WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Wednesday, January 6, 2016

BABA KAMA ULIVYOTUFUNDISHA KUSALI



January 6

Tafakari ya leo hebu tusali pamoja tukimshukuru Mungu kwa wema na ukuu wake kwetu;

Eh Baba kama ulivyotufundisha  kusali katika sala kuu  ya Bwana ambako tunautukuza ukuu wako na pili tunaomba msamaa wa makosa yetu na hatiamye tunaomba Baraka ya mahitaji yetu na kuutukuza ukuu wako;

Tunatakiwa kuhesabu furaha tupu tunapopatwa na majaribu mbalimbali, kwa sababu tunajua ya kuwa kujaribiwa ndani ya imani yetu huleta saburi.  Saburi na iweze kufanya kazi yake inatakiwa kuwa timilifu, ili tupate kuwa wakamilifu,  na hivyo tutakamilishwa, bila kupungukiwa na kitu cho  chote. 

Tunafahamu kuwa mara nyingi miongoni mwetu  tunapungukiwa na hekima na ndio maana tunazidi kukuomba wewe Mfalme wa wafalme , wewe uliye Alfa na Omega uzidi kuayasikiliza maombi yetu na utujalie kuupata msaada tuuombao, tunafahamu kuwa wewe ni  mwenye ukarimu na wala huna kinyongo,.

Lakini  umetufundisha kuwa tuombapo inatupasa kuwa na imani na  kuamini na  kutokuwa na shaka, kwa sababu mtu aliye na shaka ni kama  wimbi la bahari, lililochukuliwa  na upepo na kutupwa huku na huku.  Mtu kama huyo  tusidhani ya kuwa atapata kitu cho chote kutoka  Kwako. Yeye ni mtu mwenye nia mbili,  mwenye kusitasita katika njia zake zote.

Basi na tukikaribie kiti cha rehema kwa ujasiri,  ili tupewe rehema na kupata neema ya  kutusaidia wakati wa mahitaji na Maombi yetu, sisi sio wale wenye haki  tunatamani kuwa miongoni mwao kwani tunafahamu kuwa maombi ya wenye haki yana nguvu tena yanafaa sana.  Tunamkumbuka Eliya alikuwa mwanadamu kama sisi.  Akaomba kwa bidii kwamba mvua isinyeshe nayo haikunyesha juu ya nchi kwa muda wa miaka mitatu na miezi sita. Kisha akaomba  tena, mbingu zikatoa mvua nayo ardhi ikatoa mazao yake.  


Tunajongea mbele ya kiti chako kwa unyenyekevu tukiomba wingi wa huruma yako na utusikilize katika shida zetu, na utupe majibu ya maombi yetu. Amen

No comments:

Post a Comment