WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Monday, January 25, 2016

NINAYO FURAHA YA KWELI LEO

January 25



Leo Tafakari yetu inaangalia mafundisho ya Biblia kuwa Walio na
furaha ya kweli , ni hao walio masikini rohoni , yaani tegemeo lao
haliko katika mambo ya kidunia ila wanamtegemea Mungu kwa kila
kitu. Walio na huzuni au wanateseka kwa sababu yake Mungu, nao
watafarijiwa .

Bibilia inatufundisha kuwa ili kuitwa wana wa Mungu yatupasa
 kuleta amani na upatanisho miongoni mwa watu na kati ya watu
 wa miongoni mwetu.

Biblia inatoa mfano wa kuwa Chumvi huwa nzuri iwapo tu na ladha,
ikipoteza ladha yake, basi haifai kitu ila kutupwa. Rafiki, wewe ni
chumvi na ili kuhifadhi ladha, unastahili kudumisha amani wakati
wote. 

Je daima tunamshukuru Mungu kwa neema ya ya uzima ambayo tumejaliwa kwa wiki hii nzima iliyokwisha?

Je tunamshukuru Mungu kwa neema ya uzuri tunaoringia miongoni mwetu?


Wakati unafanya tafakari ya jumapili ya leo wewe uko kwenye kundi gani, kati ya makundi haya matatu hapo chini?


·   Watu wema wataendelea kudumu katika uaminifu na uokovu wa maisha  yao .

· Watu aliokuwa sio wema ambao wanakubali makosa waliyofanya na  wanapojirekebisha huwa thabiti katika msimamo wao, watu walio  katika kundi hili Mungu atazidi kuwabariki.



·        Watu wa kundi la tatu wanategemea hali ya jamii ilivyo, ikiwa jamii iko katika tamaduni nzuri na wao hufuata namna ya utamaduni wao ulivyo, na ikiwa jamii haiko katika tamaduni nzuri na wao vile vile hufuatanamna ya utamaduni wao ulivyo. Mungu hutukumbusha kuwa daiama tunatakiwa kuwa na msimamo na imani katika maisha na matendo yetu na sio kuishi bila msimamo kama mawimbi ya bahari ambayo yanasukumwa na upepo kwa mwelekeo wowote ule. Hii ndio tafakari yetu ya leo

No comments:

Post a Comment