WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Thursday, January 21, 2016

Msiupende Ulimwengu




January 21
Tafakari ya leo tuangalie ni kitu gani sisi huwa tunakipenda zaidi katika maisha yetu: Je tunaupenda ulimwengu kwa vile tunaufahamu au tunapenda Mbingu kwa vile tumehaidiwa mazuri mengi? Leo tuangalie kitabu cha 1 Yakobo 2; 15 -17; Msiupende ulimwengu wala mambo  yaliyoko ulimwenguni. Kama mtu ye yote  akiupenda ulimwengu, kumpenda Baba hakumo  ndani yake.  

Kwa maana kila kitu kilichomo  ulimwenguni, yaani, tamaa ya mwili, tamaa ya  macho na kiburi cha uzima, havitokani na Baba bali hutokana na ulimwengu.  

Nao ulimwengu  unapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye  afanyaye mapenzi ya Mungu adumu milele;


                   Starehe za Walimwengu

Kwa walimwengu mtazamo ni kuwa yafurahie maisha katika hali yeyote ile hata kama maisha yanakufanya ulie kwa ugumu wake lakini wewe uonyeshe ulimwengu kuwa unasababu elfu moja za kifurahia kwa staili yeyote kama picha hii hapa juu inavyoonyesha; starehe kwanza halafu mengine baadae; Mungu tutamkimbilia “ BAADAE” baada ya starehe, bado tuna muda wa kutosha;

Tutafakari  yetu tukiulizwa na Muumba wetu je unapendelea kupita daraja gani kumfikia yeye?

1.   Daraja la uzima ambalo linakwenda moja kwa moja kwake na kwa Muda mfupi kama Waraka wa Yakobo unavyotufundisha;

2.  Daraja la anasa na malimwengu linavyojieleza ambalo huna uhakika wa kumfikia yeye kwa wakati muuafaka kabla milango ya mbinguni haijefungwa;


La msingi huu ni wakati mzuri wa kufanya tafakari kuhusu hatima ya maisha yetu  - Amen-

No comments:

Post a Comment