WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Thursday, January 14, 2016

TUMEPEWA NGUVU NA UWEZO WOTE KUSHINDA



January 14

Tafakari ya leo inahusu nguvu na uwezo ambao Mwenyezi Mungu ametujalia sisi kama tunavyosoma kutoka kitabu cha mwenjili Luka 10:19 “Tazama, nimewapa Amri ya kukanyaga Nyoka na Nge, na nguvu zote za yule Adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru ” Somo hili linatumbusha kuwa sisi wanadamu tumepewa uwezo wa kumshinda Shetani na Nguvu; kupitia hii Mamlaka tuliyopewa na mungu kupitia Bwana wetu Yesu Kristo, tuna uwezo wa kuzikanyaga na kuzisambaratisha Nguvu za Yule Adui Shetani.

Leo tunapotafakari tukumbuke kuwa ni ukweli usiopingika kwamba tumepewa uwezo wa kuharibu nguvu za aina yoyote za adui. Lakini ni ukweli usiojificha tulio wengi tumekosa imani thabiti ya kutumia nguvu hii kubwa hivyo ni wakristo wachache sana wanaojitambua kwamba wana uwezo huu ndani yao na kuweza kutumia nguvu hizo; Mara nyingi Yesu aliona udhaifu huu hata kwa wafuasi na Mitume wake ndipo tukisoma  Yohana 14:12 alituasa hivi; Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.

Leo tujipime na kujitambua kuwa kila mtu ana nguvu na uwezo wa kuziharibu nguvu za giza. Lakini  lazima tukubali kuwa mwanadamu yeyote asiye jitambua hawezi kufaulu katika jambo lolote. Usipojitambua kwamba waweza kufanya kitu Fulani, basi huwezi kusonga mbele, maana tayari umeshaona huwezi. Mtu yeyote aliyefanikiwa kimwili na kiroho huanza kwanza kujitambua ndani yake.  Na utambuzi anakuja na Imani ambayo inakujengea uwezo mkubwa wa kutekeleza jukumu lolote lile ambalo liko mbele yako;

Tafakari ya leo inatakiwa itukaribishe karibu kabisa na utekelezaji wa jukumu hili ambalo linaanzia kwenye maombi na kumshukuru Mungu. Ni kazi ambayo inakuwa na vikwazo vingi lakini inahitaji Nguvu imara ya Imani ili  mkono wa Mungu uwe juu yako/yangu katika kuifanya kazi hii ilojaa vikwazo kila mahala adui anapoona  anakanyagwa naye hujitutumua kukushinda hivyo shetani  ndivyo alivyo;

Hii ni tafakari kubwa kuwa nguvu ya ushindi i katika kukiri na kuamini kwetu, tumepewa mamlaka ya kumiliki kila tunapokanyaga iwe ofisini, shuleni kwenye biashara zetu sehemu yoyote ile tumepewa mamlaka ya kutawala kila kitu na kila mahali kama Mungu alivyomwabia Adamu. Luka 10.19-20 anasema tazama nimepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachonidhuru.

Tukumbuke Jinsi wale wafuasi wa yesu walivyorudi kwa furaha baada ya kupewa mamlaka ya kutenda kazi:  Wafuasi wale sabini walipewa na Yesu amri ya kukanyaga nyoka na nge na wasiwadhuru na kisha pepo wakawatii, hii inawezekana tu kwa mamlaka kutoka kwa mfufuka, Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako. Akawaambia, ..…Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru


Hii ni tafakari yetu ya leo tutumie mamlaka ambayo Yesu ametupatia kwa siafa na utukufu wake na kwa ili nasi turudi na ushuhuda wa furaha kama wafuasi wa Yesu- Amina 

No comments:

Post a Comment