WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Wednesday, February 10, 2016

HAKIKA SISI NI MAVUMBI MBELE YA MACHO YA BWANA.




February 10,

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa asili ya binadamu ni vumbi , tuliumbwa kwa udongo na tukapewa neema ya mwili wa utukufu, lakini tukaukana utukufu huo kwa dhambi ya kutosikiliza maagizo ya Bwana; kutokana na dhambi hii basi kwa udongo tutarudi mwisho wa maisha yetu hapa dunia. Zaburi ya 49:11 itatueleza kuwa Makaburi ni nyumba zao hata milele; maskani zao vizazi hata vizazi; hao waliotaja mashamba yao kwa majina yao wenyewe. Mwanzo 3:19 kinatukumbusha kuwa  kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe,nawe mavumbini utarudi.
Tafakari ya leo inatukumbusha kuanza kwa kipindi cha mfungo wa siku arobaini katika kipindi hiki cha Lent; 

Lengo kubwa la mfungo huu  ni kujitathimini sisi wenyewe wafuasi wa Kristo na kuona je njia zetu za kila siku katika maisha yetu zinampendeza Bwana; Kama sivyo basi tunatatkiwa kutubu; hii taathimini inatutaka kuwa waaminifu na matendo yetu katika maisha yetu, Je matendo yetu ni yale ambayo yanatakiwa mbele ya Mungu? Na kama sivyo je toba yangu itanisaidia mimi kuondoka katika njia hizi mbaya?

Hiki ni kipindi ambacho tunatakiwa kutumia muda wetu mwingi pekeyetu na Mungu, ni wakati wa kufunga na kujinyima kwa kweli kwa faida ya uokovu war oho zetu; ni kipindi ambacho tunatakiwa  kitabu cha Mathayo 6:20-21 anapotukumbusha kuwa  msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; bali jiwekeeni hazina mbinguni kusikoharibika kitu hakuna nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi. Kwa kuwa hazina yako ilipo ndipo utakuwapo na moyo wako.

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa tunapojitathimini wenyewe tukumbuke kuwa sisi ni wadhaifu ambao tunahitaji msaada, na sio watu wenye afya njema ambao hawaitaji matibabu. Tu wadhaifu hivyo tunaomba huruma ya Yesu katika kipindi hiki cha toba kwani tumekwenda kinyume na sheria za bwana na Bwana wetu Yesu Kristo yuko tayari kutusikiliza na kutusaidia. Lakini tunatakiwa kukumbuka kuwa sisi ni mavumbi na tutarudi mavumbini, hata kama wakati mwingine kutokana na mafanikio yetu hatuko tayari kukubali ukweli huu lakini ni ukweli usiopingika kuwa maisha ni zawadi ambayo tumepewa na Mwenyezi Mungu, hivyo hatutakiwi kuichukulia kama haki yetu. Hivyo tunakila sababu ya kufunga na kutubu dhambi zetu katika kipindi hiki cha Kwaresima; ni wakati mzuri wa kujichunguza ni kipindi ambacho tunatakiwa tumpe Mungu mioyo yetu ili aweze kuichunguza ili kupitia microscope (darubini) yake aweze kuisafisha na kuondoa wadudu wote wabaya wanaoharibu maisha yetu kwa maagizo yake kupitia Bibilia.

Tafakari ya leo inatupa wakati mzuri wa kutafakari kitabu cha Yoshua 1: 8 aliposema  Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana. Ni kweli ni wakati mzuri wa kutafakari maagizo ya Mungu ili kupata kibali cha maisha ya utukufu ambao tumeandaliwa katika maisha yetu ya baadae. 

Tukisoma kitabu cha Mathayo 6:16-18 tunataadhalishwa kuwa tunatakiwa kuwa wanyenyekevu wakti huu wa mfungo; Basi mfungapo, msiwe kama wanafiki wenyeuso wa kukunjamana; maana hujiumbuanyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Aminnawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe ufungapo,jipake mafuta kichwani, unawe uso; ili usionekane na watu kuwa umefunga, ila na Baba yako aliye sirini, na Baba yako aonaye sirini atakujazia. Tunatakiwa kuwa makini na kuepuka tabia za kiunafiki katika kipindi hiki, kiwe kweli ni kipindi cha Toba na kumrudia Mungu. Mithali 2:1-5 Mwanangu, kama ukiyakubali maneno yangu, Na kuyaweka akiba maagizo yangu; hata ukatega sikio lako kusikia hekima, Ukauelekeza moyo wako upate kufahamu; naam, ukiita busara, Na kupaza sauti yako upate ufahamu;ukiutafuta kama fedha, Na kuutafutia kama hazina iliyositirika; ndipo utakapofahamu kumcha Bwana, Na kupata kumjua Mungu 

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa tunatakiwa kuuitafuta na kuisikiliza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, Tumshukuru Mungu kwa ushindi amboa uko mbele yetu kupitia Mkombozi wetu Yesu kristo. Hiki ni kipindi cha kusafisha hekalu letu, tukumbuke kuwa mwili wetu ndio hekalu la kudumu la Mungu. Hivyo tuna kila sababu ya kuhakikisha kuwa linakuwa safi muda wote na kufuata maelekezo ya Mungu katika utimilifu wake. Nawatakieni Jumatano ya Majivu Njema iliyojaa Toba ya kweli mbele ya Mungu wetu Amina.





No comments:

Post a Comment