WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Monday, November 7, 2016

JE UNATAMBUA KUWA MLANGO ULIOFUNGWA NI BARAKA?


NOVEMBER

Tafakari yetu leo tujikumbushe ujumbe huu mzuri kuwa kama una imani mlango wa matumaini utafunguliwa dhidi yako; tunajua kuwa maisha yetu hayajejengwa katika mstari ulionyoka ambao sisi tunatembea tukiwa huru; bali ni safari ambayo huwa ina vikwazo, vigugumizi, mabonde, milima na mapingamizi  ambayo tuwapo safarini lazima tuwe tayari kukabiliana navyo, na urahisi wa kushinda vikwazo hivi ni kuwa na imani inayotakiwa. Hivyo tukiwa na imani tuwe na uhakika kuwa mlango utafunguliwa;

Tafakari yetu inatufundisha huu ukweli ambao haupingiki kuwa kujifunza tofauti kati ya imani na kuamaini ni kitu ambacho tunatakiwa kukifanya kila siku katika maisha yetu yote; ndio maana mafundisho yanatukumbusha kuwa  Mungu anapenda sisi tumwamini yeye kwa akili zetu na kwa dhamira zetu bila shuruti; na tutaweza kumwamini yeye kwa matendo yetu na katika shida zetu; tukiamini kuwa yeye pekee ndiye kimbilio letu katika mahitaji yetu;
Tafakari inatukumbusha kuwa matumaini na kumwamini mungu lazima yaanzie kwetu kupitia maombi yetu ya kusifu na kushukuru; Tumkumbuke Ayubu pamaoja na shida na magonjwa aliendelea kumtumaini Mungu na Mungu alimbariki; Kama ilivyotokea kwa Ayubu nasi tumaini letu katika mahangaiko yetu ni  imani na matumaini makubwa ambayo tunatakiwa tuyatangulize mbele ya Mungu, kwa kufanya hivyo Mungu hufunga mlango wa mateso na kwa kweli huwa hauana faida na maisha yetu na kukufungulia Mlango mwingine ambao umejaa matumaini; Mungu huonyesha njia kupitia mlango ambao umefungwa na ule ambao anaufungua kwa ajili maisha yetu; Mwenyezi Mungu anapofunga mlango mmoja anataka wewe ubadilisha mwelekeo wako wa maisha; na unavyobadilisha mwenendo wako wa maisha na ili uweze kutembea katika mafanikio na neema ya utukufu wako kupitia mlango mpya alioufungua kwako;

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa tatizo letu mara nyingi tunajikwaa katika barabara yenye makorongo ambayo imetengenezwa kwa lami ambayo imejaa mashaka na kukosa imani; lakini mwenyezi Mungu daima hututembeza katika barabara iliyo imara na bora yenye imani kubwa ambayo hutuongoza sisi katika mlango ambao umejaa matumaini na kutufungulia mlango ambao hatukuutegemea kabisa; mungu wakati mwingine hata hatuambia kuwa tuende kushoto au kulia yeye anachofanya ni kufunga mlango ambao hauna faida kwetu na kutufungulia mlango ambao umejaa neema. Hivyo wakati mwingi mlango ukifungwa ni neema vile vile.


Tafakari tunatakiwa tuendelee kushukuru hata tukiwa kazini tunapopatwa na mitiani mbalimbali  iyojaa fitina, chuki na kadhalika mshukuru Mungu kwani kuna neema kubwa inakuja mbele yako. Tukumbuke kuwa Mungu anayaendesha maisha yetu upendo wake hufunga na kufungua milango ya kuingia na kutoka katika maisha yetu; Tunajua kuwa inakuwa ngumu katika ubinadamu kulikubali na kulishukuru hilo mara moja. Tukumbuke kuwa Daima Mungu anatemebea mbele yetu, anajua mapito yetu kabla sisi hatujeyajua yeye ni kinga yetu ya kweli; ndio maana siku zote tukiwa na imani hutuepusha na mabaya yote mbele yetu; lakini kwa sababu ya kukosa kwetu hekima sisi tunajiona kuwa tunajua na kumsukuma pembeni lakini baada ya kumsukuma na kupata matatizo tunarudi na kuanza kumlilia huku tukimlalamikia sana kwa nini umenifanyia hivi na hivi.

Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa tunapopatwa na tatizo kwa kiwango chochote kila Mungu tayari anakuwa ameshajua tatizo na suluhisho lake; anachohitaji kutoka kwetu ni sisi kumwamini yeye na kutekeleza sehemu yetu ambayo ni maisha kulingana na maagizo yake; na jukumu letu nyingine ni kuendelea kusali na kumshukuru; na tukumbuke kuwa tutafanikiwa kwa kusoma vitabu vyake na kuamini kuwa yeye ndiye suluhisho la matatizo yetu yote:

Hii ndio tafakari yetu ya leo tumtumaini mungu katika njia zake na katika maamuzi yake kwetu ili tuendelee kupokea Baraka zake bila kikomo. Amina

Emmanuel Turuka




No comments:

Post a Comment