WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Tuesday, November 8, 2016

WEWE UNAKUBALI UMEBARIKIWA?


November

1 wakorinto. 12.13

Tafakari ya neno kubalikiwa lina maana pana na sio ile ambayo imezoeleka ya kufurahia mafanikio au raha hasa za kimaisha yetu ya kila siku; na mara nyingi tunafurahi sana tunapofanikiwa katika maisha yetu na hapo kwa sauti ya juu tunaimba na kushukuru kuwa tumebarikiwa; wote tunahitaji kubarikiwa na kufurahaia maisha yetu ya kila siku katika ubora wake wa khali ya juu. Nami  najua kabisa hakuna mtu hata mmoja katika misha yetu ya kila siku ambaye hukataa maisha mazuri ya Baraka.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa mara nyingi tunapoangalia kubarikiwa tatizo letu tunaangalia Baraka katika upande tofauti nap engine kwa namna ya pekee; tukiangalia kuwa Baraka asili yake mafanikio ya asili; kwa msingi huu pale tunapokaa kwenye nyumba nzuri, kazi nzuri,gari nzuri na kadhalika kwetu tunajiona kuwa tumebarikiwa na tunafurahia sana na tunaimba aleluya kwa Mungu ametubariki; warumi 8:17 na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye. 

Tafakari yetu inataka tujiulize je pale inapotokea pengine tunaumwa; au unaendesha gari ambalo sio nzuri au unaishi katika nyumba ambayo sio nzuri; je hapo tumekuwa tumepoteza Baraka za Mungu? Au pale maisha yanapokuwa magumu ha uwezo wa kifedha umeondoka na hatuwezi kuyakabili msiaha kwa ujumla je hapo Baraka za Mungu ziko wapi? Nafikiri kuwa tatizo letu tunaangalia Baraka katika mwelekeo mmoja tu wa mafanikio na sio shida; katika mwelekeo huu wa kuwaza kutumbuke kuwa Gari linaweza toweka siku moja, pesa zinaweza toweka siku moja, hivi vitu vyote ambavyo tunavyoviona katika macho ya kidunia ni njia ya kutusaidia sisi ili tuweze kuzifikia barka za Mungu katika ukamilifu wake; tujue kuwa hivyo vyote ni vya muda tu lakini Baraka na neema za Mungu ni za kudumu. Hata afya yetu siku moja itaporomoka na hatutaweza irudisha tena;  hivyo tunatakiwa kufahamu kuwa Baraka za kweli sio mali ni vyote vinavyotuzunguka bali baraka ya kweli ni roho wa Mungu ndani yetu; Warumi  8:28-31 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza. Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu? 

Tafakari yetu inaendelea kusisitiza kuwa Je ni furaha ya namna gani pale ambapo vyote vimetoweka lakini bado unaendelea kumiliki Baraka za Mungu , hivyo ni wajibu wetu sasa kutambua Baraka za Mungu ndani ya Maisha yetu; halafu kitu ambacho tunatakiwa tujivunie ni utambuzi kuwa tayari Mungu ameshatujalia Baraka katika maisha yetu; katika wakati uliopita ,wakati wa sasa na wakati wa baadae;lakini Mungu ametupa sisi vitu vyote vya kutupatia na kutuongoza kuishi katika Baraka zake, ili tuweze kuwa washindi, ili kutusaidia kuwa watiifu, na kuwa na thamani katika maisha ya Kimungu katika ufalme wake;

Tafakari yetu tukisoma Waefeso  2:12, kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani.  tukumbuke kuwa  tumepata kibali cha baba na tumelelewa  kwa damu ya Yesu; hivyo njia pekee za kufurahia Baraka za Mungu lazima tuuishi wokovu na neema ya Mungu itubariki, hivyo tunatakiwa tuziangalie Baraka zetu kutoka katika mpangilkio na mwelekeo wa Kimungu; hapa tutaweza kutambua kuwa kila kitu ambacho kipo mbele yetu kimebarikiwa kweli kweli; hapo tutatambua kuwa Mwenyezi Mungu ametubariki sisi san asana ambazo hazipimiki hivyo wajibu wetu ni sisi kumshukuru Mungu kwa Baraka hizo hata kama tunakabiliwa na matatizo mengi ya maisha lakini wajibu wetu ni kumshukuru na kumsifu Mungu kwa Baraka zake juu yetu .

Hii ndio tafakari yetu ya leo Amina
Emmanuel Turuka




Monday, November 7, 2016

JE UNATAMBUA KUWA MLANGO ULIOFUNGWA NI BARAKA?


NOVEMBER

Tafakari yetu leo tujikumbushe ujumbe huu mzuri kuwa kama una imani mlango wa matumaini utafunguliwa dhidi yako; tunajua kuwa maisha yetu hayajejengwa katika mstari ulionyoka ambao sisi tunatembea tukiwa huru; bali ni safari ambayo huwa ina vikwazo, vigugumizi, mabonde, milima na mapingamizi  ambayo tuwapo safarini lazima tuwe tayari kukabiliana navyo, na urahisi wa kushinda vikwazo hivi ni kuwa na imani inayotakiwa. Hivyo tukiwa na imani tuwe na uhakika kuwa mlango utafunguliwa;

Tafakari yetu inatufundisha huu ukweli ambao haupingiki kuwa kujifunza tofauti kati ya imani na kuamaini ni kitu ambacho tunatakiwa kukifanya kila siku katika maisha yetu yote; ndio maana mafundisho yanatukumbusha kuwa  Mungu anapenda sisi tumwamini yeye kwa akili zetu na kwa dhamira zetu bila shuruti; na tutaweza kumwamini yeye kwa matendo yetu na katika shida zetu; tukiamini kuwa yeye pekee ndiye kimbilio letu katika mahitaji yetu;
Tafakari inatukumbusha kuwa matumaini na kumwamini mungu lazima yaanzie kwetu kupitia maombi yetu ya kusifu na kushukuru; Tumkumbuke Ayubu pamaoja na shida na magonjwa aliendelea kumtumaini Mungu na Mungu alimbariki; Kama ilivyotokea kwa Ayubu nasi tumaini letu katika mahangaiko yetu ni  imani na matumaini makubwa ambayo tunatakiwa tuyatangulize mbele ya Mungu, kwa kufanya hivyo Mungu hufunga mlango wa mateso na kwa kweli huwa hauana faida na maisha yetu na kukufungulia Mlango mwingine ambao umejaa matumaini; Mungu huonyesha njia kupitia mlango ambao umefungwa na ule ambao anaufungua kwa ajili maisha yetu; Mwenyezi Mungu anapofunga mlango mmoja anataka wewe ubadilisha mwelekeo wako wa maisha; na unavyobadilisha mwenendo wako wa maisha na ili uweze kutembea katika mafanikio na neema ya utukufu wako kupitia mlango mpya alioufungua kwako;

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa tatizo letu mara nyingi tunajikwaa katika barabara yenye makorongo ambayo imetengenezwa kwa lami ambayo imejaa mashaka na kukosa imani; lakini mwenyezi Mungu daima hututembeza katika barabara iliyo imara na bora yenye imani kubwa ambayo hutuongoza sisi katika mlango ambao umejaa matumaini na kutufungulia mlango ambao hatukuutegemea kabisa; mungu wakati mwingine hata hatuambia kuwa tuende kushoto au kulia yeye anachofanya ni kufunga mlango ambao hauna faida kwetu na kutufungulia mlango ambao umejaa neema. Hivyo wakati mwingi mlango ukifungwa ni neema vile vile.


Tafakari tunatakiwa tuendelee kushukuru hata tukiwa kazini tunapopatwa na mitiani mbalimbali  iyojaa fitina, chuki na kadhalika mshukuru Mungu kwani kuna neema kubwa inakuja mbele yako. Tukumbuke kuwa Mungu anayaendesha maisha yetu upendo wake hufunga na kufungua milango ya kuingia na kutoka katika maisha yetu; Tunajua kuwa inakuwa ngumu katika ubinadamu kulikubali na kulishukuru hilo mara moja. Tukumbuke kuwa Daima Mungu anatemebea mbele yetu, anajua mapito yetu kabla sisi hatujeyajua yeye ni kinga yetu ya kweli; ndio maana siku zote tukiwa na imani hutuepusha na mabaya yote mbele yetu; lakini kwa sababu ya kukosa kwetu hekima sisi tunajiona kuwa tunajua na kumsukuma pembeni lakini baada ya kumsukuma na kupata matatizo tunarudi na kuanza kumlilia huku tukimlalamikia sana kwa nini umenifanyia hivi na hivi.

Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa tunapopatwa na tatizo kwa kiwango chochote kila Mungu tayari anakuwa ameshajua tatizo na suluhisho lake; anachohitaji kutoka kwetu ni sisi kumwamini yeye na kutekeleza sehemu yetu ambayo ni maisha kulingana na maagizo yake; na jukumu letu nyingine ni kuendelea kusali na kumshukuru; na tukumbuke kuwa tutafanikiwa kwa kusoma vitabu vyake na kuamini kuwa yeye ndiye suluhisho la matatizo yetu yote:

Hii ndio tafakari yetu ya leo tumtumaini mungu katika njia zake na katika maamuzi yake kwetu ili tuendelee kupokea Baraka zake bila kikomo. Amina

Emmanuel Turuka




Tuesday, October 11, 2016

JE WEWE NI MTUMISHI?

Tafakari ya leo tuangalie dhana ya utumishi ambayo Yesu aliwaambia wafuasi wake,  yule anayetaka kuwa mkubwa lazima awe mtumishi.  Yesu alikuwa na maana gani alivyosisitiza dhana hii?

Sunday, October 9, 2016

NENO LENYE NGUVU LINATOKA WAPI?

Tafakari yetu Leo inatukumbusha kuwa matendo yetu ni zao la neno , la kujiuliza je chanzo chake kinatoka wapi? Je tunasikiliza neno kutoka wapi? Neno lenye nguvu linatoka wapi?

Saturday, October 8, 2016

FAIDA YA KUWA NA KIBURI NI NINI?

Tafakari ya Leo tuangalie faida ya kiburi katika maisha yetu ya kila siku na katika kumfuata Yesu Kristo. Je unapata faida gani kwa kuwa mtu uliyejaa kiburi. Ni wakati mzuri wa kuyatathimini maisha yetu na kupima kwa karibu faida na hasara ya kujijengea kiburi katika maisha yetu.

Friday, October 7, 2016

JE UNAJIONA MWENYE HATIA MBELE YA MUNGU?

Tafakari ya Leo tuangalie dhana nzima ya kuwa na hatia? Swali la msingi je wewe unajiona kuwa na hatia mbele ya jamii na Mungu katika msingi wowote ule? Hatia ya kitu chochote kile?  Kama ni  ndio umeipima hatia yako katika kigezo gani?

Wednesday, October 5, 2016

JE WEWE MAISHA YAKO YAMEJAA AIBU?

Tafakari yetu ya Leo tuangalie dhana ya aibu ndani ya maisha yetu. Aibu inatokana na nini? Je tunaweza kuikwepa aibu?

Friday, September 30, 2016

UWEZO WA KUPIMA MAPUNGUFU YETU UNATOKA WAPI?

Tafakari ya Leo tujiulize je uwezo na hekima ya kupima mapungufu yetu tunaupata wapi? Je maisha yetu yamekamilika na  hatuna mapungufu?

Thursday, September 29, 2016

KWA NINI TUNAKAWAIDA YA KUFANYA MAAMUZI KATIKA JAMBO MOJA?

Tarafakari yetu Leo tunaangalia upungufu wetu ambao tunao, kamwe hatuangalii ukuu wa Mungu juu ya maisha yetu. Bali sisi maamuzi ya kushukuru au kulaani huangalia jambo moja ambalo tunalitilia mkazo.

Wednesday, September 28, 2016

KULA NA KUNYWA KWETU KUNATOKA WAPI?

Tafakari yetu Leo tuangalia je yote ambayo Mwenyezi Mungu ametufanyia ameyafanya kwa upendo mkuu. Tukisoma Mhubiri 3: 11,13 Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho. 13 Tena ni karama ya Mungu kila mtu apate kula na kunywa, na kujiburudisha kwa mema katika kazi yake yote.

Tuesday, September 27, 2016

UNATAKA NIKUFANYIE NINI?

Tafakari yetu ya Leo Yesu anakuuliza wewe unataka ukufanyie nini? Yule kipofu aliomba aponywe ili aweze kuona. Jemedali aliomba mtumishi wake aponywe. Je wewe unataka Yesu akufanyie nini?

Sunday, September 25, 2016

JE WEWE NI MPOLE?

Tafakari ya Leo tujipime kwa kiwango gani wewe na mimi ni wapole.  Je tunaelewa nini maana ya upole na kuwa mfuasi wa kristo? Wafilipi 2:3 Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake.

Friday, September 23, 2016

NI WAJIBU WETU KUSUBIRI

Tafakari ya leo inatukumbusha umuhimu wa kusubiri: Zaburi ya  106:13 inatukumbusha adhaa ya kushindwa kusubiri Wakayasahau matendo yake kwa haraka,Hawakulingojea shauri lake. Mara nyingi tunakosa subira katika kusubiri maombi na haja zetu kupata kibali cha Mungu. Tukumbuke kuwa Mwenyezi Mungu hutujibu kwa wakati wake na sio kwa wakati wetu. Wakati wa Mungu ndio wakati sahihi kupita wakati wetu. Hivyo ni wajibu wetu kusubiri.

Thursday, September 22, 2016

JE WEWE NI TAA?

Tafakari ya Leo tuangalie umuhimu wa taa katika maisha yetu ya imani: Je wewe unaogopa giza, na tunafanya nini kuondoa giza?

Wednesday, September 21, 2016

JE MAISHA YAKO YANA THAMANI:

Tafakari ya Leo tuangalie  nini thamani ya maisha yetu. Je maisha yako yanathamani? Kwa kiasi gani?

JE WEWE UNA AMINI UMEBARIKIWA?

Leo jiulize je wewe umebarikiwa na unaitumiaje baraka hii ya kubarikiwa. Ni tafakari yetu ya leo ambayo inatakiwa kuamsha unyenyekevu ndani ya maisha yetu.

Monday, September 19, 2016

ASANTE MUNGU

September 19


Ni wajibu wetu kushukuru kwa neema ya ufahamu wa maisha yetu kwani daima tumekuwa tukikosa hii busara ya utambuzi; Ni jukumu letu kusema asante;

Sunday, September 18, 2016

AMANI YA KWELI INATOKA WAPI

September  18


Mungu wetu ndio asili ya amani yetu; amani ya kweli huletwa na Mungu na amani hiyo tayari Mungu ametujalia sisi tuweze kuiishi; laniki kwa tamaa zetu tumekuwa chanzo cha kuharibu amani yetu.

Saturday, September 3, 2016

WEWE NI MUNGU

September 3



Tafakari yetu leo ni kweli kuwa Mungu anabaki kuwa Mungu; ni wajibu wetu kumwabudu;

Friday, September 2, 2016

YESU NI BWANA

September 2


Tafakari yetu leo inatuonyesha kuwa ukuu wa Yesu hauna mipaka yuko pande zote za dunia kwa wakati mmoja; Hivyo Yesu ni kimbilio letu;

Wednesday, August 31, 2016

KUTEMBEA NA YESU NI FURAHA



August 31

Luka 10:41-42

Tafakari yetu leo tunaangalia umuhimu wa kutembea na Yesu katika kila hatua ya maisha yetu; dhana ya kutembea ni kitu cha kawaida katika maisha yetu; na tunapotembea katika maisha yetu ya kila siku mara nyingi watu wanaotuzunguka wanatuangalia jinsi tunavyotembea; na hata wakti mwingine wanakuwa na maoni tofauti kuhusiana na matembezi au kutembea kwetu; hii ni tofauti unapomkaribisha Yesu aje kutembea nawe; tukiwa tunatembea na Yesu tofauti yake kubwa ni kuwa uwe unaangaliwa na watu; au matembezi yako yana furaha au ugumu; hiyo haijarishi la msingi tunatakiwa kukumbuka kuwa kutembea na Yesu kunahitaji hatua tofauti kabisa na umakini mkubwa: tukisoma Waefeso 2:8-10  Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;  wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.  inatukumbusha kuwa kutembea na Yesu kunahitaji neema ya Mungu;

Tafakari yetu tukiangalia na kusoma Waefeso 4:1-3  Kwa hiyo nawasihi, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa; kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo; na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani. tunatambua kuwa Mtume Paulo anaainisha jinsi tunavyotakiwa kutembea na Yesu kwa kuzingatia vipau mbele hivi; uvumilivu; unyenyekevu; ubinadamu; upole; kuvumiliana;kupendana;kuimarisha umoja wa waamini kwa kufanya kazi kwa bidii; tukiweza kuzingatia haya kutembea kwetu na Yesu ni rahisi sana na tutakufurahia sana; kama tutaweza kutembea katika msingi huu kinachotokea hapa ni kuwa watu wengine watapata nafasi ya kwanza katika kila kitu unachofanya;watathaminiwa zaidi , watapendwa, wata saidiwa hivyo ndivyo Yesu anavyotamani iwe;

Tafakari yetu msisitizo yatupasa kufanya nini ili tuweze kufurahia kutembea kwetu na Yesu; Waefeso 3:20-21 Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu; naam, atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele Amina. Ili kuweza kutimiza ndoto hii lazima tuweze kujitambua na kukua kiroho; Kukua kiroho kunaendana na kutimiza vipau mbele vyote ambavyo Paulo ameviainisha;

Tafakri yetu inatukumbusha somo nzuri kutoka kwa injili ya Luka 10:38-40 Ikawa katika kuenenda kwao aliingia katika kijiji kimoja; mwanamke mmoja jina lake Martha akamkaribisha nyumbani kwake. Naye alikuwa na umbu lake aitwaye Mariamu, aliyeketi miguuni pake Yesu, akasikiliza maneno yake.  Lakini Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi; akamwendea, akasema, Bwana, huoni vibaya hivyo ndugu yangu alivyoniacha nitumike peke yangu? Basi mwambie anisaidie. Tunachojifunza hapa kuwa kati ya hawa ndugu wawili mmoja aliamua kutembea na Yesu katika matendo yake na Mwingine alikuwa bado anahangaika na maisha ya dunia; sio kwamba mambo aliyokuwa anayafanya yalikuwa hayafai lakini sio katika kipau mbele cha maisha ya kiroho; kama anavyofundisha Luka 10:41-42 Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi; lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa;

Tafakari yetu basi inatufundisha kuwa kwa habari hii njema wewe leo hii ni nani kati ya Mariamu au Martha; Je uko karibu na Yesu kwa kiasi gani? Je unaweza kujihesabu kuwa unatembea na Yesu katika kila hatua ya Miasha yako? Hili ni swali la msingi katika tafakari yetu ya leo, hatujechelewa kumkaribisha Yesu katika maisha yetu; Amina

Emmanuel Turuka





Sunday, August 21, 2016

UWE NAMI BWANA

August 21


Tafakari yetu leo tuendelee kumshukuru Mungu kwa neema ya ulinzi wetu wake juu yetu Yesu  ndiye hutembea nasi kila siku katika maisha yetu; hatuna sababu ya kuhofu wala kuwa na mashaka yeyote yale; Amina

KAA NAMI BWANA

August 20


Tafakari ya leo tuendelee kuomba ulinzi wa Mungu hasa katika kipindi cha mpito wa mashaka yetu pale ambapo tunajua kabisa hatuna msaada mwingine zaidi ya Mungu tu; Mungu daima atakuwa nasi katika maisha yetu yote;

YESU NJOO KAA KWANGU LEO


August  19

2 Timotheo 1:7-8

Tafakari yetu leo inamwita Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ni Mwokozi wetu aweze kuja kukaa nasi; Maisha yetu kama binadamu tunapambana na matatizo na mahitaji mengi ambayo mengine hujisababishia sisi wenyewe na Mengine Husababisha na watu wetu wengine: katika mazingira ya aina yeyote ile hatutakiwi kupoteza imani; kama Mtume Paulo anavyotukumbusha kuwa pamoja na mateso ,kufungwa na kujua kuwa maisha yake yataishia kuuawa bali hakupoteza iamani yake aliendelea kumwamini Mungu kupitia kwa bwana wetU Yesu Kristo ambaya alikuwa anakaa ndani ya Moyo wake; Hivyo ni jukumu letu nasi leo kumkaribisha Yesu katika mwili wetu aweze kuisha nasi katika maisha yetu; tunajua kuwa ugumu wa maisha uko mbele yetu; msongamano wa mawazo uko mbele yetu; haya yote yanavyotokea lazima tuwe tayari kuyakabili, lakini unapomkaribisha Yesu ndani ya maisha yetu changamoto hizi ni rahisi kuzikabili kwani neno lake linatoa faraja kubwa na kufukuza mbali shida zote;

Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa ushindi mkubwa wa msiaha yetu ni kuwa kwani yeye anafahamu hata idadi  ya nywele Mathayo 10:20 lakini ninyi, hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. Sisi hatuna uwezo wa kujua idadi yake lakini yeye anajua; hivyo tunataka zawasi gani zaidi katika maisha yetu kama sio uwepo wake katika maisha yetu? Yesu ni jibu la maswali yetu yote; je nani angeweza kufanya kama Yesu ambaye aliuacha utukufu wake wote na kukubali kuja duniani na kupata mateso, kudharauliwa, kupigwa, kutukanwa na kasha kusulubiwa msalabani kwa ajili yangu mimi? Kwa nini sasa nisimkaribishe Yeye katika maisha yangu? 2 Timotheo 7-8 Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi. Basi usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu, wala usinionee haya mimi mfungwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja nami kwa ajili ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu; 

Tafakari yetu leo inaendelea kutukumbusha kuwa; inatukumbusha mfano wa Yule mama ambaye alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kutoka damu kwa miaka mingi na alikuwa akitafuta tiba kwa kipindi hicho chote; Lakini aliposikia habari za Yesu na ukuu wake alijisemea moyoni mwake namkaribisha Yesu katika maisha yangu, lakini kwa uwezo ambao anao pamoja na kumkaribisha katika maisha yangu nitaligusa tu pindo la vazi lake nami nitapona. Pamoja na umati mkubwa wa watu alifanya kila jitihada za kujipenyeza, kusukuma na watu ambo pia walitaka kumwona na kumsikiliza Yesu lakini walikuwa hawaka tayari kumkaribisha Yesu katika maisha yao ili aweze kuwaponya na matatizo yao; lakini yeye alifanikiwa kumgusa pindo lake kwa imani moja tu kuwa ugonjwa wangu utapona kwa tendo langu na ilikuwa hivyo; hivyo tunamwitaji yesu kwa kuwa Yesu ni jibu katika matatizo yetu:

Hii ndio tafakari yetu ya leo- Amina

Emmanuel Turuka



Friday, August 19, 2016

YATUPASA KUMWANGALIA YESU;

AUGUST 18

Isaya 45: 22-25

Tafakari yetu leo inatuhimiza kuwa yatupasa kumwangalia yeye kama Isaya anavosema; Niangalieni mimi, mkaokolewe, enyi ncha zote za dunia; maana mimi ni Mungu; hapana mwingine.  Kwa nafsi yangu nimeapa, neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki, wala halitarudi, ya kwamba mbele zangu kila goti litapigwa, kila ulimi utaapa.  Mmoja ataniambia, Kwa Bwana, peke yake, iko haki na nguvu; naam, watu watamwendea yeye, na wote waliomkasirikia watatahayarika.  Katika Bwana wazao wote wa Israeli watapewa haki, na kutukuka.

Wednesday, August 17, 2016

MUNGU PEKEE NDIYE ANAYETOA ADHABU NA ZAWADI YA MATENDO YETU:

AUGUST 4


Isaya 55:7-9

August 17

Tafakari yetu ya leo inatukumbusha umuhimu wa zawadi na adhabu; katika maisha yetu ya kila siku tumekuwa watu wa kupenda sana kupokea au kupewa kile ambacho ni kizuri hata kama hatustahili zawadi hiyo; ustahili wa kupokea zawadi stahilivu ni pale matendo yetu yanaonekana wazi kabisa tunatenda haki bila shuruti; tukumbuke kuwa daima Mungu kupitia kwa Bwana wetu Yesu Kristo yeye ndio mwenye usukani nay eye ndiye yeye; Mungu hapendi kutuadhibu sisi anapenda daiama kutupa sisi kile kilicho kizuri na bora kwa ustawi wa maisha yetu hapa duniani na baadae mbinguni; Zaburi 89:14 inatukumbusha kuwa Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako, Fadhili na kweli zahudhuria mbele za uso wako. Daima hukumu ya Mungu imejaa haki tupu;

Tukisoma kitabu cha Isaya 55:7-9 kinatukumbusha kuwa Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie Bwana, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa.  Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana.  Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. Kwa kuzingatia haki ya kweli ya Mungu siku ya hukumu  kutakuwa mgawanyiko wa makundi kulingana na matendo yao lile kundi la wenye haki wataungana na Mwenyezi Mungu katika utukufu wake na lile kundi la watenda maovu watatupwa kwenye moto wa milele jahanamu na watapata adhamu ya milele; kwa huruma na ukuu wa Mungu bado sisi leo hii tunanafasi nzuri ya kuungama dhambi zetu ili tusipate hiyo adhabu ya milele;

Tafakari yetu inatuuliza kama Bwana wetu Yesu kristo alivyowauliza makutano nani ni mtumishi mwaminifu? Yule ambaye katika fikra zake hana kusitasita katika matendo yake mema na yuko taayri kumtumikia Mungu kwa Moyo wake wote; au kundi ambalo haliko tayari kumtumikia Mungu wakijua kuwa bado wana muda wa kutosha hivyo ngoja waendelee kufurahia maisha ya hapa duniani na Mungu watamtumikia baadae wakisha tosheka na maisha ya Duniani? Tukumbuke kuwa Mungu ndio kila kitu utukufu na utawala wote uko juu yake na yeyey ndiye mtawala wa kila kitu. Yeye hutupa zawadi na kutupa sisi adhabu. Je tunakumbuka hadithi ya Mwanan mpotevu; tukisoma 2 Petro 3:9 Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba. Jambo la msingi nikuomba ili kuweza kufanya toba ya kweli.

Tafakari  yetu inatukumbusha kuwa kazi zetu tu hazitusaidii sisi kupata sifa ya kuridhi mzima wa Mungu, bali kazi zetu na utiii ni ishara tosha ya kumwonyesha Mungu kuwa tumepokee neema yake; lakini kama tukiendeleza kiburi na kuto kutii hivyo hiyo ni ishara tosha kuwa hatuko tayari kupokea neema zake; jukumu letu sisi leo tunatakiwa kufanya kila kitu katika uwezo wetu kumpenda na kumtumikia Mungu na kutimiza amri zake kwa msingi kwamba tukitekeleza hili hatutakosa zawadi ya kushiriki utukufu wake mbinguni.

Hii ndio tafakari yetu ya leo Amina


Emmanuel Turuka

Tuesday, August 16, 2016

WAPENDENI WAJANE NA MAYATIMA;

AUGUST 16


Isaya 1:17-18

Tafakari ya leo inatukumbusha umuhimu wa kuwapenda na kuwahudumia wajane na yatima; tujikumbushe nini maana ya kuwa yatima na mjane; katika maana ya kawaida kuwa yatima ni hali ya kukosa wazazi na kuwa mjane ni hali ya kukosa mwenza katika ndoa.  Tafsiri nyingine ya kuwa yatima au mjane tunaiongelea pale tunavpoongelea kuhusu maisha yetu ya kiroho tukiamini kuwa kila mtu amewahi kuwa yatima au mjane kiroho. Kwa tafsiri hii sote tulikuwa yatima wa kiroho mpaka pale tulipo chukuliwa na Mungu waefeso 1:5 Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake. Tukumbuke kuwa  Mungu alitupenda sana ndio maana alimua sisi tuwe  miongoni mwa familia yake Wagalatia 4:6-7 Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba.  Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu. Kwa msingi huu  Mungu aliamua kutupa sisi kila kitu kwa vile sisi ni sehemu ya familia yake;

Tafakari yetu inaendelea kutufundisha tukisoma katika maandiko ya matakatifu kuwa Mungu anasema kuwa anatutaka sisi tuwajali mayatima Yakobo 1:27 Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa. Kuwajali mayatima ni jukumu letu kuwasaidia na kuwasemea wale pale ambapo wanakuwa hawana sauti kutokana na mazingira yanayowazunguka au sauti yao haina nguvu mbele ya jamii yaani haisikiki au inadhararuiwa; kama vile Mungu anavyowajali mayatima katika njia ya ajabu sana na kwa njia na uwezo huo huo anataka sisi tuwajali na kuwasaidia. Tukiamini katika Yesu anautembea katika Imani hii ya Baba ya kuwapenda kwa moyo wetu wote; Matayo 22:37-40 Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.  Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.  Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.  Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii. 

Tafakari yetu leo inalenga kuangalia wajibu wetu wa kuwasaidia wajane na yatima; katika uumbaji mungu aliwaumba wanawake kama kiumbe muhimu cha matunzo. wanawake wameumbwa ili wapate ulinzi na matunzo mazuri. na Mungu alipowaumba alijua kuwa wanawake ni viumbe dhaifu hivyo wanahitaji ulinzi mzuri. wanaume kama viumbe vyeje nguvu ndio mlinzi wa wanawake. ni jukumu la mwanaume kumlinda,malezi, matunzo na kuwapa mwelekeo ulio bora. tukisoma zaburi ya 68: 5 Baba wa yatima na mwamuzi wa wajane, Mungu katika kao lake takatifu. Tukiangalia agano la kale Mungu alikuwa akiwaakiwalinda na kuwapa faraja wajane  na aliagiza kuwa tunatakiwa kuwapa upendo wa khali ya juu sana; Kumbukumbu ya Torati 27:19 Na alaaniwe apotoaye hukumu ya mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe. Na watu wote waseme, Amina. kwamba utalaaniwa wewe ambaye humtendei haki mjane. Isaya 1:17-18  jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane.  Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa wakati wa Agano  tukisoma kitabu cha Kutoka 22:23-24  Usimtese mjane ye yote aliyefiwa na mumewe, wala mtoto yatima.  Ukiwatesa watu hao katika neno lo lote, nao wakanililia mimi, hakika yangu nitasikia kilio chao,  na hasira yangu itawaka moto, nami nitawaua ninyi kwa upanga; na wake wenu watakuwa wajane, na watoto wenu mayatima.  Mwenyezi Mungu hapa amesema wazi kuwa yeye mwenyewe atasikia kilio chao  na atakuja kutoa msaada; kweli kuwa wajane wengi walikuwa ni masikini watu ambao hawana hata uwezo wa kujikizi mahitaji yao wao wenyewe kwa vile walikuwa hawana njia mbadala ya kujisaidia. na mara nyingi pamoja na ujane wao na umasikini ambao mara nyingi huwazunguka; mara nyingi ndio wanakuwa watu ambao wanakuwa mstaria wa mbele  wa kujitolea na kutoa kila ambacho wananacho kwa Mungu.tukisoma 2Timoteo 3:1-3 Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.  Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi,  wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema; fundisho letu hapa katika tafakari yetu ni kuwa; wakati wetu watu hujipenda Zaidi wao wenyewe.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa mazingira ambayo tunayo ya kiroho yameondoa kabisa upendo miongoni mwetu na hasa upendo wa kuwasaidia wajane. Watu  wamekosa upendo, na hakuna hamasa ya kuwasaidia watu wengine; watoto yatima nao wamepata kibali cha Mungu kuwa chini ya ulinzi na uangalizi wa wazazi wao na pale inapotokea kuwa mtoto amepoteza wazazi wake hivyo kinachotokea mtoto au watoto wanakuwa chini ya ulinzi wa Mungu kupitia binadamu ambao wanawajali Yatima. Tukiangalia  idadi ya wajane na Yatima imeendelea kuwa kubwa kwa sababu za vita, matatizo yatokanayo na mama uoto ( mother Nature) kama mafuriko, vimbunga, mafuriko, njaa na kadhalika;Mhubiri 3:19 Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama; jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili. 

Tukisoma Ayubu 29:12-13 Kwa sababu nalimwokoa maskini aliyenililia; Yatima naye, na yule asiyekuwa na mtu wa kumsaidia.  Baraka yake yeye aliyekuwa karibu na kupotea ilinijia; Nikaufanya moyo wa mjane kuimba kwa furaha.  tukumbuke kuwa tunapowasaidia wajane na mayatima tunawapunuzia hisia za upweke na kukosa ulinzi: Tunatakiwa kupigania haki zao; tunatakiwa kuwalisha na kuwavika   na tunatakiwa kuwakinga kutoka kwa watu ambao huwatenda vibaya; tunatakiwa kugawana tulicho nacho; Tunatakiwa tuwe macho kwa wasioona na tuwe na miguu kwa walemavu; je wewe uko tayari kuwa ni baba wa masikini?  Tafakari yetu inasisitiza kuwa tunatakiwa kusikiliza Mayatima  wanatakiwa kulindwa  hasa pale wanapopoteza ulinzi wao wa kininadamu; Tukumbuke maneno ya Mungu kuwa ameweka Baraka ya matunzo ya katika ngazi ile ile kama ya kutoa fungu la kumi tukiweza kuwatunza na kuwapa mayatima tukumbuke kuwa tunatoa moja kwa moja kwa Mungu naye atatulipa katika uzito ule ule.

Hii ndio tafakri yetu ya leo Amina

Emmanuel Turuka


Monday, August 15, 2016

UNAJUA KUWA BINADAMU ANA PEA MBILI ZA MACHO?

AUGUST 15



Luka 11:27-36

Tafakari yetu ya leo tunaangalia fundisho la yesu katika uwezo wetu wa kuona na kutambua maono; Yesu daima alikuwa akizungumzia mafundisho ya aina yake, hasa pale alipotaka sisi tutambue maono ya kiroho juu ya uwezo wa macho; Yesu alikuwa hazungumzii macho yetu haya ya kibinadamu au upofu wa kibinadamu bali alikuwa akizungumzia macho ya kiroho; tunatambua kuwa tukiwa na macho mazuri tunafurahia uzuri wa juu na mwanga tunaweza kuona vitu vingi vizuri na kufanya uchaguzi; na kama tutakuwa na macho mabovu hatuwezi kufaidi vitu hivi vyote; neno kubwa hapa mwanga ni kiashiria cha ukuu wa mungu katikqa maisha yetu kupitia Yesu mwenyewe; yeye alishawahi tufundisha kuwa yeye ni mwanga; Yohana 1:4-5; Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.  Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.  Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.  Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.  Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.  ni ukweli ambao haufichiki kuwa mwanga ni asili ya kila kitu; mwanga ni zao la maarifa, neema na ukweli yeye aliuwasha mwanga kwa wokovu wetu na kwa ushiriki wa roho mtakatifu;

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa ni jukumu letukupitia mwanga wa kweli kuwa wapole, wanyenyekevu, kuwa na Imani na kuendlea kutumia vipaji vyetu vizuri; 2 Petro 1:5-9 Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.  Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa,  na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa,  na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo.  Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo.  Maana yeye asiyekuwa na hayo ni kipofu, hawezi kuona vitu vilivyo mbali, amesahau kule kutakaswa dhambi zake za zamani.   

Tafakari yetu inatutaka kujiepusha tusije angukia kwenye giza la kiroho hivyo upofu hautakiwi uwe sehemu ya maisha yetu ya kiroho; tunatatikwa kutumia mwanga wa ndani na wan je kama faida ya maisha yetu ya baadae; Yohana 1:9 mwanga wa kiroho kurunzi lake kubwa ni bibilia; tujikumbushe kuwa mwanga wa mwili ni macho ambaya yanauwezo wa kuona na kuhakiki: tukumbuke kuwa mtu bila jicho ni sawa na mtu bila mwanga; mwanga wa mwili ni jicho; zaburi ya 14:1 Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema.

Tafakari yetu yatupasa pia kujua thamani ya macho ya kiroho ni mwanga ambao unaletwa na Yesu kristo kupitia mafundisho yake kuwa yeye ni mwanga na uzima hakuna ambaye anaweza kwenda kwa baba bila yeye;  kwa mwanga wa kiroho tunabarikiwa kuona kila kitu katika utukufu wa Mungu.  Tukisoma waefeso 1:18 macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo; 

Tafakari nyingine ni jicho la maelewano jicho hili kazi yake iko kwenye akili mawasiliano ndio kielelezo cha juu kabisa katika kuutafakari mwanga na kuuishi; lakini Yesu anatuagiza kuwa tunatumia macho yetu katika maono ya kiroho,tunatakiwa kutambua kuwa yatupasa kuwa wakweli,waaminifu, ambao akili zetu haziharibika; angalia mfano wa mpanzi: jinsi inavyokuwa rahisi kwetu kuangamia au kurudi katika giza; na moja ya sababu tunapenda sana vitu vya kidunia; Mathayo 13:15 Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya. 

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa  mara nyingi tuko tayari kuona kile ambacho tunataka kuona; na kile ambacho hatutaki kukiona hata kama ni kizuri na hatutakiona; kile mtu ambacho hataki kukisoma hatakisoma hata kama titakuwa rahisi namna gani; ndipo hapo tunapobadilisha macho yetu na katika mwenekano wa ajabu kabisa; mwanga unafunikwa macho yakuwa na ugonjwa roho zetu hujazwa na maumivu ya kujikataa; ni wakati ambao ukweli hukataliwa; uwongo utawala maisha , dhambi pia utawala maisha; kiburi huwa ndio mwanga wao;  1 Yohana 1:6-7 Tukisema ya kwamba twashirikiana naye, tena tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli; bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote. 

Hii ndio tafakari yetu ya leo: Amina

Emmanuel Turuka


Sunday, August 14, 2016

UTUMISHI ULIOTUKUKA MBELE YA MUNGU

 AUGUST 14

 ZAWADI AMBAYO KILA MTU ANAHITAJI KATIKA MAISHA;


2 Timothy 3:1–5

Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa kila mtu anahitaji zawadi iliyo bora kabisa katika maisha yake; ni kila mtu anahitaji zawadi kubwa ya maisha ambayo ni upendo; ukiwa na upendo kwa kweli familia zetu au jumuia zetu zitakuwaje? Je myumba zetu zitakuwaje? Je ofisi zetu zitakuwaje? Je shule zetu zitakuwaje? Natumaini kama tutakuwa katika maisha ya upendo hakika tutakuwa katika ni kisima cha ajabu chenye upendo mkubwa Galatians 6:10 . Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio  Itakuwa ni rahisi kujiuliza swali hili je leo nani atakuwa mbarikiwa kwani daima akili yetu itakuwa ikiangalia upande mzuri wa maisha yetu na sio upande mbaya: 2 Timothy 3:1–5 Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.  Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio  safi,  wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,  wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu;   wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.


Tafakari yetu inatuonya kuwa Kunyume cha upendo ni uangamizi kwani kila mtu atakuwa kweney harakati; na akiyatizama maisha yake pekee yake watakuwa wakijisifu katika mafanikio ambayo hayajali maisha ya watu wengine. Daima tunajisahau na kujiona kuwa wafalme katika mafanikio yetu; na kwa msingi huo tunakuwa hatuna muda wa kuonyesha upendo kwa wengine; lakini tukumbuke kuwa kamwe hatujeumbwa kuishi kwa ukabaila na uchoyo; ni wajibu wetu kufanya jambo lolote amablo litaonekana tofauti kwa wengine. Siri ya Mungu kwetu ni hii kamwe hatutakuwa tumeishi maisha ya kumpendeza Mungu kama hutafanya jambo njema kwa wenzetu bila kujihatijika wao kurudisha fadhila. Je umeshaona jinsi marafiki wanavyoishi kwa kuumizana? Ukiwa bizi sana huwezi kuliona hili mpaka pale utakapo tuo ushirikiano na kujifunza kwa watu wengine kwa kuona shida zao; Mathayo 25:40  Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi. Methali 19:17 Amhurumiaye maskini humkopesha Bwana; Naye atamlipa kwa tendo lake jema.

Tafakaria yetu ina tuuliza kuwa; Je wewe umefanya tofauti gani leo? Kwa mjane? Kwa mototo yatima; kwa mzee au masikini ambaye anahitaji huruma ya Mungu kupitia kwako? Tunapofanya wema kwa wenzetu tunawajengea taswira ya ajabu katika mioyo yao na wanamwona Mungu katika maisha yao kupitia kwetu: je uko tayari kuwa sehemu ya utukufu wa Mungu kwa kuwasaidia wahitaji wa kweli leo? Kama mtoto mmoja alivyomuuliza Mama mmoja ambaye alimnunulia pea tatu za viatu ambavyo alikuwa akivitamani sana kuwa je wewe ni Mke wa Mungu? Katika taswira yake anajua wema unatoka kwa Mung tu? Je wewe uko tayari kufanya wema ili utukufu wa Mungu ungae katika maisha yako? Kutoa kwa moyo ni hadhina pekee unayojijegea mbele ya Mungu. Yatupasa kujifunza kuwa watu wa kutoa na kuwa mwema katika maisha ya watu wengine; Yatupasa kuonyesha maisha yetu mema kila wakati na kila mahali tunapokwenda;

Tafkari yetu leo inaendelea kusisitiza kuwa Upendo lazima uonekane katika maisha yetu kwa vitendo;  kupitia muda wako, uwezo wako wa kifedha hata kwa maneno mazuri ya kuhamasisha kwa kufanaya hivyo tunamkaribisha Mungu katika maisha yetu ya kila siku; wakati mwingine tunakatishwa tamaa pale ambapo unatoa msaada wa wenzetu lakini wahusika wakisha pata msaada yaani wanakuwa hawana muda wa kusema asante, la msingi uelewe kuwa mungu daima anaweka kumbukumbu katika kila jambo njema ambalo tunalifanya hivyo hatunasababu ya kusubiri asante ya kibinadamu waajibu wetu yatupas kushukuru kwani Mungu yeye ndiye atakaye kurudishia wewe mara elfu elfu kwa wema wako. Jicho la mungu ni la ajabu linaona kila kitu tufanyacho. Mbegu iliyo bora hupandwa kwenye udongo mzuri na udongo mzuri hutoka kwa mungu. Sikila shida za watu nawe uwe utabarikiwa kwa msaada wako kwao kwani wao hawana uwezo mwenyezi  Mungu atakubariki kwa upendo wako;

Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa pendo la kweli lazima lionyeshwe kwa matendo yetu, tukumbuka kuwa watu wanatuangalia sisi, tukumbuke kuwa kadiri tunavyowasaidia wengine ndivyo hivyo Mungu atakavyo turudishia na kutusaidia kwa kadiri ya mahitaji yetu; Mungu  atakuzidisha mara elfu elfu lakini lazima utambulike  kwa matunda ambayo umeyapanda na yameleta furaha na amani kwa wengine; Mathayo 7:16–20. Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?  Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya.  Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.  Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni.  Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua. 

Tafakari yetu inasisitiza kuwa  ili kuweza kutekeleza utumishi ulio tukuka lazima atimize wajibu wake wa kujijenmgea msingi ulio bora Mathayo 7: 24-27 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na uyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;  mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba.  Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;  mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa. 

Hii ndio tafakari yetu ya leo Amina


Emmanuel Turuka

Friday, July 22, 2016

JE YATUPASA KULIPIZA KISASI DHIDI YA WENZETU KATIKA MAISHA YETU;


July 22

Warumi 3:10

Tafakari ya leo Kwa hakika mwanandamu anahitaji upeo mkubwa wa nuru ya kiroho ambayo itaweza kumfanya azike tamaa zake na hisia zote za kulipiza kisasi; tunatakiwa kuwa na uwezo wa kujizuia na hasira, kuzikandamiza hasira, chuki kwa moyo mpana na kujenga daraja la msamaha.  Kusamehe mtu ambaye amekukosea, kuwapenda ndugu na jamaa ambao wameukata uhusiano pamoja nawe, na kuwa mkarimu kwa yule ambaye aliwahi kukunyima, kukutukana, kukusababishia hasira,kukudharau, kukudhalilisha na kadhalika sio jambo rahisi. Tumewaona hata watumishi wa Mungu ambao wanaielewa sana bibilia wakishindwa kabisa kuktekeleza kanuni hii.

Tafakari yetu inatukumbusha umuhimu wa kumsamehe yule aliyekutendea yasiyo sahihi hutusaidia kutupatanisha na Muumba wetu; vile vile msamaha hudumisha mshikamano wa udugu ambao umeharibiwa. Kwa kusamehe tunaandaa njia ya kumwendea Mungu; Lakini  pasipo  imani  haiwezekani  (Waebrania 11:6). Inatufundisha kuwa mtu  amwendeaye Mungu  lazima  aamini  kwamba  yeye  yuko,  na  kwamba  huwapa  thawabu wale wamtafutao,”. Msamaha hutujengea wa kumwendea na Kuishi na Mungu katika Imani.

Kama ilivyoandikwa hakuna mwenye haki, hata mmoja” (Warumi 3:10). Mungu yuko tayari na anasubiri kumsamehe mtu anaye omba msamaha imeelezwa katika Zaburi 86:5 "Kama wewe Bwana u mwema, umekuwa tayari kusamehe, na mwingi wa fadhili kwa watu wote wakuitao". Daudi aliweka wapi tumaini lake la msamaha? Tukisoma Zaburi 51:1 "Ee Mungu unirehemu sawasawa na fadhili zako kiasi cha wingi wa rehema zako uyafute makosa yangu. Mathayo 6:14-15 Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao na Baba wenu wa mbinguni atawasamehe ninyi bali msipowasamehe watu makosa yao wala Baba yenu hatawasamehe makosa yenu." Wale wamesamehewa husamehe. imeandikwa Waefeso 4:32 "Tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma ninyi mkasameheane kama na Mungu katika kristo alivyowasamehe ninyi."

Tafakari inasisitiza neno kusamehe kwa kweli hakuhesabu makosa. imeandikwa Mathayo 18:21-22 "Kisha petero akamwendea akamwambia Bwana ndugu yangu anikose mara ngapi nami ni msamehe? hata mara saba? Yesu akamwambia sikwambii mara saba bali hata saba mara sabini." Katika kusamehe Yesu ametukomboa kutoka kwa dhambi na mshahara wa dhambi. Wakolosai 2:13-14 inatueleza kuwa "Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu aliwafanya hai pamoja naye akisha kutusamehe makosa yote akisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake iliyo kuwa na uwadui kwetu akiondoa isiwepo tena akaigongomea msalabani."
Zaburi 51:7-12 "Unisamehe nami nitakuwa safi, unioshe nami nitakuwa mweupe kuliko dheluji unifanye kusikia furaha na shangwe, mifupa ilio ponda ifurahi. usitiri uso wako usitazame dhambi zangu uzifute hatia zangu zote Ee Mungu uniumbie moyo safi uifanye upya roho iliyo tulia ndani yangu usinitenge na uso wako wala roho wako mtakatifu usiniondolee unirudishie furaha ya wakovu wako unitegemeze kwa roho ya wepesi."
Zaburi 32:1-6 "Heri aliyesamehewa dhambi na kusitiriwa makosa yake heri Bwana asiyemhesabia upotovu, ambaye rohoni mwake hamna hila niliponyamaza mifupa yangu ilichakaa kwa kuugua kwangu mchana kutwa na kwa maana mchana na usiku mkono wako ulinilemea jasho langu likakauka hata nikawa kama nchi kavu wakati wa kaskazi nalikujulisha dhambi yangu wala sikuuficha upotovu wangu nalisema nitayari maasi yangu kwa Bwana naweukanisamehe uoptovu wa dhambi yangu kwa hiyo kila mtu mtauwa akuombe wakati unapopatikana hakika maji makuu yafurikapo hayatamfikia yeye."
Tafakari yetu inaonyesha umuhimu wa kuwa mnyonge wa moyo wako mbele ya Mungu na wala kutambua hatia yangu, haijafika hali ya kwanza ya kukubalika. Tunahitaji kuokolewa kutoka katika aina zote za tabia zetu mbaya pamoja na misukumo ya ndani inayotushurutisha kufanya mambo fulani mabaya: kama vile, kusema uongo, hasira inayomfanya mtu atukane watu, tamaa mbaya za mwili, uchungu, kutaja machache tu.
Hatuwezi kujiokoa wenyewe kutoka katika dhambi au kuigeuza tabia yetu kwa kujitegemea wenyewe kama vile Simba asivyoweza kuamua awe mwana-kondoo (Warumi 7:18). Dhambi ina nguvu nyingi kuliko nia yetu ya kufanya yale tuyatakayo. Lakini Kristo anaweza kukufanya wewe uwe "imara kwa uweza wake, kwa kazi ya Roho wake katika utu [wako] wa ndani" (Waefeso 3:16). Anafanya kazi yake ili kuondoa tabia zetu ziletazo uharibifu na mahali pake kuweka tabia hizi nzuri: upendo, amani, furaha, upole, uwezo wa kujitawala (Wagalatia 5:22,23). Kristo anaishi maisha yake kupitia ndani yetu, kisha tunapokea uponyaji wa kiroho, tunarejeshwa katika maisha mapya, na kuwezeshwa kuishi maisha hayo mapya.
Ni jambo la muhimu sana kujua kuwa hakuna dhambi ambayo ni ya kutisha sana asiyoweza kuisameka Yesu anatamani sana kwamba kila mmoja wetu hatimayeawe na uhusiano mzuri na Yule aliyemkosea na kumsababishia majeraha ambayo yamejenga chuki ambayo inahitaji msamaha. Yesu anataka tupokea msamaha na utakaso wa Mungu ni; katika  imani jambo ni  rahisi na la maana sana kama tunavyofurahia kumpokea motto mdogo aliyezaliwa na kumkumbatia. Lakini kutokana na ubinadamu wetu, majivuno, kiburi, masengenyo inatuwia vigumu sana kutoa msamaha wa kweli pale tunapokosewa, tunakuwa na kiburi ambacho kinatufanya kuona kuwa Yule aliyetukosea hastaili msamaha wetu; lakini kama tunayafuata mafundisho ya yesu na mifano ambayo ametutolea katika Bibilia Takatitifu tunatakiwa tuondoe ugumu katika mioyo yetu na kuuvaa unyenyekevu kama yeye alivyovaa unyenyekevu na kuuvua Umungu kwa ajili ya makosa yetu, na alikuja kukaa nasi na ametutengenezea daraja la msamaha ambalo kila mwanadamu lazima alipite ili kuweza kukamilisha safari yake ya kwenda mbingu.
Hii ndio tafakari yetu ya leo hebu jitafakari kwa nini umekuwa na kiburi cha kushindwa kabisa kumsamehe, jirani yako, ndugu yako ambao wamekukosea kutokana na ubinadamu wao, usijali amekukosea mara ngapi angalia je wewe uko tayari kumsamehe wakati wowote ule na mara ngapi?- amina
Emmanuel Turuka