WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Tuesday, January 12, 2016

TUSAFISHE NYOYO ZETU ILI KUISHI INAVYOTUPASA


JANUARY 12

Kitabu cha Maombolezo 3; 40 kinatukumbusha kuwa na tuchunguze njia zetu na kuzijaribu, na kumrudia bwana tena, Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.Warumi :23 Mungu alimwumba mwanadamu kwa kusudi la kushirikiana naye, lakini mwanadamu alikwenda Kinyume cha mpango wa Mungu. Alichagua kumwasi Mungu badala ya kumtii. Kumwasi Mungu ni kufanya Zambi; hi maana yeke ni nini, mtu anapoishi kinyume cha mapenzi ya Mungu anaendelea kuishi maisha ya dhambi. Hapa ndipo tunapoona umuhimu wa kuanza kusafisha nyoyo zetu

Lazima tujisafishe tukijua kuwa Mungu Mtakatifu hana ushirika na dhambi. Kati yake na mwanadamu kuna ufa mkubwa ambao unaotutenganisha na ufa huu ni dhambi. Mwenyezi Mungu anatutaka sisi leo tujisafishe ili tuweze kuondoa huu Ufa  na hatimaye kumfikia Mungu na kuishi naye tena katika bustani ya Adeni. Tukumbuke kuwa mwanzo Mungu alipomuumba Adamu na baadae Hawa  waliishi naye bila kuwa na Ufa wowote ule; Lakini walipotenda dhambi ndipi Mungu alipojenga Ufa na Kuwafukuza kutoka Adeni kwani walikuwa ni wadhambi;

Tunatakiwa Kujisafisha  kwa  matendo mema na  sala na kumkaribisha Mwokozi wetu Yesu Kristo Mioyoni mwetu kwani yeye ni Mpatanishi wetu kama anavyosema ; Tazama, nasimama mlangoni, nabisha, mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake. Yesu  anaishi ndani ya nafsi ambayo inachukia dhambi tumeonywa kuwa dhambi isitawale ndani ya miili yenu. Sisi kama wafuasi wa Kristo ambao tuko tayari kusafisha nyoyo zetu tukumbuke kuwa  tunaishi chini ya neema ya uokovu wa mungu tukikubali kubadilika.

Luka 7.21 inatukumbusha kuwa  “ Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni”. Mapenzi ya Baba ni kukubali kubadilika ili nasi   tuhesabiwa haki.  Yatupasa kutenda yale yatupasayo kutenda;  ili tuendelee kumwita Yesu Bwana  na hatutendialiyofundisha? Kila mtu ajaye kwangu na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda.  Tunatakiwa tusafishe  nyoyo zetu tukizingatia kuwa upendo wa mungu ni tofauti kabisa na upendo wetu kwa binadamu mwingine; tukumbuke kuwa baba mzuri anapenda mazuri zaidi kwa watoto wake anajitoa sadaka kwa ajili ya yao na anawapatia mahitaji yao wanayoyahitaji kwa wakati na pale wanapokosea  kwa faida yao anawaadibisha na kuwasamehe.

Tunatambua kuwa wakati mwingine watoto wetu wanakataa ushauri wa baba ambao ni mzuri na kukimbilia ushauri wa kuaacha kilicho bora na muhimu; hapa tunaona kiburi na ubinafsi ukiwa unatawala zaidi. Wanaingia atika maisha ya anasa na mwisho wa siku wanaishia pabaya. Tujifunze kutoka hadithi ya mtoto mpotevu. Tunashauriwa kujisafisha kwa kuzingatia kuwa mwenyezi Mungu ametupa uhuru wa kuchagua nakutenda tutakavyo, yeye alichotusaidia ametuwekea sheria tuzifuate ili tuweze kuwa miongoni mwa wateule wake; amaetujalia ufahamu na uwezo wa kuamua kati ya mabaya na mazuri. Mungu aliumba ulimwengu na sheria zinazo ongoza kila kitu ili tuzitii; tukumuke kuwa sheria ya maadili ya Mungu ni muhimu kwa sababu inatokanamisingi ya Kimungu.

Hivyo zambi zetu kutoka zile za mababu zetu  zimevunja uhusiano wetu na Mungu. Tusafishe uasi wetu ambao umetengeneza ukuta wa utengano kati ya Mungu na sisi. Ni kweli kuwa tumekuwa bize katika maisha yetu ya kila siku ya kidunia na tumekosa muda hata kidogo tu wa kumshukuru Mungu.

Tafakari ya leo bado hatujechelewa tunanafasi kubwa tu ya kusafisha nyoyo zetu ni kutambua kwamba Neema ya Mungu bado iko juu yetu ya kuendelea kumshukuru Yesu kuwa ni bwana na mwokozi wa maisha yetu na alikufa msalabani ili aweze kuondoa ukuta wa utengano ambao uko kati yetu na Mwenyezi Mungu kwa Dhambi zetu. Tunatakiwa kubadilisha fikra zetu  kuwa tukisafisha Nyoyo zetu tutapata haki za  kuwa watoto wa Mungu. Hii ndio tafakari yetu ya leo.


Amen

No comments:

Post a Comment