WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Monday, August 15, 2016

UNAJUA KUWA BINADAMU ANA PEA MBILI ZA MACHO?

AUGUST 15



Luka 11:27-36

Tafakari yetu ya leo tunaangalia fundisho la yesu katika uwezo wetu wa kuona na kutambua maono; Yesu daima alikuwa akizungumzia mafundisho ya aina yake, hasa pale alipotaka sisi tutambue maono ya kiroho juu ya uwezo wa macho; Yesu alikuwa hazungumzii macho yetu haya ya kibinadamu au upofu wa kibinadamu bali alikuwa akizungumzia macho ya kiroho; tunatambua kuwa tukiwa na macho mazuri tunafurahia uzuri wa juu na mwanga tunaweza kuona vitu vingi vizuri na kufanya uchaguzi; na kama tutakuwa na macho mabovu hatuwezi kufaidi vitu hivi vyote; neno kubwa hapa mwanga ni kiashiria cha ukuu wa mungu katikqa maisha yetu kupitia Yesu mwenyewe; yeye alishawahi tufundisha kuwa yeye ni mwanga; Yohana 1:4-5; Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.  Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.  Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.  Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.  Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.  ni ukweli ambao haufichiki kuwa mwanga ni asili ya kila kitu; mwanga ni zao la maarifa, neema na ukweli yeye aliuwasha mwanga kwa wokovu wetu na kwa ushiriki wa roho mtakatifu;

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa ni jukumu letukupitia mwanga wa kweli kuwa wapole, wanyenyekevu, kuwa na Imani na kuendlea kutumia vipaji vyetu vizuri; 2 Petro 1:5-9 Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.  Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa,  na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa,  na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo.  Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo.  Maana yeye asiyekuwa na hayo ni kipofu, hawezi kuona vitu vilivyo mbali, amesahau kule kutakaswa dhambi zake za zamani.   

Tafakari yetu inatutaka kujiepusha tusije angukia kwenye giza la kiroho hivyo upofu hautakiwi uwe sehemu ya maisha yetu ya kiroho; tunatatikwa kutumia mwanga wa ndani na wan je kama faida ya maisha yetu ya baadae; Yohana 1:9 mwanga wa kiroho kurunzi lake kubwa ni bibilia; tujikumbushe kuwa mwanga wa mwili ni macho ambaya yanauwezo wa kuona na kuhakiki: tukumbuke kuwa mtu bila jicho ni sawa na mtu bila mwanga; mwanga wa mwili ni jicho; zaburi ya 14:1 Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema.

Tafakari yetu yatupasa pia kujua thamani ya macho ya kiroho ni mwanga ambao unaletwa na Yesu kristo kupitia mafundisho yake kuwa yeye ni mwanga na uzima hakuna ambaye anaweza kwenda kwa baba bila yeye;  kwa mwanga wa kiroho tunabarikiwa kuona kila kitu katika utukufu wa Mungu.  Tukisoma waefeso 1:18 macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo; 

Tafakari nyingine ni jicho la maelewano jicho hili kazi yake iko kwenye akili mawasiliano ndio kielelezo cha juu kabisa katika kuutafakari mwanga na kuuishi; lakini Yesu anatuagiza kuwa tunatumia macho yetu katika maono ya kiroho,tunatakiwa kutambua kuwa yatupasa kuwa wakweli,waaminifu, ambao akili zetu haziharibika; angalia mfano wa mpanzi: jinsi inavyokuwa rahisi kwetu kuangamia au kurudi katika giza; na moja ya sababu tunapenda sana vitu vya kidunia; Mathayo 13:15 Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya. 

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa  mara nyingi tuko tayari kuona kile ambacho tunataka kuona; na kile ambacho hatutaki kukiona hata kama ni kizuri na hatutakiona; kile mtu ambacho hataki kukisoma hatakisoma hata kama titakuwa rahisi namna gani; ndipo hapo tunapobadilisha macho yetu na katika mwenekano wa ajabu kabisa; mwanga unafunikwa macho yakuwa na ugonjwa roho zetu hujazwa na maumivu ya kujikataa; ni wakati ambao ukweli hukataliwa; uwongo utawala maisha , dhambi pia utawala maisha; kiburi huwa ndio mwanga wao;  1 Yohana 1:6-7 Tukisema ya kwamba twashirikiana naye, tena tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli; bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote. 

Hii ndio tafakari yetu ya leo: Amina

Emmanuel Turuka


No comments:

Post a Comment