January
19.
Tafakari ya leo tujiulize swali hili muhimu je mimi
ni miongoni mwa wateule wa Mungu? Na ili
uwe mteule wa Mungu lazima uwe na sifa zipi za msingi?. Je bahati hii ni ya
kila mtu au ni ya watu wachache tu?
Jibu la swali hili ni kuwa kuwa mteule ni zawadi ya
kila mtu kwani mungu anatujua na anajua kuwa sisi tumepungukiwa na haki ya
ukamilifu wa mungu. Hivyo tukisoma kitabu cha waefeso tunaona kuwa tumepata
uteule kwa kuokolewa na neema, kwa njia ya imani ambayo hiyo haikutokana na
nafasi zenu,ni kipawa cha Mungu wala si
kwa matendo mtu asijekujisifu.
Tito 3:5-7 alituokoa si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyotenda
sisi bali kwa rehema yake kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa mara ya pili na kufanywa
upya na roho Mtakatifu: amabaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia Yesu Kristo
Mwokozi Wetu: ili tuhesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima
wa milele kama ilivyo tumaini letu.
Ibrahimu alikuwa mteule wa Mungu ambaye alihesabiwa
haki kwa matendo yake mema na kufuata sheria ya Mungu; tukumbuke kuwa mungu
awezi kuwa na ushirika na Mtu asiye kuwa na haki kamilifu. Lakini mungu
ametuonyesha kuwa sisi sote ni wateuliwa wake kwa kumtuma Kristo kufa kwa ajili
yetu tulipokuwa tungali wenye dhambi. Hii ni zawadi kubwa ya uteule wetu katika
maisha ya Kiroho.
Tukisoma kitabu cha warumi 4:3 maanamaandiko yasema;
Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki. Kikubwa ambacho
alikionyesha ni uthabiti wa imani yake Iliyo mpendeza Mungu. Mungu anatutaka
sisi tuweke imani yetu yote kwa Mwanae Yesu Kristo. Wokovu unapatikana kupitia
yeye ndio tumaini letu katika uteule wetu. Uteule wetu umekuwa rahisi sana kwa
neema ya Kuja Yesu ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kukufuliwa ili
tupate kuhesabiwa haki.
Kuwa mteule wa Mungu ni jambo ambalo kila mmoja wetu
analiweza kuifanya na kulifikia. Jambo la msingi ni kuzingatia
maelekezo,hatutakiwi kuwa kama Adam na hawa ambao walishindwa kusikiliza na kutimiza
maelekezo ambayo Mungu aliwapatia. Shetani kwa mfano wa nyoka aliweza ktumia
umahiri
wake na kuwadanganya nao wakadanganyika na hivyo kupoteza
sifa ya moja kwa moja ya uteule.
Tafakari ya leo inatufundisha kuwa sisi tunabahati
kwani hata pale tunapopoteza sifa ya uteule kwa kusudi au kwa bahati mbaya zinazotokana
na hila za shetani tumepewa bahati ya
Toba iliyotokana na kifo cha Yesu msalabani. Sasa
kama tumeweza kupata bahati hizi zote kwa nini tusiwe wateule katika karamu ya
mwisho?
Yohana
3:17-21 '' Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali
ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini
amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU. Na
hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza
kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.
Maana
kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake
yasije yakakemewa. Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake
yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika MUNGU. ''
“Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye; mteule
wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake; naye
atawatolea mataifa hukumu. Hatalia, wala hatapaza sauti yake, wala
kuifanya isikiwe katika njia kuu. Mwanzi uliopondeka hatauvunja, wala utambi utokao moshi hatauzima;
atatokeza hukumu kwa kweli. Hatazimia, wala hatakata tamaa, hata atakapoweka hukumu duniani; na
visiwa vitaingojea sheria yake.”—Isaya 42:1-4.
Tafakari
ya leo inatuhakikishia sisi kuwa “Lakini ninyi ni taifa teule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu la Mungu, mlioitwa
ili kutangaza sifa Zake Yeye aliyewaita kutoka gizani mkaingie katika nuru Yake
ya ajabu. Mwanzo ninyi mlikuwa si taifa, lakini sasa ninyi ni taifa la Mungu.
Mwanzo mlikuwa hamkupata rehema, lakini sansa mmepata rehema. 1pet 2;9.
Kwa maana alituokoa kutoka katika ufalme wa giza na kutuingiza katika
ufalme wa Mwana Wake mpendwa, kol
1;13.
Katika tafakari hii tushangilie kuwa tu wateule wa
Mungu lakini yatupasa kusikia sauti ya Mungu na kutekeleza maagizo ya sauti
hiyo;