WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Friday, January 22, 2016

Ujue kwa maombi yako mimi nitabarikiwa



January 22

Tafakari ya leo inatukumbusha  wazo nzima la kuombeana: tukumbuke kuwa kwa kuwaombea wengine  tunaonyesha upendo mkubwa miongoni mwetu. Tukisoma Yohana 1:34 anasema amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, ninyi mpendane vivyo hivyo. Tukumbuke kitabu cha Torati inasisitiza kuwa umpende jirani yako.

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa tunatakiwa kutafuta na kufuata mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana na sio kutengana. Tunatakiwa kuendelea kufarajiane na kujengana kila mtu na mwenzake na njia pekee ya kujengana ni kwa kuombeana:
Tusihukumiana tukihukuminana hatutakiani Baraka.Kitabu cha waefeso 4:32 kinatukumbusha kuwa, tena iwe wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.

Tukumbuke kuwa tunaposali tunasali katika namna tatu  aina ya kwanza ni ile ya  ya kuelekeza juu kwa Mungu sala ambazo tunaelekeza zaidi kwa Mungu wetu kwa kumwabudu, kumsifu, kumshukuru na kuomba msamaha.

Aina ya pili ni sala ya ndani yetu ambazo zinatuhusu sana sisi wenyewe tukikazia zaidi kuomba msamaha, kuomba nguvu na ulinzi wa mungu na mwongozo wa maisha bora kulingana na maelekezo ya Mungu.

Na Aina ya mwisho ni kwa ajili ya wengine zinalenga nje  sala ambazo zinalenga zaidi wengine mahitaji ya wenzetu jirani zetu, ndugu zetu tunapowaombea kuhusu shida zao na mahitaji yao.

Tukisoma bibilia inatukumbusha kuwa kuwaombea wenzetu ni wajibu wetu kama wakristo; kwani kwa kufanya hivyo tunapata faida nyingi na kama kuwaimarisha kiimani, kwani nikijua wewe unaniombea inanipa mimi ushindi na uimara.

Pili tunapoombeana inatujengea  ukaribu undugu wa kiroho na hivyo kila mmoja wetu anabarikiwa. Na hata inaweza kutusaidia kuondoa tofauti zetu tukijua kuwa sisi sote ni ndugu mmoja kwani tunajua maombi ya mwenye haki yanaleta matokeo tukumbuke Jinsi Eliya alivyoomba kuhusu Mvua na mafanikio ambayo yalikuja kulingana na maombi yake.


Kwa hivi sisi tunatakiwa kufurahi pamoja na wafurahio na kulia pamoja na nao waliao; na htutakiwi mumlipa mtu ovu kwa uovu tuangalie yaliyo mema machoni pa watu wote. Tuache kuangalia bali tuushinde ubaya kwa wema. Zaidi ya yote tuwe na juhudi katika kupendana  kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi. Tafakari ya leo tunatakiwa kutumia karama zetu katika kuhudumiana kama mawakili wema wa Yesu katika kufurahia na kushukuru neema mbalimbali za Mungu. Amina

No comments:

Post a Comment