WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Sunday, December 5, 2010

nasema asante - Sarah K



NENO ASANTE LINA MAANA KUBWA SANA KATIKA MAISHA YETU 

Nasema asante kwa maisha, familia bora ambayo ninayo, kwa wazazi wazuri ambao tunao, kwa upendeleo ambao Mwenyezi Mungu amekuwa akitujalia kila siku ipitayo ya maisha yetu; Mungu ni mwema na Mungu ni mwenye huruma na upendo mkubwa sana kwetu.

Ukuu wa Mungu, ni wa kushukuriwa kila siku na kila sekunde; mafanikio haya yote ni kwa sababu yake; kama unaungana nami katika kuona ukuu wa Mungu kwa nini basi tunakuwa wagumu  kusema asante?

Jiulize katika mwaka huu je Mwenyezi Mungu amekuepusha na mambo mangapi mabaya ambayo yange kuangamiza kimwili na kiroho? Je umekuwa ni mtu wa shukrani au wa kulalamika tu kila siku? Je umekuwa ni msamaria mwema kwa wale wenye hitaji la ukweli  au unawasaidia tu wale ambao unafahamu watakusaidia na wewe  ukiwa na shida?

Mwenyezi Mungu ametuepusha na  mengi na anaendelea kutuepusha na mengi basi tumshukuru kwa kusema asante tusiwe kama wale Wakoma Tisa ambao hawakumbuka kurudi na kusema asante kwa kutakaswa         ( kuponywa). Basi naomba uungane nami katika kufanya tafakari ya maisha yako na nafasi ya Mungu kwako kwa jinsi ambavyo amekupendelea katika maisha yako mpaka hapa ulipofikia leo. swali baada ya kutafakari kwa nini usiungane nami kumshukuru Mungu ukisindikiwa na wimbo huu wa dada yetu Sarah.

Amina

No comments:

Post a Comment