WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Wednesday, January 20, 2016

FARAJA YA KWELI INATOKA WAPI?


January 20

Tafakari ya leo tuliangalie hili wazo la kumshukuru Mungu katika kila jambo: Mtume Paulo kwa 2 Wakorinto 1-7: anatukumbusha kuwa katika kila haja yetu tukumbuke kuwa daima ; Atukuzwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba mwenye huruma na Mungu mwenye kuleta faraja yote. 

Tukumbuke kuwa Yeye hutufariji sisi katika taabu zetu zote, ili nasi tupate kuwafariji wengine katika kila taabu kwa faraja hiyohiyo tunayopokea kutoka kwa Mungu. 

Japo tunakuwa katika majaribu; Naam, kadiri mateso ya Kristo yanavyozidi ndani yetu, ni kadiri hiyohiyo tunazidi kufarijiwa naye. 
Na kubwa zaidi ni kuwa Ikiwa tunapata taabu, basi ni kwa ajili ya faraja na wokovu wenu. Tukifarijika, ni kwa ajili ya kuwafariji ninyi na kuwaunga mkono mpate nguvu ya kustahimili mateso yaleyale tunayoteseka sisi.


Katika tafakari hii tujue kuwa; Tena, matumaini tuliyo nayo kwa ajili yenu ni imara; tunajua kwamba mkishiriki mateso yetu, mtashiriki pia faraja yetu.

Tutafakari pamoja uzito wa ujumbe huu wa Paulo katika maisha yetu ya kila siku Amen

No comments:

Post a Comment