WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Tuesday, February 2, 2016

MBINU ZA KUKUA KIROHO




February 2

Tafakari ya leo tunakumbushwa kujitambua na kuona kuwa  kuna umuhimu mkubwa wa kujiwekea Mkakati binafsi katika ukuaji wa kiroho.  Ukuaji wa kiroho ni njia pekee ambayo inatunganisha sisi binadamu na Mungu: pamoja na kupotea kwetu katika safari hii ya Kiroho bado Mwenyezi Mungu kupitia Bwana wetu Yesu Kristo anatumia mambo mawili katika maisha yetu ya kutusaidia kurudi kwenye njia sahihi; ni kupitia neno lake na kwa sisi wenyewe kundelea kuomba na kushukuru.

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa Mungu anazungumza nasi kupitia Neno lake na sisi kujibu kwa maombi. Tukitekeleza hilo ukuaji wetu wa kiroho huleta maana; Yesu alisema kwamba kama tunampenda wajibu wetu kushika amri zake. sisi ni wafuasi  Kristo moja ya wajibu wetu mkubwa ni kuendelea kumtafuta  na kutii maelekezo yake.

Tunaonywa kuwa ili tufanikiwe kukua kiroho tunatakiwa  kuwa msatari wa mbele katika kuonyesha upendo wa Kuwahudumia wengine na kuondokana na dhana ya  ubinafsi ambao ndio hulka kubwa kwetu. Tunajua kuwa Mwenyezi Mungu ana majukumu katika mchakatowa mabadiliko ya maisha yetu, lakini anataka yaanzie kwetu. Na tukumbuke kuwa ni wajibu wetu sisi kushirikiana na Mungu  Yeye daima hufanya kazi ndani yetu. Tukisoma kitabu cha waefeso 2:10 Kwa maana sisi tu viumbe vyake - tuliumbwa katika Kristo Yesu tutende matendo mema; na tukumbuke Mungu hufanya kazi ndani yetu kupitia sisi wenyewe.

Neno la Mungu heleta mabadiliko makubwa ya kiroho ndani yetu; tunapompokea Roho mtakatifu na kuamini katika uwepo wake ndani ya nafsi zetu ndipo  safari ya kiroho inapoanza na kutujengea maisha bora kabisa ya kiroho. Ukimpokea roho wa kweli huleta mageuzi ndani ya ya maisha yetu. Tunakuwa tayari katika hatua za kutimiza  wajibu wetu wa kumwambia Mungu tuko tayari kwa maisha mapya ya ukuaji wa kiroho; hivyo Mungu huanza kazi yake ndani yetu ambayo inaamsha mabadiliko ya maisha yetu.

Tukumbuke kuwa Yesu alipopaa Mbinguni aliwaambia wanafunzi wake nitawaletea msaidizi ambaye ni Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu hutupa sisi;  nguvu , hubadilisha mfumo mbaya wa maisha yetu;  Roho wa Bwana hukaa mahali pasafi na penye neema ya Kimungu. Hivyo Roho wa Mungu  husaidia kubadilisha mazingira yetu mabaya yaliyojaa dhami kwani uwepo wa Mungu ndani yetu hudhiirisha usafi wa mazingira yetu;

Mtume Paulo anatukumsha kuwa wokovu Ni zawadi ya bure ni  neema ya Mungu ambayo lazima ianzie kwetu. Kwa kweli tunatakiwa kuishi maisha kama Kristo: Yatupasa kusali bila kuchoka, na kushukuru kwa kila jambo; kwa kufanya hivi ukuaji wa kiroho utaweza kukamilika ndani yetu;

Tunatakiwa kudumu katika maombi; walipo wawili au watatu wakisali pamoja nami nitakuwa katikati yao; hivyo inatupasa  kujiepusha na upweke, na tudumu katika  ibada, kutoa fungu la kumi, kuwahudumia wahitaji wagonjwa, wajane na wenye shida mbalimbali na kuwa mtu mwaminifu. Sisi kama wanafunzi wa Yesu; yeye alitimiza wajibu wake kama mwalimu kwa kuwasilisha ukweli kuhusu Mungu; wajibu mwanafunzi kuwa tayari na kukubali kujifunza na kuwajibika ili kupata elimu anayohitaji kwa hiyari yake.

Mtume Paulo, anatukumbusha kuwa katika mpango wa kukua kiroho tunatakiwa tutazame mambo yaliyo mbele yetu na kukaza mwendo kufikia yaliyo  bora katika kufikia hatua ya mwisho ya wokovu  ambayo ni zawadi ya pekee ambayo Mungu ametutayarishia mbinguni kupitia Mwokozi wetu Kristo Yesu.

Hii ni tafakari ya leo amina



No comments:

Post a Comment