WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Tuesday, January 19, 2016

JE WEWE NI MTEULE WA MUNGU?



January 19.

Tafakari ya leo tujiulize swali hili muhimu je mimi  ni miongoni mwa wateule wa Mungu? Na ili uwe mteule wa Mungu lazima uwe na sifa zipi za msingi?. Je bahati hii ni ya kila mtu au ni ya watu wachache tu? 

Jibu la swali hili ni kuwa kuwa mteule ni zawadi ya kila mtu kwani mungu anatujua na anajua kuwa sisi tumepungukiwa na haki ya ukamilifu wa mungu. Hivyo tukisoma kitabu cha waefeso tunaona kuwa tumepata uteule kwa kuokolewa na neema, kwa njia ya imani ambayo hiyo haikutokana na nafasi zenu,ni kipawa cha Mungu  wala si kwa matendo mtu asijekujisifu.

Tito 3:5-7 alituokoa  si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyotenda sisi bali kwa rehema yake kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa mara ya pili na kufanywa upya na roho Mtakatifu: amabaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia Yesu Kristo Mwokozi Wetu: ili tuhesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele kama ilivyo tumaini letu.

Ibrahimu alikuwa mteule wa Mungu ambaye alihesabiwa haki kwa matendo yake mema na kufuata sheria ya Mungu; tukumbuke kuwa mungu awezi kuwa na ushirika na Mtu asiye kuwa na haki kamilifu. Lakini mungu ametuonyesha kuwa sisi sote ni wateuliwa wake kwa kumtuma Kristo kufa kwa ajili yetu tulipokuwa tungali wenye dhambi. Hii ni zawadi kubwa ya uteule wetu katika maisha ya Kiroho.

Tukisoma kitabu cha warumi 4:3 maanamaandiko yasema; Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki. Kikubwa ambacho alikionyesha ni uthabiti wa imani yake Iliyo mpendeza Mungu. Mungu anatutaka sisi tuweke imani yetu yote kwa Mwanae Yesu Kristo. Wokovu unapatikana kupitia yeye ndio tumaini letu katika uteule wetu. Uteule wetu umekuwa rahisi sana kwa neema ya Kuja Yesu ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kukufuliwa ili tupate kuhesabiwa haki.

Kuwa mteule wa Mungu ni jambo ambalo kila mmoja wetu analiweza kuifanya na kulifikia. Jambo la msingi ni kuzingatia maelekezo,hatutakiwi kuwa kama Adam na hawa ambao walishindwa kusikiliza na kutimiza maelekezo ambayo Mungu aliwapatia. Shetani kwa mfano wa nyoka aliweza ktumia umahiri
wake na kuwadanganya nao wakadanganyika na hivyo kupoteza sifa ya moja kwa moja ya uteule.

Tafakari ya leo inatufundisha kuwa sisi tunabahati kwani hata pale tunapopoteza sifa ya uteule kwa kusudi au kwa bahati mbaya zinazotokana na hila za shetani tumepewa bahati ya
Toba iliyotokana na kifo cha Yesu msalabani. Sasa kama tumeweza kupata bahati hizi zote kwa nini tusiwe wateule katika karamu ya mwisho?

Yohana 3:17-21 '' Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU. Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.

Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa. Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika MUNGU. ''

“Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake; naye atawatolea mataifa hukumu. Hatalia, wala hatapaza sauti yake, wala kuifanya isikiwe katika njia kuu. Mwanzi uliopondeka hatauvunja, wala utambi utokao moshi hatauzima; atatokeza hukumu kwa kweli. Hatazimia, wala hatakata tamaa, hata atakapoweka hukumu duniani; na visiwa vitaingojea sheria yake.”—Isaya 42:1-4.

Tafakari ya leo inatuhakikishia sisi kuwa “Lakini ninyi ni taifa teule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu la Mungu, mlioitwa ili kutangaza sifa Zake Yeye aliyewaita kutoka gizani mkaingie katika nuru Yake ya ajabu. Mwanzo ninyi mlikuwa si taifa, lakini sasa ninyi ni taifa la Mungu. Mwanzo mlikuwa hamkupata rehema, lakini sansa mmepata rehema. 1pet 2;9. Kwa maana alituokoa kutoka katika ufalme wa giza na kutuingiza katika ufalme wa Mwana Wake mpendwakol 1;13.


Katika tafakari hii tushangilie kuwa tu wateule wa Mungu lakini yatupasa kusikia sauti ya Mungu na kutekeleza maagizo ya sauti hiyo;

No comments:

Post a Comment