WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Monday, February 8, 2016

KUSUBIRI MAJIRA YA MUNGU NI JAMBO LINALOTUSUMBUA SANA



February 8

Tafakari ya leo tangalie kuwa dhana ya kusubiri  majira ya mungu imekuwa ni jambo gumu kwetu wanadamu;  zaburi ya 27:14 umngoje Bwana, uwe hodari, upige moyo konde naam umngoje Bwana; Isaya 40:31 bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, walahawatachoka; watakwenda kwa miguu wala hawatazimia.

Kusubiri wakati wa Bwana ni  kila kitu katika maisha yetu  kwani tunaendelea kuliweka tumaini letu mikononi mwa Mungu; sisi binadamu majira yetu tumeyafunga zaidi katika kuupenda ulimwengu huu. Leo dunia yetu na majira yetu yametawaliwa sana na dhana ya umimi na hakuna dhana ya subira; Tumesahau  kuwa subira ni fadhila na kamwe hatutaki kusubiri. Matatizo mengi tunayoyashuhudia leo msingi mkubwa ni kushindwa kusubiri. Binadamu leo tumetawaliwa na msemo huu 'Nipatieni mimi haraka au sahau kuhusu hilo!

Majira au wakati ni dhana ambayo inatembea na haisubiri hivyo yatupasa kutumia sana busara kuikabili ili mwisho wake tuweze kuona faida; mfano tu binadamu tunapitia majira makubwa matatu, kuzaliwa ; kipindi cha mpito cha kuishi na hatimaye kifo; hivyo kwa sentensi moja ninaweza sema Majira ni  ni kila kitu katika maisha yetu. Lakini tunatakiwa tukumbuke kuwa Mungu ndiye kila kitu katika majira yetu kama Isaya  55:8-9 anavyosema maana mawazo yangu si mawazo yenu wala njia zenu sio njia zangu, zi juu sana kuliko njia na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji kutoka mbinguni wala hairudi huko bali huinywesha ardhi na kuizalisha na kuchipuza ikampa mtu apandaye mbegu na mtu alaye chakula;

Tafakari yetu leo inatuonyesha jinsi Majira yanavyoweza  kukuletea  furaha, chuki, mafanikio,utajiri na kumpenda Mungu; tukimwangalia mkulima anahitaji kujua wakati gani  wa kupanda mazao yake  na wakati gani atatakiwa  kuvuna. Hii inamsadia kufanya maandalizi yanayofaa kwa ajili ya mbegu na matayarisho ya shamba na hata matayarisho ya ghala la kuhifadhia mazo pindi akimaliza kuvuna.

Mwekezaji anahitaji kujua wakati gani akitaka kununua kahawa itakuwa tayari kwa manunuzi;  hii itamsaidia kujiandaa kuwa na fedha ambazo atakuwa anahitaji kwa manunuzi ya kiasi kila ambacho anahitaji, kuandaa namna ambayo atakuwa akisafirisha mazao aliyonunua; na wapi atauza mazao yake na itamchukua muda gani kuweza kuuza mazao yake.

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa tupende tusipende hatuwezi kushindana na wakati; hata kuongea kwetu kwa afya njema yatupasa tuzingatie majira/wakati kuna wakati wa kuongea na wakati wa kukaa kimya; 

Je tunampa Mungu wakati mzuri wa kutafakari zawadi ya maisha ambayo tunayo; Mungu ametupa uwezo wa kuweza kutawala majira yetu kwa namna tupendavyo. Tukumbuke kuwa ile tuweze kuutumia wakati wetu vizuri bado tunahitaji masaada wa Mungu.

Najua wakati mwingine tunapata wakati mgumu wa kuelewa ugumu wa majira hasa pale ambapo mategemeo yetu  na matokeo yetu yanakuwa tofauti. Kwani wakati unasonga mbele bila kuwa na mafanikio ambayo tulikuwa tunayafikiria utayapata. Kalalamika, kukasirika, kugombana au hata kuuana kamwe hakutasimamsiha wakati bali kutaendelea kuleta wakati mgumu zaidi. Kama binadamu tunaishia tu kusema Ninge…… ninge… lakini huwezi simamisha wakati hata kwa sekunde moja tu. Sisi binadamu mara nyingi tumekuwa ni watu wa kujisahau na kujua kuwa tunaouweza wa kuuchezea na kubadilisha wakati/majira ili uweze kwenda sambamba na matakwa yetu ya maisha.

Ni mungu peke yake anayeweza kusimamisha majira au wakati; tukiangalia ukuu wa mungu wa milele tunaona kuwa wakati au majira yote yako mikononi mwake nay eye anaweza kupanga vile ambavyo anataka iwe;  hata pale ambapo sisi hatuelewi yeye tayari ameshakuwa na mipango yake endelevu juu yake.  Hata majira mazuri ambayo tunayafurahia tayari yamepata kibali cha Mungu. Mungu anapanga  majira yote kulingana na kalenda yake na sio kalenda yetu. Majira ya mungu hayana mfano ni mazuri na yanaleta Baraka kwa watu wake.

Tukisoma litabu cha warumi 8.28 tunakumbushwa kuwa  katika mambo yote Mungu hufanya kazi kwa manufaa ya wale wanaompenda, walioitwa kwa kusudi lake. Mungu amefanya kila kitu kizuri kwa wakati

Mungu ameumba vitu vyote kwa wakati wake kwa faida yetu japo tumeshindwa kutimiza maelekezo yake, tukakimbilia zaidi anasa na dunia na mambo ambayo sisi tunafikiri ya maana kumbe sio ya maana kabisa, tukaacha kufanya mambo yenye faida kubwa kwetu tukifikiri kuwa wakati utaendelea kutusubiri. Tukasahau kuwa haya mambo ya dunia yanakuja na kupotea na kamwe hatutaridhika wala hatutosheka  kabisa. Majira na wakati ulio nao unatakiwa kutupa sisi hamu ya kuonja maisha bora ya mbinguni.

Ni sawa kama unakwenda kwenye sherehe  mategemo ambayo wengi tunayo ni kupata chakula kizuri na kingi ambacho kitatosheleza haja ya mwili wako ukizingatia wakati wako ambao umetumia;  cha ajabu kama ukifika hapo na wakawa wanatoa tu chakula kidogo na chepesi ni wazi kuwa utakasisirika kuwa umepoteza wakati wako; lakini kumbe tatizo hawakusema kuwa hicho ni kisafisha kinywa, na wakatangaza baadae kuwa tusubiri mlo kamili unakuja, utaridhika na kufurahi  hata kama utasuburi kwa muda mrefu hutajali kuhusu muda unaopoteza kwani  haja ya moyo wako itakuwa imekamilika.

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa kwa vyovyote vile tunavyofikiria kuhusu majira kamwe hatuwezi kubadilisha mipango ya mungu; yeye ndiye aliyeweka mchana na usiku, yeye ndiye aliyeweka siku, yeye ndiye aliyeweka masika na kiangazi: kama mzaburi 31.15 anavyosema nyakati zangu zimo mikononi mwako,Uniponye na adui zangu, nao wanaonifuatia.  Kitabu cha Maombolezo 3.25 Bwana ni mwema kwa hao wamngojeao, kwa hiyo nafsi imtafutayo. Kwa maneno mengine majira ya Mungu ni ya uhakika kwa mafanikio yetu.

Tafakari ya leo inatukumbusha jambo moja kubwa Sisi binadamu  tunapaswa kushukuru  mungu siku zote na kwa wakati wote; japo hatuwezi kuelewa mipango ya Mungu juu yetu bado tuna wajibu wa kuendelea kumshukuru mungu wakati wote; Mungu ana makusudi yake juu yetu kuhusu utendaji wake kwetu kwa wakati wake na sio kwa wakti wetu. Mungu anajua nini tunahitaji na kwa wakati gani. Kwa hiyo Majira au Wakati wa Mungu hauna mbadala.

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa maisha yetu yamejaa SUBIRI; Japo ni kitu ambacho hatukitaki lakini ukweli utabaki kuwa ukweli KUSUBIRI ni sehemu ya maisha yetu; kwani wengi wetu ni afadhali kufanya kitu chochote kuliko kusubiri. Baadhi yetu ni afadhali kufanya kitu kibaya kuliko kusubiri.

Ukweli lazima usemwe; Msingi mkubwa wa maisha   ni kusubiri. Tunausubiri ili tuweze kumwona daktari. Tunasubiri ili tuweze kumaliza shule na kuhitimu. Tunasubili ili tuweze kupata nafasi ya kukubalika na Kuingia  katika chuo. Tunasubiri  kwa ajili ya kuanza kazi kwa mara ya kwanza. Tunasubiri kuona kama benki itaweza kutoa mkopo. Tunasubiri kwa Bwana kuleta mume au Mke bora ndani ya maisha yetu. Tunasubiri Kwa mwenyezi Mungu kujibu sala zetu.

Je, umewahi kujiuliza kwa nini Mungu hasemi nasi kwa uwazi zaidi? Inawezekana ni kwa sababu wewe unakwenda kwa mwendo kasi na hivyo  huwezi kusikia sauti yake? tunatakiwa tutafakari vipaumbele vyetu, kupunguza  mwendo kasi wetu na kuangalia upya ratiba yetu, kwa kufanya hivyo tutaweza sisi kupata nafasi ya kusikiliza sauti ya Mungu. 

Hii ni tafakari yetu ya leo Amina



No comments:

Post a Comment