WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Monday, February 1, 2016

KWA NINI TUNALALAMIKIA UGUMU KATIKA MAISHA?


February 1

Katika Tafakari yetu  YA LEO tuanze Kwanza kwa kumshukuru Mungu kwa Kutojalia kumaliza Mwezi wa January kwa usalama na kheri; Pili tuwaombee wale wote kwa namna moja au nyingine ambao wako katika khali ngumu au wametangulia mbele ya haki;

Je umeuanza mwezi February kwa maswali kwa nini mimi?  Kwa nini hiki kinatokea kwangu? Kwa nini maisha ni magumu? Kwa nini naandamwa na ambo haya? Magojwa, kukosa pesa, kutokuwa na maelewano mazuri ya kindoa; na kadhalika.

Tukisoma  2 Corinthians 1:1-11 mtume Paulo anatukumbusha kuwa daima maisha yetu yamejaa masononeko, malalamiko, malinganisho; anasema lakini nachelea; kama Yule nyoka alinyomdanganya hawa kwa hila yake, asije kuwaharibu fikra zenu, mkauaacha unyofu na usafi wa kristo. Mtume Paulo anatusahauri kuwa katika khali kama hii bado tumtumaini Kristo kuwa ndiye pekee anaweza wajibu maswali haya yote magumu.

Ni kweli katika wakati kama huu tunajiuliza maswali mengi yuko wapi Mungu wangu na kwa nini ananipa mimi wakati mgumu kiasi hiki? Kama wafuasi wa Kristo imara hatutakiwi kuwa na mashaka tunalotakiwa kulifanya ni kuendelea kuomba neema ya Mungu ambayo iko juu ya kila kitu na ambayo ndio pekee katika ushindi wetu wa ugumu wa maisha yetu;

 Na tukumbuke kuwa ugumu ambao tunaouona katika kila jambo ndani ya maisha yetu sio kwa sababu ya ugumu bali ni jinsi sisi tunavyo ukabiri ugumu huo. Je tunapokabiriwa na ugumu wa maisha kama magonjwa, khali ngumu ya kiuchumi, magomvi miongoni mwetu;

Je hatua yetu ya kwanza katika kutatua tatizo hilo inakuwaje? Namna ambayo tutakayo ichukua katika kutatua tatizo hilo ndio itakuwa suluhisho  sahihi. Mara nyingi tunakimbilia kujihukumu kwa nini hii imetokea kwangu? Lakini njia sahihi ilitakiwa tujiulize hapa ninajifunza nini? Ni wapi nimekosea mpaka nimefikia hapa nilipofikia? Je uchaguzi wa njia ya kutatua tatizo hili kwa mara ya kwanza ulikuwa sahihi? Je niliomba mwongozo wa Mungu kabla ya kufanya uamuzi huu? Tunajua Mungu anaruhusu ugumu wowote kutokea katika maisha yetu ikiwa ni njia ya kujifunza na vile vile ili uwe ni fundisho kwa siku zijazo;  au matayarisho ya jambo kubwa zaidi mbele ya maisha yetu;

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa tujitambue kuwa sisi katika ugumu wowote ule sio waathirika (victim); na hivyo Mungu anatuadhibu la hasha daima Mungu yuko nasi  na wakati mwingine anaruhusu vile vile ugumu katika maisha yetu  ili kutusaidia sisi kutembea  katika njia sahii kufikia mahitaji yetu; Mtume Paulo kwa Warumi 8:28 anatukumbusha kuwa  nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kumpatia mema, yaani wale walioitwa kwa kusudi lake. Hivyo hata katika ugumu wa maisha yetu lazima tuendelee kuamini kuwa Mungu yuko kazini kwa faida yetu;

 Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa daima tumpe sifa Mungu kwani ni yeye pekee ambaye ni kitulizo katika shida zetu; ni yeye pekee hututuliza katika magonjwa yetu tukiwa wagonjwa au pale mpendwa etu anapokabiliwa na tatizo kama hili; Tukumbuke kuwa  zaburi ya 23 inavyosema; bwana ndiye mchungaji wangu na sitapungukiwa na kitu. Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, kando ya maji ya utulivu huniongoza. Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza katika njia za haki kwa ajili ya jina lake. Naam nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya kwa maana wewe upo pamoja name, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.

Hivyo tukumbuke kuwa matatizo yetu au ugumu wa maisha unaotukabili unaweza kuwa ni Baraka kutoka kwa Mungu sio tu kwako na kwa wengine ambao wanaweza kujifunza kwa faida kubwa mbeleni.

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa katika ugumu wa maisha yetu kuna mwingine ambaye anatuangalia na kutubariki na sio mwingine bali na Mungu Kupitia Bwana wetu Yesu Kristo.

Hivyo tunavyokuwa katika wakati mgumu tunatakiwa tujifunze kuwa tumwamini Mungu; tuangalie matendo makubwa ya yesu Kristo kama alivyowafufu wafu; Je atashhindwa kutatua ugumu ulio nao katika maisha yako? Upeo wetu wa kutatua ugumu wa maisha yetu unakikomo lakini kwa Mungu na Mkombozi wetu Yesu hakuna kikomo; utendaji wao ni wa milele yote;


Tumeagizwa jambo moja katika kutatua shida za ugumu wowote unaotukabili ni kwa kusali bila kukoma au kuchoka; tunatakiwa kuwa na imani tuombapo; nah ii ni tafakari yetu ya leo. 

Amina

No comments:

Post a Comment