WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Friday, January 15, 2016

BWANA NDIYE NGOME YANGU;




January 15

Tafakari ya leo hebu tuangalie ulinzi wa mungu juu ya maisha yetu; Daud katika zaburi ya 23 anasema hivi:
1  Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.
2  Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza.
3  Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.
4  Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
5  Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika.
6  Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele

Nimeipenda sana zaburi hii ukiisoma na kama unaielewa ni mwongozo pekee wa maisha ya kila siku. Na somo jingine ambalo tunafundishwa katika zaburi hii kuwa Mkristo sio hasa inahusu madhebebu yetu bali ni zaidi inahusu uhusuiano wako na Yesu ukoje;

Tukumbuke Yesu Mwenyewe alijiita yeye ni Mchungaji Mwema tukisoma injili ya Yohana 10:11. Maana yake ni nini? Kuwa yesu kwa kuwa mchungaji Mwema hapungukiwi na kitu chochote unachohitaji katika malisho bora, Majani mazuri yeye hutoa; ulinzi wa mifugo yeye husimamia kwa msingi huu kuwa Mungu yeye ni kila kitu tunachohitaji na hivyo Mungu alimtuma Mwanae aje kutukomboa kutoka katika utumwa wa dhami hivyo kwa msingi huu tukiwa na Yesu hatupungukiwi na kitu.

Ukiwa mfugaji na ukiwa kwenye machungio na wakati wa jioni ukifika na mifugo yako iko tayari kupumzika kuna mambo manne ambayo yatafanya mifugo yako iweze kulala salama:

Kondoo hawatakuwa tayari kulala kama wanahofu ya usalama wao yaani wamenusa hatari ya adui: Kondoo hawatakuwa tayari kulala kama kuna kuto elewana miongoni mwao ( friction); kondoo hawatakuwa tayari kulala kama kuna wadudu kama        (mbung’o) katika eneo ambalo wanatakiwa walale. Na mwisho kondoo hawatakuwa tayari kulala kama hawajeshiba na bado wanataka kuendelea kutafuta chakula.

Tafakari hii inatufundisha kuwa lazima kuwe na uhuru ambao hujitenga na woga wa usalama, ugomvi miongoni mwao, wadudu na njaa kabla kondoo kuweza kulala. Je tunaitafasiri hali hii vipi katika maisha yetu ya kila siku. Jibu la msingi kama  Daudi alivyolezea katika zaburi hii ya 23 kuwa Mungu anaondoa vikwazo katika maisha yetu, kwa dhumuni la kutupa sisi ufadhali wa maisha yetu.
Tukiendelea kutafakari siku ya leo tukumbuke kuwa Baraka ambayo yesu anatueleza sio kuwa tutaishi bila shida au majaribu; katikati ya majaribu ndipo tunapopata furaha ya kweli ya kimungu na tunaendlea kujaliwa Baraka mara dufu. Tunatakiwa kumuamini Mungu, kuwa anajali; anasikiliza; na ananipenda na atanilinda na nguvu zote za shetani; sisi kama kondoo sio viumbe wenye akili kumzidi Mungu, sisi kama viumbe hatuna nguvu ya kujilinda kama sio kwa nguvu ya Mungu; sisi ni viumbe ambao tunamtegemea Mungu; lakini kama walivyo kondoo lazima tuishi kwa Imani ya kumtegemea Muchungaji wetu Bora ambaye ni Yesu Kristo.


Tatizo letu leo hii sisi tulio wengi tunaishi maisha yetu katika uliwengu wa kulalamika na kukata tama; tukumbuke kuwa Mungu ndio nguvu yetu nay eye peke yake ataimarisha nguvu zetu. Hii ni tafakari yetu ya leo ; Amina

No comments:

Post a Comment