WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Friday, January 1, 2016

TAFAKARI YA KILA SIKU

                                                         JANUARY 1

Leo tunapoanza mwaka mpya 2016 tuna kila sababu ya kuanza kwa kumshukuru Mungu kwa upendo wake kwetu na kwa familia zetu. Tuendelea kujiuliza tumpe  Mwenyezi Mungu kwa upendeleo huu mkuu wa kuweza kuiona siku hii mpya katika mwaka huu mpya? Je mimi/wewe tunaupekee gani tofauti na wale wote ambao wameitwa katika pumziko la milele? Kwa baraka na neema hii kubwa sisi sasa tunatakiwa tumrudishie nini mungu wetu? Je mwaka huu mpya kwetu una maana gani?
Je nini tunatakiwa kutafakari katika mwaka huu 2016?

Niliyoyafanya mwaka 2015 yote yalimpendeza Mungu au yalikuwa yananipendeza mimi mwenyewe?
Mwaka huu mpya tuiwekee nadhiri ya kuyaacha yote ambayo yalikuwa hayampendezi Mungu na kutuletea utengano naye; tukisoma kitabu cha waefeso sura ya 5:14-18 mtume Paulo anatukumbusha kuwa kwa matemdo yetu mabaya anatuasa tuamke na kubadilisha tabia kwani hakuna mtu mwingine yeyote atakaye ibadilisha tabia yangu/yako isipokuwa mimi/wewe mwenyewe. Njia pekee ni kumkaribisha kristo Yesu ambaye ni mwanga katika mabadiliko ya maisha yetu.

Mwaka wa 2016 uwe ni mwaka wa matendo yanaendana na kutumia muda wetu vizuri kwa utukufu wa mungu, kutisoma kitabu cha waefeso sura ya 6 Mwenyezi Mungu ametupa uwezo wa kutumia kila kitu, kwa kupambanua uthamani wake mbele ya mungu na utukufu wake. Inatakiwa tukumbuke kuwa yesu ni sadaka yetu pekee kupitia damu yake takatifu iliyomwagika msalabani kwa ajili ya msamaha wa dhambi zetu, na hatuhitaji hata kidogo msamaha mwingine wa dhami zetu, kama kitabu cha John 3:16 kinavyotukumbusha, sisi tunachotakiwa kuwa hekalu la Mungu ambaye ataishi ndani yetu. Sasa kama ukimkarisha mungu ndani yako unahitaji nini tena?

Zaburi ya 46:10 inatuonya kuwa sisi binadamu daima tunafanya vitu kwa uwezo wetu baada ya kutegemea nguvu za Mungu, na tunajivuna sana kama tukiona kuwa tumefanikiwa na kudharau nguvu ya Mungu. Lakini tunajisahau kuwa maisha yetu sio chochote na hatuwezi kuyamuda hata kidogo. Tukumbuke kuwa katika mazingira yeyoye yale, mungu peke yake ndiye anayeongoza na kutawala maisha yetu.

Katika mahangaiko, hofu, mashaka na mafanikio ya maisha yote naamini kuwa mungu peke yake ndio daraa pekee la mafanikio yangu/yako na familia yangu/yako. Mimi binafsi naamini kuwa kwa namana yeyote ile mafanikio yangu ni baraka pekee kutoka kwa Mungu juu yangu. Ninatembea katika ushindi mwaka huu wa bwana kwa sababu kubwa moja kuwa mimi daima natembea na bwana. Kama mwenjili Luka 1.28 anavyosema kuwa Mungu yu pamoja nami; kinachohitajika ni uwezo wa kusikia sauti ya kimungu ndani yetu hiyo ndio msingi wetu wa mafanikio na imani yetu ya ushindi wa mafanikio yetu.


Mwenjili matayo katika sura ya 7:8 anatukumbusha kuwa kwa yeyote ambaye anaomba hupokea, na yule atafutaye huona na yuke abishae hufunguliwa. Kwa hiyo tunatakiwa kuwa na imani na uthabiti na unyenyekevu ili tuweze kuuridhi utukufu na neema ya kimungu juu ya maisha yetu. Hatutakiwi kukata tamaa hata kidogo. Isipokuwa tunatakiwa tuendelee kumshukuru Mungu kwa uaminifu wake kwetu kwa kuendelea kusali kila siku na kila wakati bila kuchoka. Hatutakiwi kukata tamaa kwa kuchelewa kupata matokeo ya maombi yetu. Daima mwenyezi Mungu anafanya kazi katika utukufu wa maficho yake kwa faida yetu sisi. Na tusifahau kuwa majira ya mungu kwetu ni ya uhakika sana sana lakini kama tunaenenda katika imani.

Nakutakia safari njema ya Tafakari katika mwaka huu 2016 tembea nami kila siku katika kusifu na kumshukuru mungu kwa mema ambayo ameendelea kutenda juu yetu .Amina

No comments:

Post a Comment