WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Tuesday, February 9, 2016

JE WEWE NI MTU WA SHUKRANI?





February 9

1 Wathesalonike 5:18 , Paulo anaandika, " shukuruni kwa kila jambo maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu. " Paulo anatuagiza bila kuchagua maneno kwamba ni lazima tushukuru kwa kila jambo; katikana hili tumeambiwa hakuna udhuru bali wajibu wetu ni kutoa  shukrani .  Tafakari yetu inatukumbusha kuwa tendo la kushukuru ni la lazima na linatuunganisha na kila jambo katika maisha yetu ambayo yanatakiwa kujaa shukurani, bila kujali nini kitatokea mbele yetu. Lazima tutambue kuwa tendo la kushukuru ni

kiini cha maisha na bora ya Kikristo. Na kuwa wasio na shukrani ni kiini na moyo watu waovu wasio mwogopa Mungu.  Watu wa namna hiyo hawako tayari kumpa Mungu sifa za utukufu kwa matendo yake makuu kwetu. Tunajua kuwa Mungu ndiye muumba wa kila kitu, mungu ametupa sisi wanadamu uhai, mungu ametupendelea sisi wanadamu na ametupa akili ya utambuzi wa jambo jema na baya; hivyo tuna kila sababu ya kumpa asante kwa zawadi hii kubwa.


Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa tusiwe katika kundi lile wa watu wapumbavu ambao wao wanajua kuwa kila kitu katika maisha yetu vinatokea kwa bahati na hakuna mkono wa Mungu juu yake, hivyo kwani wawe ni watu washukurani? Wamshukuru nani wakti vitu vyote vinatokea kwa bahati? Ni kweli utawezaje kuishukuru Bahati na bahati haina hata bahati kwa yenyewe? Watu wa aina hiyo ni wanyama hawana kabisa moyo wa utu na wa ubinadamu ndani yao; 

Tafakari ya leo pia inatumbusha kuwa tujitahidi kujiepusha kundi la watu wanaoamini kuwa hawana shida ya kushukuru kwa kuwa wao wenyewe tayari wameshafanikiwa kimaisha, wanamawazo mazuri, wanao ujuzi wa kutosha kuendesha maisha yao, na mafanikio yote ambayo wanayafurahi ni kazi ya mikono yao bila msaada wa Mungu; sifa za mafanikio yao ni katika mikono yao na akili zao kwa mipango yao, bidii yao; ujuzi wao na mbinu za ubunifu ambazo wanazo; sasa kama wao ndio vinara wa mafanikio yao nafasi ya mungu iko wapi? Na kwa nini wamshukuru? Hivyo wanajipongeza wenyewe kwa sababu wao wenyewe ndio mafundi na masonara wa maisha yao. 

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa dunia hii ukiangalia imeundwa na makundi matatu ambayo hayana shukrani kwa Mungu. Kundi lile linaloamini kuwa wao maisha yao yamejengwa katika bahati hivto hawana sababu ya kumshukuru Mungu; Kundi la pili ni lile linalofikiri kuwa hawaamini katika uwepo wa Mungu ila kuna nguvu tu ya aiana yake katika mafanikio yao sasa hawaoni sababu ya kushukuru. Na kundi la mwisho linalojiamini kuwa wao ndio sababu ya mafanikio yao na maendeleo yao sasa kunasababu ya kutoa shukrani? Na kama ndio sasa wamshukuru nani, kwani wanastahili kujishukuru wao wenyewe.

Tunachojifunza hapa ni kuwa wajibu wa shukrani uko mikononi mwa watu wote wanaoamini katika ukuu wa mungu na matendo yake makuu katika maisha yao. Wakristo wanapaswa kumshukuru Mungu kwa kila jambo; Shukrani ni jambo muhimu sana katika maisha yetu kama wakristo. Ni ukweli usiofichika kuwa kuna wakristo ambao sio watu wa shukrani. Je wewe unamshukuru hata jirani yako aliyekutendea jambo njema? Ni rahisi kumwona Mungu kupitia upendo wa jirani yako; hivyo tunakila sababu ya kusema asante Mungu kwa wema wa Jirani yangu.

Tukisoma Warumi 8:28 nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendaokatika kuwapatia mema yaani wale walioitwa kwa kusudi lake. Mungu anafanya kila jambo kwa ajili ya mafanikio yetu hivyo tuna kila sababu ya kumshukuru; na kama tuanaamini kuwa Mungu yuko kazini katika maisha yetu, na kubadilisha maisha yetu kuelekea katika maisha bora, tuna kila sababu ya kusema asante. Hata tunapopatwa na shida bado twatakiwa kushukuru kwani hatujui nini hatiam ya maumivu yetu. Kwa Mungu baada ya maumivu yetu mwisho wake ni kheri. Hata unapofanyiwa upasuaji wa tunashuhudia maumivu makali lakini hatima ya maumivu haya makali ni uponywaji wa kudumu.

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa tuwe watu wa shukrani kila wakati na katika mazingira yeyote yale. Amina


No comments:

Post a Comment