WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Thursday, February 4, 2016

MDOMO WAKO UWE NI NURU YA MATAIFA;



February 4

Tafakari ya leo hebu tuangalia umuhimu wa kutumia mdomo  vizuri ili uwe nuru kwa mataifa. Tunakumbushwa kuwa wakati wa kufungua mdomo na kuanza kufanya mawasiliano tunashauriwa tuutumie mdomo wetu kwa faida ya wote na kuondoa mashaka ambayo yanasababishwa na Mdomo. Kitabu cha Zaburi 19:14 kinasema Maneno ya kichwa change, na mawazo ya moyo wangu, yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu, na mwokozi wangu.

Tafakari ya leo inatuasa mdomo hufanya mambo kadhaa kutengeneza maneno na mawazo kulingana na mazingira ya moyo kutafakari maneno hayo kabla ya kufanya hatua ya mwisho ya kuyatoa kwa kusema kwa mtu mmoja na kikundi cha watu ili kufikisha ujumbe kutoka ndani ya nafsi yako; hivyo kwa kumsikiliza mwongeaji hivyo unaweza kujua kabisa; kuwa anaongea kutoka katika mazingira gani;

Leo tunashauriwa kuwa wakati mwingine ni bora kufunga mdomo wako na kuonekana kama ni mjinga, kuliko kusema kitu cha kijinga na kisha watu wakajidhihirisaha kuwa kwa kupitia mdomo wako umeonekana kweli ni mjinga. Au wewe ni katili au wewe sio mtu ambaye unahofu na Mungu.

Kupitia mdomo wako unaweza kukufundisha unyenyekevu wa kufikiri na kuongea pale tu panapopaswa kuongea au kushauri kitu ambacho unakifahamu na unauhakika nacho. Mdomo wenye kheri huwa na subira, na utafakari kabla ya kusema; na unakufundisha kukubali kwamba hujui kitu,  na kutumia mdomo wako kujifunza kwa kuuliza maswali na kujifunza kwa ufanisi zaidi.
Tukisoma 1 Peter 3:10 kwa maana, atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila.

Kwa Msingi huu ukiwa na mdomo wenye unyenyekevu; mdomo wako unakuwa na subira na unakubali kuwa haujui kila kitu; na kukubali kuwa wakati mwingine unakuwa mjinga mwerevu anayekuwa tayari kujifunza kupitia mdomo na hatimaye kuwa nuru kwa mataifa;

Je umewaona wale ambao  hujifanya kujua kila kitu kupitia midomo yao na kuwapotosha wengine? Ni bora kujua kidogo na kuwa nuru ya mataifa kuliko mdomo wako kuwa na ujuwaji mwingi na kuwaangamiza walio wengi.

Marko 7:20-23 anatukumbusha kuwa kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati. Wivi, uuaji, uzinzi, tama mbaya, ukorofis, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi upumbavu. Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani ya moyo na kutekelezwa kwa mdomo.

Tafakari ya leo inatukumbusha ushawishi wa mdomo uwe kwa ajili ya nuru ya mataifa na sio kuwa sababu ya maangamizo ya mataifa. Mdomo hutengeneza maneno, na maneno haya yawe ni nuru kwa mataifa. Mdomo wako usitumike katika kuwahukumu wengine. Mdomo wako uwe ni hakimu wa haki; mdomo wako uwe ni kioo cha haki; mdomo wako utangaze amani, upendo na sio kuwa daraja la chuki au utengano au mafarakano; Mdomo wako usiwe daraja la rushwa, wizi  au ufisadi; mdomo wako usiwe ni sababu ya udikteta na ukandamizaji; Je mdomo wako uko katika ngazi gani?

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa lazima tujenge hofu ya Mungu kupitia midomo yetu; zaburi ya 50: 19,20 umekiachia kinywa chako kinene mabaya, na ulimi wako watunga hila. Umekaa na kumsengenya ndugu yako, na mwana wa mama yako umemsingizia. Hili ndilo tatizo ambalo tunalo na ni kubwa kwa jamii yetu sasa. Tumekuwa sio watu ambao ni wakweli katika kutimiza wajibu wetu; tunatumia nguvu nyingi kupitia midomo yetu katika kumtia hatiani mtu mwenye haki ili tu tufurahia starehe fupi katika ulimwengu huu. 2 wakorinto 13:5.


Tafakari ya leo inamaliza kwa kusisitiza kuwa mdomo ukitumika vizuri una nguvu ya kuponya, kubariki, kukwemea maovu, mapepo; kuleta Baraka; kwani kwa neno tu Mungu aliumba ulimwengu huu, Tukijikumbusha Kitabu cha Mwanzo 1:3 Mungu alisema, Iwe nuru; ikawa Nuru. Na tunatumia midomo yetu kuomba msamaha kwa Mungu- hivyo MDOMO WAKO UWE NI NURU YA MATAIFA – AMINA.

No comments:

Post a Comment