WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Monday, January 18, 2016

JE WEWE NI SEHEMU YA AMANI



January 18

Tafakari ya leo tuangalie jinsi bibilia ilivyohubiri amani; swali la msingi ambalo mimi najiuliza nani anatawala dunia yetu leo? Jibu ni rahisi tu amani ya bwana ndio inayotawala dunia yetu hii kwa wale ambao wanaamini; yesu aliwaambia mitume wake amani yangu nawaachia, sio tu amani bali ni amani yake YESU; kama utaweza kupokea amani ya bwana utaweza kuishi maisha mazuri sana yenye utulivu wa kihoro na kimwili; na hiyo amani itakuwwezesha wewe kuishi kwa nguvu ya Kimungu.

Amani  iletwayo na Yesu ni ajabu kwani imejaa neema na matumaini; kwani mwenye Matumaini huongozwa na Mungu ambaye analindwa na hila za adui; nakumbuka nilipokuwa mdogo giza lilipokuwa likiingia na nilipokuwa natumwa kwenda kuchukua kuti chochote nilikuwa naogopa nilikuwa sina amani na daima niliomba ulinzi wa kunisindikizwa. Na nilipoulizwa nilijibu kuwa giza ni nene hivyo nahitaji mssada. Hivyo nilikuwa sina amani wala matumaini; Lakini Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa tukiwa na amani ya Bwana hatutaogopa chochote kwani tayari tupo ndani ya ulinzi wa Mungu.

Tukisoma warumi 14.19 paulo basi kama ni hivyo na mfuate mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana. Ni jukumu letu kuitafuta amani na kuitetea kwa faida ya wote, lakini inakuwa ni rahisi kama amani yako itakuwa ni za la kristo Yesu;

Zaburi ya 119:165, 167 inasema wana wa amani nyingi waipenda sheria yako, wala hawana la kuwakwaza; ndipo tutakaposifu na kusema nafasi yangu imezishikashuhuda zako name nazipenda mno. Hivyo yatupasa kukumbuka kuwa mungu yu daima juu yetu na uwepo wake ndio chanzo cha amani yetu. Tunatimiza uwepo wa Mungu pale tunapo yaelekeza mawazo yetu mazuri juu yake na amri zake katika utekelezaji wa majukumu yetu ya kila siku. Lakini tuka kuumbwa kwa dunia Mungu ametupa uhuru wa kuchagua kumtegemea yeye katika yetu au kuendelea kuhangaika na matatizo yetu. Tukumbuke kuwa nani ameshikilia suluhu la matatizo yetu?

Hata pale ambapo matatizo ambayo yako mbele yetu hayaeleweki bado tunatakiwa tumtumaini Mungu ambaye yey ndio asili ya amani ya fikra zetu; tukumbuke kitabu cha Methali 3:5 -6 mtumaini bwana kwa moyo wako wote wala usizitegemee akili zako mwenyewe. Katika njia zako zote mkiri yeye naye atayanyosha mapito yako. Ndio katika maisha yetu ya kila siku mambo mengi yako nje ya uwezo wetu na ndio asili ya kuvunjika kwa amani. La msingi tusijaribu kuhangaika kupata suluhu ya mambo pasipo Mungu. Tukumbuke kuwa bila uwepo na nguvu yake mungu tunapoteza nguvu nyingi katika kutafuta amani ya kweli ndani ya maisha yetu. Tumesahau kuwa tunatakiwa tukae kwa furaha tukijua kuwa Mungu tayari anatembea nasi siku zote kama tukizikaribisha sheria zake na kuzitekeleza kwa maelekezo yake.
Mtume Paulo kwa Wafilipi 4:6-7 msijisumbue ka neon lolote; bali katika kila neon kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo yesu.

Je ni kitu gani tunatamani kumwuliza Mungu sasa hivi? Je unatamani yeye aje ndani ya maisha yako ili uweze kufurahia amani yake: ili ikusaidie wewe uweze kufurahia amani iel ya milele yote?


Nini kinaharibu amani yetu leo? Ni dhana ya kujisikia mkosaji na kama hii ndio kweli umemkosea nani? Amani ya kweli inaletwa na upendo wa kweli miongoni mwetu; Tumefundishwa kuwa tuwapende wenzetu kama tunavyojipenda kwani kipimo kile kile ambacho tunamtendea mmoja wetu ndicho kitakuwa kipimo chetu. Tutafakari Pamoja siku hii ya leo kuwa je wewe ni kwa namna gani unahubiri amani?

No comments:

Post a Comment