WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Monday, January 11, 2016

JE NI ZAWADI GANI KUBWA TULIYOJALIWA NA MUNGU

January 11

                             HAPPY BIRTHDAY

Kama Kitabu cha (Yakobo 1:17)  kinavyo chambua kuhusu Kila kilicho chema,  kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kutoka kwa Baba wa mianga, ambaye Kwake hakuna kubadilika: Leo tutafakari kwa pamoja kuona ni zawadi gani kubwa ya maisha ambayo mwenyezi Mungu ametuajalia sisi waja wake?

Zawadi ya uhai na kutenda yale ambayo yana mpendeza Mungu ni kubwa kuliko zote;Je  kuna zawadi zaidi ya hii?

Leo hii tunaposherekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa wapendwa wetu tunatakiwa kuinua mikono yetu juu tukiwambia Mungu asante sana kwa zawadi hii muhimu ya maisha ambayo ni kubwa na bora ambayo Mungu amewajalia wapendwa wake. Siku ya kuzaliwa ni siku muhimu sana katika maisha ya kila mmoja wetu hasa wale ambao tumaini lao liko kwa Mungu wao;

(Yakobo: 4:6) anatuabarisha kuwa tunapompa Mungu asante, tuna mshukuru yeye kama ndiye pekee mtoaji ya vyote tunavyovifurahia hapa dunia, tunasherekea ukuu wake na wema  wake; na kwa kumshukuru yeye tunaonyesha unyenyekevu wetu kwake yeye; hii ni shukrani pekee ambayo tunastahili kumrudishia bwana kwa wema na Baraka zake.

Hivyo tuzidi kuomba Baraka na upendo wa pekee, tunaomba Mwenyezi  Mungu uzidi kutubarika kadiri unavyotujalia maisha utaangazie neema zaidi, upendo, msamaha na uwe taa inayomulika katika haya maisha ambayo hayana uhakika kwetu, ni wewe tu ambaye unajua nini hatima ya maisha ambayo yako mbele yetu; hii ni tafakari ya leo.


Amina

No comments:

Post a Comment