WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Wednesday, February 3, 2016

AKILI YAKO INAKUONGOZAJE KATIKA MAISHA YAKO?



February 3

Mungu alituumba katika namna ambayo matendo yetu hufuata mawazo yetu; maisha ya mwanadamu yameoanishwa na asili yake, au tabia ya mtu. Asili ya mwanadamu na maisha ni zao la yale yaliyomo moyoni wake.

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa mazingira tuishio ndio zao letu wanadamu;Mazingira huzalisha watu wenye tabia zinazoshababiana; swali ambalo nataka tujiulize leo ni kuwa je ni mazingira gani huzalisha watu  wanyenyekevu; au watu waliojaa tamaa za mali? Au kiburi?, maringo?, majivuno? na uzuri? Je ni mazingira gani huzalisha watu ambao katika maisha yao huongozwa na Roho wa Bwana waliojawa na hofu ya Mungu na upendo wa kweli?;

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa akili yetu ni kama shamba la mkulima. Kama mkulima akipanda mbegu za mahindi atarajie kuvuna mahindi; Kama amepanda ngano atavuna ngano. Itakuwa ni wazo la kufikirika na la kijinga kwa mkulima kupanda mahindi na kisha kutarajia kuvuna ngano.

Tupandacho ndicho tuvunacho; hivyo hata katika akili zetu jinsi tunavyozipanda tutegemee mavuno sawa; Hivyo katika tafakari ya leo tujiulize je matendo yetu tunayopanda katika mioyo yetu yatatuletea mazao gani mwishoni?

Kama ni kiongozi na huwajibiki kulingana na sheria na utaratibu wa kazi yako, na mwisho wa siku unategemea kuvuna mafanikio hizo zitakuwa ni ndoto. Haiwezekani kwa mtu yeyote kwenda kupanda kwa maovu na wizi na ukatarajia mwisho wa siku uvune matunda ambayo yatakupa Baraka za Mungu. Mungu amekupa uwezo wa kudhibiti unachopanda na hivyo ni busara tuanze  kudhibiti kile ambacho tunachotarajia kuvuna.

Kama Warumi 8: 5-8. "Kwa wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatayo roho huyafikiri mambo ya roho. Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti bali nia ya roho ni uzima na amani. Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii. Wale waufuatao mwili hawawezikumpendeza mungu.

Tunanahitaji  kuangalia na kutumia sheria ya akili yetu kuwa kile ambacho tumeamrishi akili yetu ifuate ndicho hatimaye kitakuletea matokeo yake mwisho. Haiwezekani kuweka mambo ya kidunia katika akili yetu na utegemee matunda ya kiroho; kwani anasa na starehe za dunia hazichangamani na maisha ya kiroho.

Tafakari ya leo inatumbusha kuwa sisi binadamu tunaweza kubadilisha maisha yetu kwa kubadilisha utendaji na mawazo ya akili zetu. Akili yetu iko sahihi kwani hutumwa kufanya kazi, sisi ndio wenye maamuzi ya kufanya jambo njema au baya; Kama nabii Isaya anayosema 55: 7, 8 Mtu mbaya na aache njia yake, na mtu asiye haki aache mawazo yake. Na amrudie bwana, naye atamsamehe kabisa. Maana mawazo yangu si mawazo yenu wala njia zenu si njia zangu asema Bwana.

Kama tunaamua kufuata njia ya kutenda haki haki basi akili yetu itekeleze mawazo ya haki.Ndio maana njia za Mungu ni tofauti sana kuliko njia yetu ni kwa sababu mawazo yake ni tofauti kuliko mawazo yetu mawazo yake daima hufikiria haki, upendo na ukombozi wetu sisi binadamu baada ya kumwasi na kujaza akili zetu matendo mabaya.

Tafakari ya leo inatumbusha kuwa yale yanayoendelea katika vichwa vyetu ni hivi sasa ni muhimu sana kwani yanaelekeza hatima ya maisha yetu. Hivyo ni vyema tudhibiti matendo yetu kwa kudhibiti mawazo yetu. Ni vyema kuyatafakari na kuyaangalia mawazo yetu na hatimu yetu ya milele.


Tafakari ya leo inalenga zaidi kutukumbusha kutaathimini mawazoyetu, amabayo mwisho yatakuwa  maneno; tutafakari manenoyetu, mwisho yatageuka kuwa matendo yetu; tuangalia matendo yetu, ambayo mwisho yatageuka kuwa tabia zetu na tuangalia tabiazetu, ambazo mwisho zitakuwa hatima mwelekeo wa maisha yetu ya Kiroho; Amina

No comments:

Post a Comment