WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Tuesday, November 8, 2016

WEWE UNAKUBALI UMEBARIKIWA?


November

1 wakorinto. 12.13

Tafakari ya neno kubalikiwa lina maana pana na sio ile ambayo imezoeleka ya kufurahia mafanikio au raha hasa za kimaisha yetu ya kila siku; na mara nyingi tunafurahi sana tunapofanikiwa katika maisha yetu na hapo kwa sauti ya juu tunaimba na kushukuru kuwa tumebarikiwa; wote tunahitaji kubarikiwa na kufurahaia maisha yetu ya kila siku katika ubora wake wa khali ya juu. Nami  najua kabisa hakuna mtu hata mmoja katika misha yetu ya kila siku ambaye hukataa maisha mazuri ya Baraka.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa mara nyingi tunapoangalia kubarikiwa tatizo letu tunaangalia Baraka katika upande tofauti nap engine kwa namna ya pekee; tukiangalia kuwa Baraka asili yake mafanikio ya asili; kwa msingi huu pale tunapokaa kwenye nyumba nzuri, kazi nzuri,gari nzuri na kadhalika kwetu tunajiona kuwa tumebarikiwa na tunafurahia sana na tunaimba aleluya kwa Mungu ametubariki; warumi 8:17 na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye. 

Tafakari yetu inataka tujiulize je pale inapotokea pengine tunaumwa; au unaendesha gari ambalo sio nzuri au unaishi katika nyumba ambayo sio nzuri; je hapo tumekuwa tumepoteza Baraka za Mungu? Au pale maisha yanapokuwa magumu ha uwezo wa kifedha umeondoka na hatuwezi kuyakabili msiaha kwa ujumla je hapo Baraka za Mungu ziko wapi? Nafikiri kuwa tatizo letu tunaangalia Baraka katika mwelekeo mmoja tu wa mafanikio na sio shida; katika mwelekeo huu wa kuwaza kutumbuke kuwa Gari linaweza toweka siku moja, pesa zinaweza toweka siku moja, hivi vitu vyote ambavyo tunavyoviona katika macho ya kidunia ni njia ya kutusaidia sisi ili tuweze kuzifikia barka za Mungu katika ukamilifu wake; tujue kuwa hivyo vyote ni vya muda tu lakini Baraka na neema za Mungu ni za kudumu. Hata afya yetu siku moja itaporomoka na hatutaweza irudisha tena;  hivyo tunatakiwa kufahamu kuwa Baraka za kweli sio mali ni vyote vinavyotuzunguka bali baraka ya kweli ni roho wa Mungu ndani yetu; Warumi  8:28-31 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza. Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu? 

Tafakari yetu inaendelea kusisitiza kuwa Je ni furaha ya namna gani pale ambapo vyote vimetoweka lakini bado unaendelea kumiliki Baraka za Mungu , hivyo ni wajibu wetu sasa kutambua Baraka za Mungu ndani ya Maisha yetu; halafu kitu ambacho tunatakiwa tujivunie ni utambuzi kuwa tayari Mungu ameshatujalia Baraka katika maisha yetu; katika wakati uliopita ,wakati wa sasa na wakati wa baadae;lakini Mungu ametupa sisi vitu vyote vya kutupatia na kutuongoza kuishi katika Baraka zake, ili tuweze kuwa washindi, ili kutusaidia kuwa watiifu, na kuwa na thamani katika maisha ya Kimungu katika ufalme wake;

Tafakari yetu tukisoma Waefeso  2:12, kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani.  tukumbuke kuwa  tumepata kibali cha baba na tumelelewa  kwa damu ya Yesu; hivyo njia pekee za kufurahia Baraka za Mungu lazima tuuishi wokovu na neema ya Mungu itubariki, hivyo tunatakiwa tuziangalie Baraka zetu kutoka katika mpangilkio na mwelekeo wa Kimungu; hapa tutaweza kutambua kuwa kila kitu ambacho kipo mbele yetu kimebarikiwa kweli kweli; hapo tutatambua kuwa Mwenyezi Mungu ametubariki sisi san asana ambazo hazipimiki hivyo wajibu wetu ni sisi kumshukuru Mungu kwa Baraka hizo hata kama tunakabiliwa na matatizo mengi ya maisha lakini wajibu wetu ni kumshukuru na kumsifu Mungu kwa Baraka zake juu yetu .

Hii ndio tafakari yetu ya leo Amina
Emmanuel Turuka




No comments:

Post a Comment