WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Monday, January 4, 2016

JIRANI NI NANI




January 4

Tafakari yetu leo inaelekwezwa katika agizo la Yesu kwa wafuanzi wake na wananfunzi wake pale alipofundisha kuhusu amri ya Upendo kwa jirani kama tunavyojipenda wenyewe. Yesu angeweza tu kusema mpende jirani yako na kuishia hapo; lakini kwanini aliamua kuhitimisha kwa maneno haya “ Kama unavyojipenda Mwenyewe”?
Binadamu tuna huluka na silika ya kujipenda zaidi sisi wenyewe kuliko kumpenda mtu mwingine. Ni tabia ambayo tunayo na imekuwa vi vigumu kuondokana nayo; tafakari ya leo inatukumbusha kuwa agizo la Yesu ni la muhimu ili tuweze kuuridhi uzima wa milele lazima na jirani zetu tuwapende katika mizani ile ile tunayojipenda sisi wenyewe. Katika biblia kuna amri kuu mbili za upendo wa kumpenda Kwanza Mungu  kwa moyo wetu wote, na ya pili inafanana na hii  ya kwanza ya kumpenda jirani: “Mpende jirani yako kama wewe mwenyewe.” (Mathayo 22:39) 

Hapa tuna jifunza kuwa kumpenda jirani, kama vile kumpenda Mungu, si hisia tu; ni jambo linalotakiwa lionyeshwe kwa matendo. Kuwapenda wengine kama tunavyojipenda wenyewe kunamaanisha kwamba tunawaona wengine kama tunavyotaka watuone na kuwatendea kama tunavyotaka watutendee. Golden Rule; ambayo msingi wake kiimani kuwa Mtu wa MUNGU ni yule aliyekaa katika pendo. Je wewe leo unajitambua kuwa umekaa katika upendo?

Tukisoma kitabu cha Walawi 19:17  kinatukumbusha kuwa : Usimchukie ndugu yako moyoni mwako; na pale ambapo jirani yako hajefanya sawasawa ni lazima kumkemea jirani yako, hatuna sababu ya kuumia kimoyomoyo  na kutenda dhambi ya masengenyo dhidi yake; pale inatotupasa kumsahihisha jirani kwa upendo na tatufnji hivyo tunaishia kutenda dhambi  mbele ya mungu kwa malalamishi yetu juu ya jirani. Tunaweza kuirekebisha dhambi hii kwa kukwemea.

Mfano mwingine mzuri kuhusu upendo wa jirani  hadithi ya Yesu inayopatika katika kitabu cha Lk. 10:30 mtu aliyeshuka kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko na kuangukia katika mikono ya wanyanganyi  ambao walimpiga , kumvua nguo, walimwumiza na kumwacha karibu kufa; Tunaona Kuhani ambaye ni mtu anayejua sheria za dini na wajibu wake kwa jamii alikuwa akipita alimwona na kupita kando bila kutoa msaada wowote; Mlawi naye alifanya hivyo hivyo; lakini msamaria mwema yeye alifika mahali hapo na kwa matendo alionyesha upendo wa khali ya juu kwa kumfunga majeraha yake na kumpa huduma zote kama alivyoweza na kasha kuondoka naye na kumpeleka katika sehemu nyingine ambyo aliweza kupata matibabu zaidi kwa gharama zake. Msamaria mwema hapa ameonyesha upendo wa khali ya juu na hivyo yeye amekuwa jirani kwa  mtu hutu aliyekuwa akihitaji msaada.

Ni vigumu sana kutekeleza agizo hili la Yesu kama hatuna upendo wa kweli; tukumbuke kuwa tunda la Roho ni upendo, ambao utaleta  furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, na upole; kwa kutekeleza upendo huleta ujirani mwema na utekelezaji wa amri hii kubwa ya kupendana kwani huta mwia mwenzako na kitu chochote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria. Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yoyote, inakamilishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Pendo halimfanyii jirani neon baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria”.

Tunaishia kuvunja amri hizi zote kwa sababu hatuna upendo ndani yetu; tukiwa tumetawaliwa na upendo, hatutaweza kuiba kwani kwa kuiba unamwibia jirani yako; kwa kusema uwongo unamkosea jirani yako ili kumletea matatizo ambayo hastahili kuyabebe. Ukizini unatenda kosa la kumsaliti jirani yako ambye ni mUme wako au Mke wako; kwa ufupi tukitimiza amri ya upendo inavyotatimwa hatuwezi kufanya dhambi yeyote, bali tutaweza kuishi maisha ya amani na upendo mkubwa sana kwa kujali na kusaidiana kama biblia inavyotaka sisi leo tuishi.

Basi siku ya leo tuendelee kutafakari nafasi yako au yangu katika kutekeleza amri hii kubwa ya upendo kwa matendo amen.



No comments:

Post a Comment