WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Tuesday, August 16, 2016

WAPENDENI WAJANE NA MAYATIMA;

AUGUST 16


Isaya 1:17-18

Tafakari ya leo inatukumbusha umuhimu wa kuwapenda na kuwahudumia wajane na yatima; tujikumbushe nini maana ya kuwa yatima na mjane; katika maana ya kawaida kuwa yatima ni hali ya kukosa wazazi na kuwa mjane ni hali ya kukosa mwenza katika ndoa.  Tafsiri nyingine ya kuwa yatima au mjane tunaiongelea pale tunavpoongelea kuhusu maisha yetu ya kiroho tukiamini kuwa kila mtu amewahi kuwa yatima au mjane kiroho. Kwa tafsiri hii sote tulikuwa yatima wa kiroho mpaka pale tulipo chukuliwa na Mungu waefeso 1:5 Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake. Tukumbuke kuwa  Mungu alitupenda sana ndio maana alimua sisi tuwe  miongoni mwa familia yake Wagalatia 4:6-7 Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba.  Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu. Kwa msingi huu  Mungu aliamua kutupa sisi kila kitu kwa vile sisi ni sehemu ya familia yake;

Tafakari yetu inaendelea kutufundisha tukisoma katika maandiko ya matakatifu kuwa Mungu anasema kuwa anatutaka sisi tuwajali mayatima Yakobo 1:27 Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa. Kuwajali mayatima ni jukumu letu kuwasaidia na kuwasemea wale pale ambapo wanakuwa hawana sauti kutokana na mazingira yanayowazunguka au sauti yao haina nguvu mbele ya jamii yaani haisikiki au inadhararuiwa; kama vile Mungu anavyowajali mayatima katika njia ya ajabu sana na kwa njia na uwezo huo huo anataka sisi tuwajali na kuwasaidia. Tukiamini katika Yesu anautembea katika Imani hii ya Baba ya kuwapenda kwa moyo wetu wote; Matayo 22:37-40 Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.  Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.  Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.  Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii. 

Tafakari yetu leo inalenga kuangalia wajibu wetu wa kuwasaidia wajane na yatima; katika uumbaji mungu aliwaumba wanawake kama kiumbe muhimu cha matunzo. wanawake wameumbwa ili wapate ulinzi na matunzo mazuri. na Mungu alipowaumba alijua kuwa wanawake ni viumbe dhaifu hivyo wanahitaji ulinzi mzuri. wanaume kama viumbe vyeje nguvu ndio mlinzi wa wanawake. ni jukumu la mwanaume kumlinda,malezi, matunzo na kuwapa mwelekeo ulio bora. tukisoma zaburi ya 68: 5 Baba wa yatima na mwamuzi wa wajane, Mungu katika kao lake takatifu. Tukiangalia agano la kale Mungu alikuwa akiwaakiwalinda na kuwapa faraja wajane  na aliagiza kuwa tunatakiwa kuwapa upendo wa khali ya juu sana; Kumbukumbu ya Torati 27:19 Na alaaniwe apotoaye hukumu ya mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe. Na watu wote waseme, Amina. kwamba utalaaniwa wewe ambaye humtendei haki mjane. Isaya 1:17-18  jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane.  Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa wakati wa Agano  tukisoma kitabu cha Kutoka 22:23-24  Usimtese mjane ye yote aliyefiwa na mumewe, wala mtoto yatima.  Ukiwatesa watu hao katika neno lo lote, nao wakanililia mimi, hakika yangu nitasikia kilio chao,  na hasira yangu itawaka moto, nami nitawaua ninyi kwa upanga; na wake wenu watakuwa wajane, na watoto wenu mayatima.  Mwenyezi Mungu hapa amesema wazi kuwa yeye mwenyewe atasikia kilio chao  na atakuja kutoa msaada; kweli kuwa wajane wengi walikuwa ni masikini watu ambao hawana hata uwezo wa kujikizi mahitaji yao wao wenyewe kwa vile walikuwa hawana njia mbadala ya kujisaidia. na mara nyingi pamoja na ujane wao na umasikini ambao mara nyingi huwazunguka; mara nyingi ndio wanakuwa watu ambao wanakuwa mstaria wa mbele  wa kujitolea na kutoa kila ambacho wananacho kwa Mungu.tukisoma 2Timoteo 3:1-3 Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.  Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi,  wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema; fundisho letu hapa katika tafakari yetu ni kuwa; wakati wetu watu hujipenda Zaidi wao wenyewe.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa mazingira ambayo tunayo ya kiroho yameondoa kabisa upendo miongoni mwetu na hasa upendo wa kuwasaidia wajane. Watu  wamekosa upendo, na hakuna hamasa ya kuwasaidia watu wengine; watoto yatima nao wamepata kibali cha Mungu kuwa chini ya ulinzi na uangalizi wa wazazi wao na pale inapotokea kuwa mtoto amepoteza wazazi wake hivyo kinachotokea mtoto au watoto wanakuwa chini ya ulinzi wa Mungu kupitia binadamu ambao wanawajali Yatima. Tukiangalia  idadi ya wajane na Yatima imeendelea kuwa kubwa kwa sababu za vita, matatizo yatokanayo na mama uoto ( mother Nature) kama mafuriko, vimbunga, mafuriko, njaa na kadhalika;Mhubiri 3:19 Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama; jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili. 

Tukisoma Ayubu 29:12-13 Kwa sababu nalimwokoa maskini aliyenililia; Yatima naye, na yule asiyekuwa na mtu wa kumsaidia.  Baraka yake yeye aliyekuwa karibu na kupotea ilinijia; Nikaufanya moyo wa mjane kuimba kwa furaha.  tukumbuke kuwa tunapowasaidia wajane na mayatima tunawapunuzia hisia za upweke na kukosa ulinzi: Tunatakiwa kupigania haki zao; tunatakiwa kuwalisha na kuwavika   na tunatakiwa kuwakinga kutoka kwa watu ambao huwatenda vibaya; tunatakiwa kugawana tulicho nacho; Tunatakiwa tuwe macho kwa wasioona na tuwe na miguu kwa walemavu; je wewe uko tayari kuwa ni baba wa masikini?  Tafakari yetu inasisitiza kuwa tunatakiwa kusikiliza Mayatima  wanatakiwa kulindwa  hasa pale wanapopoteza ulinzi wao wa kininadamu; Tukumbuke maneno ya Mungu kuwa ameweka Baraka ya matunzo ya katika ngazi ile ile kama ya kutoa fungu la kumi tukiweza kuwatunza na kuwapa mayatima tukumbuke kuwa tunatoa moja kwa moja kwa Mungu naye atatulipa katika uzito ule ule.

Hii ndio tafakri yetu ya leo Amina

Emmanuel Turuka


No comments:

Post a Comment