WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Wednesday, August 17, 2016

MUNGU PEKEE NDIYE ANAYETOA ADHABU NA ZAWADI YA MATENDO YETU:

AUGUST 4


Isaya 55:7-9

August 17

Tafakari yetu ya leo inatukumbusha umuhimu wa zawadi na adhabu; katika maisha yetu ya kila siku tumekuwa watu wa kupenda sana kupokea au kupewa kile ambacho ni kizuri hata kama hatustahili zawadi hiyo; ustahili wa kupokea zawadi stahilivu ni pale matendo yetu yanaonekana wazi kabisa tunatenda haki bila shuruti; tukumbuke kuwa daima Mungu kupitia kwa Bwana wetu Yesu Kristo yeye ndio mwenye usukani nay eye ndiye yeye; Mungu hapendi kutuadhibu sisi anapenda daiama kutupa sisi kile kilicho kizuri na bora kwa ustawi wa maisha yetu hapa duniani na baadae mbinguni; Zaburi 89:14 inatukumbusha kuwa Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako, Fadhili na kweli zahudhuria mbele za uso wako. Daima hukumu ya Mungu imejaa haki tupu;

Tukisoma kitabu cha Isaya 55:7-9 kinatukumbusha kuwa Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie Bwana, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa.  Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana.  Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. Kwa kuzingatia haki ya kweli ya Mungu siku ya hukumu  kutakuwa mgawanyiko wa makundi kulingana na matendo yao lile kundi la wenye haki wataungana na Mwenyezi Mungu katika utukufu wake na lile kundi la watenda maovu watatupwa kwenye moto wa milele jahanamu na watapata adhamu ya milele; kwa huruma na ukuu wa Mungu bado sisi leo hii tunanafasi nzuri ya kuungama dhambi zetu ili tusipate hiyo adhabu ya milele;

Tafakari yetu inatuuliza kama Bwana wetu Yesu kristo alivyowauliza makutano nani ni mtumishi mwaminifu? Yule ambaye katika fikra zake hana kusitasita katika matendo yake mema na yuko taayri kumtumikia Mungu kwa Moyo wake wote; au kundi ambalo haliko tayari kumtumikia Mungu wakijua kuwa bado wana muda wa kutosha hivyo ngoja waendelee kufurahia maisha ya hapa duniani na Mungu watamtumikia baadae wakisha tosheka na maisha ya Duniani? Tukumbuke kuwa Mungu ndio kila kitu utukufu na utawala wote uko juu yake na yeyey ndiye mtawala wa kila kitu. Yeye hutupa zawadi na kutupa sisi adhabu. Je tunakumbuka hadithi ya Mwanan mpotevu; tukisoma 2 Petro 3:9 Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba. Jambo la msingi nikuomba ili kuweza kufanya toba ya kweli.

Tafakari  yetu inatukumbusha kuwa kazi zetu tu hazitusaidii sisi kupata sifa ya kuridhi mzima wa Mungu, bali kazi zetu na utiii ni ishara tosha ya kumwonyesha Mungu kuwa tumepokee neema yake; lakini kama tukiendeleza kiburi na kuto kutii hivyo hiyo ni ishara tosha kuwa hatuko tayari kupokea neema zake; jukumu letu sisi leo tunatakiwa kufanya kila kitu katika uwezo wetu kumpenda na kumtumikia Mungu na kutimiza amri zake kwa msingi kwamba tukitekeleza hili hatutakosa zawadi ya kushiriki utukufu wake mbinguni.

Hii ndio tafakari yetu ya leo Amina


Emmanuel Turuka

No comments:

Post a Comment