAPO NGONGANA
MARKO 9: 14-24
WAEBRANIA 12:1
Kama tulivyoona katika masomo yaliyopita kuwa Imani hufanya Kazi yake vizuri sana pale ambapo mashaka hakuna :
Mashaka ni adui mkubwa sana wa Imani: Lakini Imani ya kibibilia inahimili mashaka;
Tukumbuke kuwa Mungu anapenda Sisi kumtumaini yeye katika kila jambo katika maisha Yetu yote: Hivyo hata katika mashaka Mungu Bado anatuopoa sisi kama alivyomwopoa Petro:
Tukisoma Mathayo 14: 29 Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu.
Tukumbuke kitendo cha Petro kuyaangalia maji na dhoruba yalimjengea mashaka; Lakini tukubali ukweli huu Kitendo cha Petro kushuka kutoka kwenye mashua na kuwa tayari kutembea juu ya maji ni uwepo wa imani ya kweli mbele ya Yesu :
Tukumbuke kuwa mashaka kama yaliyompata Petro sio kuwa Petro alikuwa hana Imani kabisa isipokuwa imani yake ilitoweka kufuatia mazingira ambayo yalikuwa mbele yake baada ya kupoteza umakini wa wapi aangalie na nani amemwambia ashuke kwenye Chimborazo:
Kwa kupoteza mwelekeo akaanza kuzama: Mathayo 14:31 Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka?
Wengi wetu tuko kwenye kundi la Petro na ukristo wetu: la kutoamini katika njia inayotakiwa ya kuamini kuanzia mwanzo wa tukio mpaka Mwisho wake:
Tumkumbuke Tomaso hakuamini kuwa Yesu amefufuka na amewatokea mitume wenzake: Sio kuwa Tomaso alikuwa hajui nguvu za Yesu lakini mazingira ambayo Yesu alikufa na kuzikwa yalimpa wasiwasi mkubwa hata alipopata taarifa kuwa amefufuka na wamemwona hakuweza amini:
Tomaso aliona jinsi Yesu alivyokuwa alifanya miujiza yote ile lakini Bado alikuwa amejawa na mashaka tunakumuka jinsi Yesu alivyomwambia Tomaso tukisoma; Yohana 20:27 Kisha akamwambia Tomaso, Lete hapa kidole chako; uitazame mikono yangu; ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu, wala usiwe asiyeamini, bali aaminiye.
Tukumbuke kuwa kuamini ni rahisi sana lakini kuishi katika uhalisia wa kuamini ni kazi nzito: wakati mwingine nafasi katika jamii: uwezo wa kifedha; uwezo wa maarifa na kadhalika unaweza kubomoa Imani yako kama Mkristo:
Methali 3:5–6. Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; 6 Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.
Kumweka mashaka katika ukristo wetu ni kujirudisha nyuma katika imani ambayo Mungu kaiweka kwetu kupitia Mwanae Yesu Kristo: Ndio maana katika Injili ya Yohana Yesu anaongelea sana Imani Imani Imani;
Yesu anataka Sisi tutue mzigo mzito tulioubeba ulioja mashaka; Anataka Sisi tumwamini Yeye; Ndio maana amesisitiza sana kuwa Yeye ni njia na uzima: yeye ni maji ya uzima: Yeye ni mkate wa uzima na kadhalika;
Leo tuamue kuwa ni wakati umefika wa kutua huu mizigo mzito wa mashaka: Mashaka katika imani isiwe kikwazo katika Mbio za kutenda miujiza: tumtumiini yeye naye atakuwa nasi: Waebrania 12:2 tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.
Tukumbuke kuwa hatuwezi kuishi Imani ya ukristo kama hata Mungu tunamwonea mashaka; Leo jiangalie wewe kama Mkristo ambaye mkono wa Mungu umekubariki na kukupitisha katika Magumu mengi na kukupatia faraja: na Bado baada ya kuvushwa na kupata Mafanikio Bado wamekuwa na mashaka na Mungu:
Ni wajibu wetu Leo kuipokea Imani na kuishi ili tuweze kutenda Kazi ya Mungu Kwa uhakika wote na kuweza kufanya miujiza:
Amina 🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿Amina
Emmanuel Turuka
Kalamazoo MI
2019
No comments:
Post a Comment