WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Wednesday, January 13, 2016

SEMA NENO TU NA MTUMISHI WANGU ATAPONA.




January 13

Tafakari ya neno tunaipata kutoka kitabu cha Mwanjili Matayo 8: 5-10. Yesu alipoingia Kapernaumu, askari mmoja alikuja kumwomba msaada,  akisema, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani amepooza, tena ana maumivu makali.  Yesu akamwambia, Nitakuja kumponya.  Lakini yule askari akamwambia, Bwana, mimi sistahili wewe uingie nyumbani kwangu; lakini sema neno tu, na mtumi shi wangu atapona.  Yesu aliposikia maneno haya, alishangaa, akawaambia wale waliomfuata, Nawaambia kweli, hata katika Israeli sijaona imani ya namna hii.  

Tafakari ya leo inatuonyesha kuwa tunatakiwa tuwe na imani dhabiti, na kwa kuwa na Imani imara basi kwa neno tu kila kitu tukiombacho hutimia; kama yesu alipomjibu Yule Askari “Nenda nyumbani, na yale uliyoamini yatimie kwako. Na yule mtumishi akapona tangu wakati ule ule”.Hapa mwinjili Matayo anatuonyesha zaidi kuhusu nguvu ya imani:

Binadamu tunaamini zaidi katika nguvu mwili, kuguswa kama unaumwa ndipo upone; tunaona hata wachungaji wengi hutumia njia hii. Lakini Hapa Yesu kupitia kwa askari alionyesha kuwa Imani dhabiti huzaa tunda lililo njema ambalo ni neno.

Kuna maswali mengi ya kujiuliza kulikoni asiingie kwenye Nyumba hiyo na akamguse ili kumponya mtumishi mgonjwa? Inaonekana kuwa askari alikuwa amesikia kuhusu nguvu, uwezo na mamlaka ya Kimungu na uponyaji ambayo anayo Yesu alikuwa navyo. Lakini aliamini kuwa Yesu kwa nguvu ambayo alikuwa nayo haikuwa lazima kwake kwenda kumwekea mkono ili apone bali kwa NENO lake tu lilikuwa linatosha kumponya mtumishi wake mgonjwa. Hii ni imani ya Ajabu na kubwa sana.

Katika tafakari ya leo lazima tukubali kuwa katika maisha yetu ya Kila siku lazima tukuze na kuimarisha imani yetu ili tuweze kufanikiwa katika maombi yetu. Hata kama tunasali vipi, tunaomba vipi lakini bila Imani ya kweli hatuwezi kufanikiwa na tutaendlea kulalamika na kusikitika kuwa Mungu asikilizi kilio na shida zetu;tukumbuke kuwa katika maisha yetu ya Kiroho Imani huza NENO lenye nguvu ya kukamilishi mahitaji yetu.

Tafakri yetu leo inalenga kuwa hata Yesu alikuwa hajeona mtu mwenye imani kubwa namna hii na unyenyekevu mkubwa; kwa sababu walio wengi kwanza walikuwa hawaamini kuwa kweli anaponya kwa nguvu ya kimungu.

Imani ni kila kitu katika maisha yetu, na mwenyezi mungu anapendezwa na mtu mwenye imani imara, tunapomwamini Mungu na kuamini kuwa yeye ni kila kitu katika maisha yetu nasi hubarikiwa; imani ambayo askari huyu alionyesha ilikuwa zawadi kubwa sana mbele ya mungu naye alipokea zawadi kubwa sana. Mungu ni Imani na Mungu Ni Neno.

Imani ya Asakari huyu ilikuwa kama imani ya baba yetu Abraham ambaye aliamini kwa neno na bila kuwa na mashaka alitimiza maagizo ya Mungu. Aliamini katika ahadi za Mungu bila kuzitilia mashaka; na kwa kuamini Abraham alipata zawadi kubwa sana ya kuwa baba wa Imani.

Je wewe na mimi leo imani yetu iko wapi? Tunaamini katika nguvu na uwezo wa Neno la uzima ambalo ndilo mwanga katika maisha yetu ya kila siku na mafanikio yetu hapa duniani na hatimaye mbinguni? Ni wakati mzuri wa kutafakari wazo hili;

Amina


No comments:

Post a Comment