WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Monday, May 30, 2016

TWATAKIWA KUWA NA NIA YA THABITI;



May 30

Wagalatia 6:9

Tafakari ya leo tunaangalia dhana nzima ya maisha yetu tukijua kuwa Maisha yetu yamezungukwa na mitihani mingi sana. Lakini ili tuweze kukabiliana vizuri na mitihani hiyo ya maisha lazima tujijengee nidhamu ya hali ya juu na nia madhubuti ili tuweze kushinda. Hivyo hivyo katika kuimarisha ukristo wetu; lazima daima tuweke katika akili zetu malengo yetu ni yapi; Tujifunze kusahau yaliyopita; lazima tuondoa katika akili yetu dhan zima ya mambo magumu ambay tunafikiri hayawezekaniki; na kujiondole avipingamizi vinavyokuzunguka wewe mwenyewe ambavyo kwa namna moja au nyingine hukurudisha nyuma; hatutakiwi kufikiria mambo hasi; hatutakiwi kutaka tama na kuishi kwa kunungunika;

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa lazima tuishi katika malengo makuu mawili; kuishi maisha yenye mwelekeo na maisha yaliyojaa shauku; Mwenyezi Mungu siku zote ametupa sisi njia na mbinu za kushinda; lakini wajibu wetu lazima tuwe na nia ya ushindi; nia ambayo haiwezi kukatisha tama na yeyyote Yule; Mwenyezi Mungu kwa kutambua ushindani wa maisha ambao uko mbele yetu alitupa sisi maarifa kwani kwa maarifa sisi tutakuwa huru na kufanya maamuzi sahihi; Ametupa sisi uhuru wa kufanya maamuzi yaliyo sahihi; lakini kwa udumafu wetu hata pale ambapo maji ni mengi lakini bado tunalalamika kuwa tunaona kiu; kwa nini khali kama hii inaweza tokea Jibu ni rahisi tu ni ukosefu wa Maarifa sahihi na kujiamini.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa lazima tuachane na vitu vyote ambavyo vinazuia na kuchelewesha utekelezaji wa mipango endelevu ya kuwa na nia nzuri ya kufanya mazuri katika maisha yetu katika kuufikia uzima wa kweli; Ili tuweze kufanya vizuri tunahitaji kutayarisha akili zetu ili ziweze  kuwa tayari kupokea matokeo ya matendo mazuri. Tukikumbuka kuwa kuweka Nia ni kitu muhimu katika maisha yetu; ni tendo linalotufanya sisi kuendelea kutenda jmabo wakati tayari tulikuwa tumeanza kukata tama; Kuweka nia kutufanya sisi tusiwe na mawazo ya kuacha kutenda jambo iwe katika kazi; maisha ya kawaida na hata kwenye ndoa zetu; Kuweka nia kunatusaidia sisi kupambana na dhoruma za maisha na vishawishi mbali mbali;  hakuna kati yetu anaweza kufanikiwa bila kuwa na nia dhabiti. Hata kuishi kwa mafanikio katika maisha ya kumpigania Kristo kunahitaji kuwa na nia dhabiti; wagalatia 6:9 inatufundisha kuwa Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho.

Tafakari yetu inatufundisha kuwa ujasili unategemezwa na nguvu ya Mungu kwa kuomba na kumtegemea yeye  kwani katika 2 Wakorinto 12:9 anatuhakikishia kuwa Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. Tunachotakiwa kukumbuka kuwa wakati wako Mungu aliokupa katika kufanikiwa haya ya moyo wako ni wakati wako na unatakiwa kuufanyia kazi bila kuogopa; tukumbuke kuwa unapokabiliwa na vipingamizi vyovyote unachotakiwa kusema kuwa kwa nguvu za Mungu hakuna awezaye kusimamisha hiki ambacho nimepanga au lengo ambalo nimetaka kulifikia. Nguvu za Mungu zimenijengea nia madhubuti katika moyo wangu na utendaji wangu; Popote nitakapo kanyaga nguvu na Baraka na Mwongozo wa Mungu u juu yangu.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa sisi binadamu tukumbuke kuwa kitu cha thamani sana ambacho tunakimiliki ni kuwa na NIA thabiti; hata kama utakuwa na Pesa lakini huna NIA ni kazi bure mali zako zitapotea bure. Hivyo hatak kama tutakuwa tukitembea katika bonde la uvuli wa mauti kama tuna nia na tunamtegemea Mungu hakuna kitu ambacho kitaturudisha nyuma lazima tuwe na NIA thabiti ya kuvuka na kufika katika uvuli ambao umejaa majani mabichi.

Hii ndio tafakari yetu ya leo;

Emmanuel Turuka


Thursday, May 26, 2016

NINI KINA THAMANI KUBWA KATIKA MAISHA YAKO

May 27

Je katika maisha yako ni kipi ambacho kinathamani kubwa kupita vingine? jiulize na jitathimini kwa kina kujipima nini cha thamani katika maisha yako sasa.

JE TUNAJUA WAPI TUNAKOKWENDA?




May 26

Zaburi 32:8,

Tafakari ya leo hebu tujiulize swali moja je tunajua wapi tunakokwenda? Mwanazaburi anatukumbusha kuwa atatuongoza na kutufundisha njia mbayo yatupasayo kwenda. Kwa maneno mengine sisi hatujui tunakokwenda bila msaada wa Mungu. Kwa kweli japo tunajifanya tunajua wapi tunakutaka kuwa lakini Mungu anatukumbusha kuwa bila yeye sisi hatujui na wala hatuna hata hisia ya wapi tunapaswa kwenda. Kwa maisha ya kawaida tuonaona jinsi watu wanavyobadilisha kazi, kuhama makazi kila baada ya muda mfupi; ndio sababu kila baada ya muda mfupi inatupasa kuanza kuzoeana upya na majirani wapya tatitzo sisi kama binadamu hatujui wapi tunakwenda. Nafikiri japo tuko barabarani tunakwenda kwa vile hatujui tunakokwenda hata tunavyopotea hatujui. Uelewa wa kupotea lazima ujue mwisho wa safari yako; safari hii ya kiroho ambayo inachanganya watu wengi  tunashindwa kujua wapi tunakokwenda kwa vile GPS ambayo tumepewa ili tuifuate hatujewasha kwa makusudi kwa kuona kuwa itatuchelewesha kwa vile inambambo mengi ya kuyafuata kabla ya kuanza safari.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa kwa kweli safari hii kama hatutaruhusu miingiliano ambayo inachukua akili na mawazo yetu kando ni rahisi san asana; tatizo letu tunaruhusu vitu ambavyo sio vya msingi na lazima kuingilia safari hii na matokeo yake tunaishi kuto jua njia ipi tunatakiwa kupita na kuisha kuwa hatujui wapi tunanataka kwenda. Wakati mwingine ni woga na kuogopa maneno ya watu ambao watakucheka katika safari yako hii. Tujajua kuwa Yesu alipoanza safari yake ya ukombozi alijua safari yake inaanzia wapi na atapambana na vikwazo gani mpaka mwisho wa safari yake ilipowadia pale Goligoata na kufa Msalabani na Damu yake ikamwagika kwa ajili ya wokovu wetu. Hivyo hata maandalizia yake yalikuwa wazi aliongonzwa na roho Mtakatifu, alifunga kwa siku 40, alikuwa akisali muda wote daiama alifuata maelekezo ya Mungu ambaye alimtuma aje duniani kwa ajili ya wokovu wetu;

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa Yesu pekee alijua wapi ametoka na anakwenda wapi na nini alikuwa anatakiwa afanye wakati wa safari; na hata wakati wa mapumziko wakati wa safari aliendelea kufanya matendo mema ya kuwasaidia watu wengine ili waweze kujitambua kuwa kusafiri na hasa safari ya ufalme wa Mungu lazima iweke nia madhubuti, lazima uwe na imani madhubuti na lazima uwe tayari kushinda majaribu na vishawishi mbalimbali ambavyo vitajitokeza vikiwa na lengo ya kukukwamisha ili usifike salama mwisho wa safari yako; majaribu yatakuja kimwili, kiroho na hata kijamii; vitu kama kupenda sana pesa ambazo zinatumika katika anasa; choyo; wivu; mauaji; wizi na unyanganyi; vitu hivi vyote hupelekea watu kufanya unyama wa ajabu dhidi ya binadamu mwenzao; lakini tukumbuke kuwa bado tunanafasi ya kuandaa safari hii na kuifanya kuwa na mwelekeo unaotakiwa kwa neema ya Mungu. Mungu ni mwema msamaha wake ni mkubwa kuliko dhambi zetu. Lakini lazima tujipende sisi wenyewe ili tuweze kuzishika na kufuata alama zote za Barabarani kama Mwenyezi Mungu anavyotaka sisi kufuata kupitia Mwokozi wetu yesu Kristo. Mungu daima yuko pamoja nasi na anataka sisi tutembee naye ili kufika mwisho wa safari yetu tukiwa washindi.

Tutafakari pamoja na tuanze kujifikiria leo kuwa je tuko katika mwelekeo ambao ni sahihi katika safari hii maisha ya baadae? Hii ndio tafakari yetu ya leo – Amina

Emmanuel Turuka








Wednesday, May 25, 2016

NIMEMPATA YESU

May 25


Tafakari ya ya leo ninafurahi nimempata Yesu je wewe unampenda yesu?

Tuesday, May 24, 2016

TUNAHITAJI MACHO YA KIROHO

May 24


Tafakari ya leo tunatakiwa tuendelee kuomba Mwenyezi Mungu atujalie kuona si kwa macho haya ambayo tumeyazoea bali tuombe katika Macho ya Kiroho; macho ambayo yatakuwa yanatuongoza katika njia zile ambazo Mungu anataka sisi tuenende. Macho ya upendo, kuwajali masikini, kuwapenda Yatima na kuishi kulingana na maelekezo na mafumdisho ya bibilia. sasa ni wa kati wa kuendelea kuomba utukufu huu wa macho bora toka kwa Mungu ni sasa.

Monday, May 23, 2016

JE WEWE NI MASIKINI WA ROHO?


May 23


Mathayo 6: 25-34

Tafakari ya leo tujikumbushe mahubiri ya Yesu alipowahutubia watu zaidi ya 5000 mlimani; Mwinjili Mathayo anaelezea mafundisho ya Yesu akizungumzia zaidi kuhusu Umasikini, Utajiri na Mamlaka. Yesu anatuonyesha kuwa yeye alikuwa kiongozi ambaye alikuwa anajali haki sawa kwa wote; ambaye alikuwa na mawazo ya kiuchumi na ambaye alikuwa hapendi matabaka katika jamii; hasa pale masikini wanapoonewa. Yesu alijidhihirisha kuwa yeye ni mkombozi wa wote; kwani alijua kuwa watu masikini katika jamii wako nasi siku zote; yesu aliona tatizo la tabaka ambalo lilikuwa likiendelea kukua miongoni mwa jamii kati ya walicho nacho na wale ambao walikuwa hawana yaani masikini. Na yesu alionyesha wazi kabisa kuwa anawachukia wanafiki; Yesu ameonyesha sana kuchukizwa na wale ambao wanawadhulumu wengine hasa wanyonge;  ambao wanawatumia masikini katika kujitajirisha; Yeasu mafundisho yake ni ya Haki kwani anapenda kuhubiri haki na kuishi haki;

Tafakari yetu leo inaonyesha msimamo wa Yesu kuwa  anataka sisi tuwe na furaha siku zote lakini furaha yetu ijengwe katika misingi ya haki; kama tunavyosoma katika kitabu cha zaburi 144:15 Bwana, ni nani atakayekaa Katika hema yako? Ni nani atakayefanya maskani yake Katika kilima chako kitakatifu?  Ni mtu aendaye kwa ukamilifu, Na kutenda haki. Asemaye kweli kwa moyo wake,  Asiyesingizia kwa ulimi wake. Wala hakumtenda mwenziwe mabaya, Wala hakumsengenya jirani yake.  Machoni pake mtu asiyefaa hudharauliwa, Bali huwaheshimu wamchao Bwana Ingawa ameapa kwa hasara yake, Hayabadili maneno yake.  Hakutoa fedha yake apate kula riba, Hakutwaa rushwa amwangamize asiye na hatia. Mtu atendaye mambo hayo Hataondoshwa milele. Hivi ndivyo sisi tunafapaswa kuwa na kwa umasikini huu war oho ni utajiri mkubwa sana mbele ya mwenyezi Mungu;

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa  Mungu anataka kutubariki sisi lakini ila Baraka zake zikae juu yetu lazima tuwe masinikini war oho; watu ambao tuko tayari kufuata maelekezo ya Mungu. Ili kupata furaha ya ndani kabisa ya Kimungu lazima tujiepushe na makando kando; furaha yetu daima iongozwe na miongozo ya Mungu na sio mambo ya kidunia; Mafundisho ya Yesu Mlimani ni kielelezo cha wazi kuwa ili uwe masikini wa roho na tajiri wa mbinguni watakiwa kufanya nini. Tuzikumbuke zile HERI; kwa mafundisho ya yesu mlimani Heri ni kunyume cha yale dunia inachofanya ili kuitafuta furaha. Na Bahati mbaya furaha hiyo ya dunia ni ya muda mfupi tu; Yesu hakusema heri matajiri lakini yeye alisema heri masikini, heri wanaolia. Heri wanaodhulumiwa, heri wanyenyekevu,heri wenye njaa ya haki; hawa wote ambao wanaombewa heri hizi ni watu ambao ni wanyonge hawana sauti katika mamalaka ya dunia hii na wamekandamizwa na hawawezi kufurahia utukufu wa Mungu japo wanatamani kwa sababu ya dhuluma na nguvu ya giza ambayo imekandamiza; Lakini kwa mafundisho ya yesu Mlimani anawafungua na kuwaondoa gizani na kuwapa nuru mpya ya kufurahia maisha ya yenye utukufu wa Mungu kwani ni masikini wa roho lakini ni matajiri katika ufalme wa Mungu.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa daima sisi wanadamu hata wale watumishi wa Mungu ambao wanadhani tayari ni masikini wa roho daima wanabadilisha na ulimwengu; wanaingia katika tama za kiulimwengu na katika tabia za kiulimwengu; na rahisi sana kubadilishwa tabia zetu kupitia matumizi ya tekinoloji; muziki, tvs; sinema, mitandao ya kijamii ambayo kwa haraka tu hukutoa kutoka katika maisha ya umasikini wa Kiroho na kukupeleka katika maisha ya Kilimwengu; lazima tutambue kuwa furaha ya kweli hutoka kwa Mungu kwa kufuata maagizo kupitia maandiko matakatifu; hivyo Mbinguni ni kielezo cha furaha; kielelezo cha neema na furaha na neema hiyo itadumu milele na hiyo ndio faida ya kuwa masikini wa Roho; Wokovu ambao tumepewa kupitia Msalaba ni kielelzo cha furaha kubwa kwa masikini war oho lakini ili kufurahia wokovu huu ni lazima tutimize kwa vitendo mahubiri ya Yesu Mlimani;

Tafakari ya leo inataka wewe na mimi tujiulize katika zile kheri tunazitimizaje: je Tunazitimiza kwa vitendo au kwa maneno?
Hii ndio tafakari yetu ya Leo:


 Emmanuel Turuka


Sunday, May 22, 2016

MILELE WEWE NI MUNGU

May 22

Mungu wetu anastahili kupewa sifa milele yote; Hastahili kulinganishwa na kitu kingine chochote. Jukumu letu ni Kuendelea kumpa sifa amina

Friday, May 20, 2016

TUWE WANYENYEKEVU KWA WENZETU

May 20



Tafakari ya leo tunatakiwa kukumbuka kuwa unyenyekevu ni neema ambayo tunatakiwa kumwomba Mungu ili aweze kutujalia; Hatuna sababu ya kuwadharau wenzetu au kuwaona hawafai kwa sababu tu wewe leo unamafanikio kwa namna moja au nyingine. tupendane tukumbuke Yesu alipofundisha kuhusu amri ya upendo. Hivyo tutakuwa wanyeneyekevu na kutoa heshima kwa wenzetu.

Thursday, May 19, 2016

TUNATAKIWA KUSIMAMA IMARA:


May 19
Zaburi 46:10
Tafakari ya leo inataka tujiulize kuwa je umewahi kujisikia kuwa maisha yamekuchakaza? Na ukajiona kuwa umebanwa katika ulingo na huna mahali pa kutokea au kujiokoa? Na unajishangaa kwa nini umefika katika wakati kama huo na huna msaada wa njisi ya kujinasua? Hata tukisoma katia katika kutoka katika Bibilia tunawaona wana wa Israeli walifikia hatua hii katika Sura ya 14 hawakuweza kujinasua kwa kurudi nyuma au kwenda mbele walikuwa na mwelekeo wa upande mmoja tu na hawakujua nini cha kufanya. Tujiulize tena je umwewahi kukumbwa na khali kama hii katika maisha yako? Unakuwa katika khali ya kupooza, huwezi kwenda kulia wala kushoto na hujui nini cha kufanya; angalisho hapa kuwa hata sisi ambao ni wakristo tunaweza kumbwa na khali kama hii lakini biblia inatufundisha kuwa tukipatwa na khali kama hii kimbilio lisiwe kujiua kama watu wa mataifa wafanyavyo.
Tafakari inatukumbusha kuwa kama wakristo tunatakiwa kuwa watu wa furaha wakati wote na hatutakiwi kuhofu chochote; bali kuwa watu wa shukrani wakati wote; najua tatizo kubwa ambalo linalutusumbua je utakuwaje na furaha wakati uko kwenye dimbwi la matatizo? Je utakuwaje na furaha wakati unamwomba Mwenyezi Mungu akutoe kwenye hizo shida na huoni dalili ya unafuu na shida zinaongezeka? Lakini bado tunasisitizwa na bibilia na mafundisho ya Yesu kuwa tunatakiwa kufungasha matatizo yetu na kumkabidhi Mungu ili yeye pekee abadilishe matatizo yetu kuwa kicheko. Hivyo hatutakiwi kabisa kugeuza mioyo yetu kuwa jehanamu. Tukumbuke kuwa shida nyingi ambazo tunakumbana nazo katika maisha yetu ni sababu ya sauti nyingi ambazo tunazongana nazo katika vichwa vetu, ambazo zimejaa Mawazo Hasi: mara nyingi mawazo yetu hasi yanatokana na ugumu wetu wa kusubiri  neema ya Mungu katika kututoa katika ugumu wetu wa maisha. Tunakuwa hatuna subira hata kidogo; tunalinganisha neema ya Mungu kama vile tunasubiri ahadi ya rafiki ambaye wakati mwingine hana uhakika kama atatekeleza; Tumesahau kuwa ahadi ya Mungu ni ya uhakika.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa tujifunze kusubiri ili kuona neema ya Mungu ndani ya maisha yetu na shida zetu; Hapo ndipo tunapotakiwa kusimaa IMARA na kuondoa tabia za kibinadamu za kujiamulia na kutekeleza hatima yetu ambayo mwisho wake haitusaidii kwani haituondoi katika matatizo. Tukishika usukani vibaya tukumbuke kuwa Mungu wakati wote anatusaidia kuonyesha na kuongoza njia ili tusinase katika tope; hataki tuendelee kuzama  Jukumu letu ni kuwa tayari pale Mungu anapoongea nasi na kutoa maelekezo ya namna ya kufanya. Ni jukumu letu kufanya na kusubiri wakati wa Mungu na si wakati wetu. Tumkumbuke Musa alipowavusha wana wa Isarel katika bahari ya sham pamoja na woga na kelele za kuwa tutaangamia; hawakufanikiwa kuvuka mpaka pale Mungu alipomwambia Musa sasa Nyosha Mkono wako , na alifuata maelekezo ya Mungu na Bahari ya sham ikagawanyika sehemu mbili na wakapata njia ya kupita.
Tukumbuke kuwa imani haisikilizi, viashiria vya nita nita, imani haisikilizi watu ambao hawana uvumilivu, imani haisikilizi waoga, walio kata tama bali Imani husikiliza Roho wa Mungu ambaye katika majaribu na shida zote Imani itakuambia Simama Imara na uamini kuwa mimi ndiye mwanzo na mwisho wa Maisha yako. Tukumbuka Hadithi ya Yairo; kama ilivyosimuliwa katika Luka sura ya 8. Alipomlilia Yesu akamponye Binti yake ambaye alikuwa anaumwa sana. Kwa sababu ya umati mkubwa wa watu Yairo hakufanikiwa kuongea na Yesu na alipokuwa tayari kuongea na Yesu alipwea taarifa kuwa Binti yake amefariki. Hapa Yairo alikuwa kwenye matatizo makubwa ambayo hawezi kujitoa mwenyewe, lakini yesu alimwambia usihofu alikwenda naye nyumbani kwake na Kumfufu Yule Binti yake wa miaka 12. Lisilowezekana kwetu kwa halishindikani kwa Mungu ndio maana tunatakiwa kusisma Imara.  
Kwa hiyo tutakumbusha kuwa katika khali yoyote ile ya matatizo yetu tunatakiwa kutanguliza imani mbele na kumtumaini Mungu tukifuata maelekezo ya kusimama Imara na kumwachia Mungu atuongoze na afanye kazi yake kwetu. Yeye anayafahamu maisha yetu na kila hatua ambayo tunakanyaga. Yeye ambaye anajua idadi ya nywele zetu ; hii ndi tafakari yetu ya leo- Amina

Emmanuel Turuka


         

.







Tuesday, May 17, 2016

JE UMEWEKA AGANO NA MUNGU

May 21

Ayubu 1:21

Tafakari ya leo tunangalia umuhimu wa kufanya agano na Mungu. Agano ni kitendo cha  kukiri kuwa tayari kutimiza ahadi ambayo umeweka. Bibilia inatukumbusha kuwa agano la Ayubu na Mungu lilikuwa la kutomsaliti pamoja na  mateso na shida zote ambazo alipata. Ayubu alisimama imara na kuitetea imani yake.

Tafakari yetu inatufundisha hata pale mke wake Ayubu alipo mbembeleza Ayubu kumwasi bwana alikataa kufuata ushauri huu  akijua kuwa Bwana aliyetoa ndiye mwenye mamlaka ya kutwaa.

Tujiulize leo mimi na wewe tumemwekea Mungu agano gani? Je wakati wa majibu bado tunaweza tunza agano hilo?  Ni wakati mzuri wa kujitafakari.  Kama ni mama au  baba wa  familia agano la ndoa mnalitekeleza kulingana na kiapo na mafundisho ya  bibilia? Je watoto wanatunzaje agano Lao la  utii na kuwaheshimu wazazi wao?

Tafakari ya leo inanyesha kuwa hili ni somo muhimu sana katika maisha yetu ya  kiroho jambo tunajua kutimiza agano ni  jambo gumu. Tupo kwenye dunia ambayo imejaa majaribu ambayo hutufanya tusahau kutimiza maagano yetu na Mungu. Habari njema hatujechelewa kabisa wakati wa utekelezaji wa agano au maagano ni sasa. Tumwombe Mwenyezi Mungu atufunulie hekima za kuona na kutekeleza maagano yetu naye  Amina.

Emmanuel Turuka

Monday, May 16, 2016

WEWE UNATAKA KUMJUA NANI?

May 16 


Tafakari yetu ya leo tunakilka sababu ya kutaka kumjua yule ambaye ni mwema kwetu anayetupenda kwa Moyo wote; ni wajibu wetu kumtafuta kwa nguvu zote ili tuweze kumjua na kumshukuru kila siku.
Huu ni wajibu wetu.

Sunday, May 15, 2016

MAFANIKIO YETU YANALINDWA NA MUNGU TU

May 15

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa mafanikio yetu ambayo tunayo hayatakuwa salama kama hayatapata kibali na  ulinzi wa Mungu.  Leo hii wengi tunaona mafanikio yetu hayahitaji mkono wa mungu.

Lakini tumejisahau kuwa bila neema ya ulinzi wake mafanikio yetu hupotea. Tunahitaji ulinzi wake katika mafanikio yetu yote.  Iwe ni swala la afya njema, Mali tulizopata, familia zetu. Vyeo ambavyo tunavyo na kadhalika.

Mungu ni  upendo na upendo wa Mungu daima unatuzunguka katika ulinzi wa maisha yetu na  mafanikio yetu. Hivyo ni wajibu wetu kuendelea kuomba ulinzi wa Mungu katika Mali na mafanikio yetu.

Tafakari yetu unaendelea kusisitiza kuwa bila mkono wa mungu tujihesabu kuwa hatuna mafanikio. Tutakuwa miongoni mwa wale wote waliofanikiwa lakini wakaona kuwa Mungu sio chochote, wakadharau na wakaishia katika maandalizi na anguko la miradi yao.

Ni jukumu letu kulinda mafanikio katika njia sahihi zinazompendeza Mungu. Ili baraka yake idumu,  na ulinzi wake uwe wa endelevu. Amina

Emmanuel Turuka

Saturday, May 14, 2016

WEMA NA FADHILI ZA BWANA

May 14

Tafakari ya leo tujikumbushe wema na fadhili za Mungu ambazo zimeendelea kutuzunguka kila siku katika maisha yetu. Sisi tumepata bahati ya kubwa ya ufadhili na upendeleo wa  Mungu katika kila hatua ya maisha yetu.

Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa pale ambapo tumekuwa tukikosea bado kwa upendo na  neema yake tumekuwa tukipata msamaha wa makosa yetu.

Tafakari yetu vile vile inatufundisha jinsi ambavyo kwa upendo wake alimtoa kwetu bwana wetu Yesu Kristu awe kimbilio letu na ondoleo la dhambi zetu. Damu yake iliyomwagika msalabani alipokufa katika kifo cha msalaba imetupa sisi ushindi wa ajabu sana.

Tunakila sababu ya kutembea kifua mbele kwani wema wake unaendelea kutuzunguka daima. Wema wake  hauna mipaka,  wema wake ufunguo wa maisha yetu  katika safari yetu ya mbinguni.

Tuna kila sababu ya kushukuru na kusema Aleluya. Ni wajibu wetu sasa kumpa Mungu shangwe zetu bila kukoma. Amina

Emmanuel Turuka

Friday, May 13, 2016

BWANA YESU NAKUPENDA

MAY 13 

Tafakari ya leo tumshukuru Mungu kwa upendo wake kwetu kwa ukombozi wa Bwana wetu yesu kristo. Yeye alitupenda sana na kutufia msalabani  tunakila sababu ya kumpenda. asante Yesu kwa upendo wako.

Thursday, May 12, 2016

TUNAHITAJI WAZO LILILO SAHIHI



May 12

Tafakari Ya Leo Tuangalie Nguvu Ya wazo Katika Maisha yetu. Tukumbuke kuwa maisha yetu yamejengwa na  wazo. Wazo  ni  zao  la kazi  ya  akili ambayo  inaleta fikra juu  jambo  au  khali fulani. Wazo huzaa  neno- kupitia neno  akili yetu hutafuta njia  ya  kuelezea wazo. Ili  neno liweze kutimiza haja hugeuka kuwa kielelezo cha wazo - neno  ili liweze kuonekana kupitia kigezo. (Concept ).
Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa wazo ambalo hugeuka kuwa neno lazima lielezwe kupitia, mawasiliano  (communication). Mawasiliano ili yaweze kufanya kazi lazima yawe ya pande mbili. Pande hizi zinaweza kukubaliana au kutofautiana.

Wednesday, May 11, 2016

HATUJECHELEWA MUNGU KUSAFISHA UCHAFU WETU




May 11

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa pamoja na uchafu wote ambao tunao katika maisha yetu, ni wazi kabisa hakuna sabuni yeyote ambayo inaweza kutusafisha na  uchafu huo. Sabuni pekee ni  damu  ya  Yesu.  Mkumbuke Daudi  alivyomlilia Mungu baada ya  kufanya dhambi ya kuua, ili kufanikisha adhama yake ya kuhahalisha uchafu wa zinaa.

Sisi leo tunafanya uchafu wa kila aina na  kujisifu kuwa nguvu yetu ya kibinadamu ina nguvu kuliko nguvu ya Mungu. Kwa kweli tunajidanganya sana. Uchafu ambao umezunguka mwili wetu, unatoka na na  kiburi chetu, na kujiona kuwa sisi tuna  akili ziadi ya Mumgu, afya njema ambayo tunayo ni haki yetu na haina uhusiano wowote na upendo wa Mungu; Lakini tunatakiwa kukumbuka kuwa hata   nguvu ni sehemu ya upendo wake kwetu ili tuweze kutimiza mahitaji yetu kulingana na mwongozo wake.

Leo hii sisi tumekuwa wale wanaoendesha Gari huku tukitazama nyuma,  hivyo hatuko tayari kwa ufalme wa Mungu. Tunatakiwa kufuata maelekezo na mafundisho ya bibilia ili tuweze kutembea katika njia ya bwana inavyotakiwa tutembee;


Siku ya  leo  tujitafakari kuwa hatujechelewa kusafisha uchafu wetu,  kwa sharti moja, la kumkabidhi Mungu maisha yetu kwa dhati na kuishi kulingana na sheria zake. tukitimiza ili amri kuu ya upendo na kuishi kwa vitendo - Amina

Tuesday, May 10, 2016

TAFAKARI UPENDO WA MUNGU

May 10


Tafakari yetu tuendelee kushukuru upendo wa Mungu na jinsi anavyotupenda wanadamu.

Sunday, May 8, 2016

SIKU YA KUMBUKUMBU YA KUSHEREKEA KIUNGO KIKUBWA CHA FAMILIA- MOTHERS'S DAY



May 8

Mithali 14; 1

Tafakari ya leo tunakumbuka kiungo kikubwa sana cha  familia yetu. Siku ya  kuwaenzi akina mama wote Duniani.  Tukumbuke kuwa mchango  wa  mama zetu na akina mama  wote  ni  mkubwa katika makuzi ya familia. Familia  ni  kielelezo cha juu kabisa cha  jamii yetu. Tukumbuke kuwa jamii ni  zao la familia.  kielelezo cha  familia zetu hakiwezi kukamilika kama hatutaenzi wajibu wa mama  ndani  ya  familia.  Kama  kitabu cha mithali 11- 6 kinavyosema Mwanamke mwenye moyo wa huruma hupata    heshima, Apataye mke apata kitu chema  naye ajipatia kibali kwa BWANA;huu ni ukweli mtupu ndio maana tuna kila sababu ya kusema asante sana kwa upendo wenu huo. 

Je umuhimu wa mama katika familia umejikita zaidi katika malezi? Jibu la  swali Hilo ni  hapana.  Wajibu wa  mama pamoja na ukuu wao katika malezi kwa  kweli wamevuka mipaka.  Ndio maana waswahili hunena kwenye mafanikio makubwa ya  mwanaume yeyote nyuma yake kuna  nguvu ya  mwanamke. Kama Mtaalam mmoja aliwahi sema kuwa  pindi mtoto anapozaliwa na mama anazaliwa pia, mama hakuishi kabla; bali mwanamke anaishi muda wote lakini mama ni kitu kipya kinachokuja baada ya mtoto kuzaliwa;lakini ndio wajenzi wakuu wa familia Mithali 14; 1 inatutaadhalisha kuwa Mwanamke mwenye hekima huijenga   nyumba yake,  bali mpumbavu huibomoa nyumba yake    kwa mikono yake mwenyewe.

Tafakari yetu Leo siku ya kuwashukuru sana  “ Mama” kwa jinsi wanavyojitolea katika kuhakisha kuwa kila kitu ndani ya familia kinakwenda vizuri, kama mama ni legelege ndani ya familia na familia itayumba tu; Ni ukweli usiopingika kuwa katika kila mafanikio makubwa ndani ya familia nyuma yake yuko Mama; Mitahali 5- 18 inaendelea kutufundisha kuwa Chemchemi yako na ibarikiwe  na ufurahie mke wa ujana wako;

Tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuwajalieni busara, upendo, ujasili na unyenyekevu ambao ni daraja la msingi sana katika kuimarisha nyumba bora yenye upendo mkubwa. Kwa namna ya pekee leo napenda kuwakumbuka na kuwashukuru sana na nazidi kumwomba Mungu azidi kuwajalia afya njema na amani katika maisha yenu ya kila siku hii ya kumbukumbu yenu mmekuwa daima kiungo muhimu sana katika maisha yetu na katika ukuaji wa familia. Hekima yenu haina mipaka, upendo wenu hauna mipaka, msamaha wenu hauna mipaka; nasi tunaendelea kumshukuru Mungu katika kuenzi ukuu na ujenzi wa familia zetu;

hii ndio tafakari yetu ya leo Amina

Emmanuel Turuka

Saturday, May 7, 2016

YATUPASA KUSHUKURU KWA KILA JAMBO

May 7


Tafakari ya leo dhana kubwa kama tulivyofundishwa katika injili mara kwa mara yatupasa kushukuru kwa kila jambo. Hii ndio tafakari yetu ya leo;

Friday, May 6, 2016

ASANTE SANA MAMA

May 6 

Tafakari ya leo tunapokaribia kusherekea siku ya kuwakumbuka mama zetu ambao wametufikisha hapa tulipo tuna kila sababu ya kumshukuru sana Mungu.Upendo wa mama ni wa ajabu ambao haulinganishwi na kitu chochote kile; hata ukimkasirisha vipi atakasirika na baada ya Muda tu atasamehe na kusahau na kurudisha upendo wake wote kwako. Je kwa nini tusiseme asante sana Mama na sina chochote cha kukulipa zaidi ya kukuombea tu kwa mungu ili neema zake ambazo hazina mipaka zizidi kutawala maisha yako amina. 

Thursday, May 5, 2016

NAKUTEGEMEA MUNGU WANGU

MAY 5



Tafakari yetu leo inalenga na kusisitiza kuwa pamoja na uelewa wetu ambao ni kazi ya mikono ya Mungu wetu bado tegemeo letu liko juu yake; yeye pekee yake anaweza kusimamisha Jua na kila kitu kwa neno lake tu; Hivyo tusijifanye kuwa sisi hatumtegemei mungu.

Wednesday, May 4, 2016

WAACHENI WATOTO WADOGO WAJE KWANGU



May 4

Mathayo 18: 3-4

Tafkari yetu leo tunaangalia jinsi Yesu alivyotuagiza kuwa tukiwa kama motto mdogo ni rahisi sana kuingia katika ufalme wa Mungu; Je Kwa nini yesu anataka sisi tuwe na fikra na akili za motto mdogo katika kuridhi ufalme wa mbinguni? Watoto wadogo mara zote ni wategemezi wa wazazi wao kwa kila kitu; ni wasikivu, na pale wanapokosea wataumia watalia lakini mwishoni hujinyenyekeza na kuomba msamaha, hawana kiburi, hawafikirii madaraka , wala mali na kila kitu mbele yao wanachokipata wanashukuru na kufurahia; hupenda kujifunza na hata wakikosolewa hucheka na kujaribu tena;
Tafakari yetu leo wazo kubwa ni ugumu wa sisi kama watu wazima ambao tayari tumeshakuwa na akili zetu zimeshakuwa na tunakuwa na ugumu wa kujinyenyekeza mbele ya mungu tukitambua kuwa sisi tunaweza kujitegemea sisi wenyewe na hatuhitaji msada wa Mungu; Yesu hapa anatukumbusha kuwa ili ukuu war oho unahitaji unyenyekevu ambao watoto wanao na sisi watu wazima tunapingana nao; tukumbuke kuwa unyenyekevu ni hatua ya kiroho ya kukua na sio hatua ya kujidumaza;  Yesu anatufundisha kuwa lazima tubadilike kama tunataka kuingia katika ufalme wa mbinguni; Lazima tutubu makosa yetu kwa moyo na kuweka kusudio la kuacha kutenda dhambi au kuendelea kutenda dhambi. Lazima tabia zetu kuhusu dhambi ziwe za kupinga dhambi.

Tafakari yetu  tukisoma 1 Wakoritho 14: 20 inatukumbusha kuwa Ndugu zangu, msiwe watoto katika akili zenu; lakini katika uovu mgeuzwe watoto wachanga, bali katika akili zenu mkawe watu wazima. Akili ya watotohawafikirii mabaya; ma hawafikirii kutendewa mabaya humpenda kila mtu, humwamini kila mtu, humfurahia kila mtu wamwonaye; hivyo sisi kama wakristo tunatakiwa kubadilika kuwa wema, kuishi katika maadili mema, kutenda mema, na tukifanya hivyo thawabu yetu itakuwa kubwa mbele ya Mungu; ndio hata tukisoma kutoka Injili ya Yohana 3:3-5 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.  Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?  Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. Kwa kuzaliwa kwa mara nyingine ni kuwa tayari kubadilika na kuuvaa unyenyekevu ambao ni msaada mkubwa katika matendo yetu katika kukamilisha safari yetu ya Mbinguni;

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa Mtoto hana hadhi yeyote ndani ya familia au jamii; kwa vile huonekana kuwa ni tegemezi basin a hana nafasi ya kufanya maamuzi yeyote; Hili ni tatizo kubwa kwetu kwani tunapenda kuheshimiwa, kunyenyekewa, hata wakati mwingine kuabudiwa; tunatakiwa tuwe watu ambao sio kitu katika ulimwengu huu bali tukijua kuwa Mungu ndio tegemeo letu na ngao na kinga yetu; Kama vile watoto wanavyowategemea wazazi wao kwa kila kitu nasi ni wakati wetu wa kumtegemea Mungu kwa kila kitu. 

Hii ndio tafakari yetu ya leo Amina

Emmanuel Turuka









Tuesday, May 3, 2016

JE WEWE NI MKE WA LUTU?



May 3

Mwanzo 19:26

Tafakari ya leo tunatafakari maisha yetu hapa dunia kwa kuangalia zaidi lengo letu kubwa na hatima ya maisha yetu tunaielekeza wapi? Yesu kupitia injili ya  Luka 17: 28-29 Na kadhalika, kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakinunua na kuuza, wakipanda na kujenga;  lakini siku ile Lutu aliyotoka Sodoma kulinyesha moto na kibiriti kutoka mbinguni vikawaangamiza wote. Bwana wetu Yesu Kristo alituonya kuwa Mke wa Lutu alikuwa Baridi, hajali, hana utii sio tu kwa mumeo hata kwa Mungu ndio sababu hukumu ya mungu alishuka juu yake; Kama uilivyokuwa kwa Adam na Hawa ndivyo ilivyokuwa na Mke wa Lutu; Aliambiwa asigeuke nyuma na akageuka nguzo ya Chumvi kwa kupenda kuishi katika ulimwengu wa dunia na sio ulimwengu wa Kimungu.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa tulio wengi leo hii ni kama Mke wa Lutu, hatusikii sauti ya Mungu na maelekezo yake, na kama tunaisikia basi hatuko tayari kufuata haya maelekezo yake na tunaishia kuwa Nguzo ya chumvi ambazo zinatemebea na hazina huhai wa kimungu. Mathayo 24:12 inatukumbusha kuwa  na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa; Kama ilivyokuwa kwa mke wa Lutu kuwa pamoja na kuishi na mume ambaye alikuwa akimwogopa na kufanya kazi na Mungu kwa imani kubwa na Mungu Kuwapa zawadi ya Kuishi zaidi pale alipoamua kuwasha moto wa kibiriti na kuiingamiza Sodoma, Mke wake alishindwa kutembea katika Mwendo huu wa imani na kumwogopa Mungu.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa wakati huu Sodoma ilikuwa imejaa uchafu wa kila aina; hivyo mke wa Lutu sio tu alihamia Sodoma bali Sodoma ilihamia ndani ya Nafsi yake; alikuwa mwanamke ambaye alipenda na kuabudu anasa ambazo zilikuwa zikifanyika Sodoma; Ndio maana hakuweza kusikia sauti ya Mungu ambayo ilikuwa ikimwokoa katika maangamizi alijawa na kiburi cha anasa na hivyo alishindwa kutekeleza agizo la Mungu. Hivyo tatizo kubwa ni nini hapa? Mke wa Lutu aliupenda zaidi ulimwengu kuliko kumpenda zaidi Mungu;

Kama ilivyo kwa mke wa Lutu hata sisi leo tumesongwa sana na anasa za dunia hata ile damu ya yesu ambayo imetukomboa hatuipi thamani kwani matendo yetu hayafanani na thamani ya Damu hiyo. Hata hatufanyi majukumu yetu vile inavyotakiwa; hatuna nafasi ya kuwalea watoto wetu katika maadili ya kimungu; muda wetu mwingi tunapotezea katika maisha ya anasa za dunia hii; sauti ya Mungu daima inatuambia kuwa “Jiponye nafsi yako usitazame nyuma, wala usisimame katika hilo bonde po pote; ujiponye mlimani, usije ukapotea”. Lakini hatusikii sauti hiyo na tunaendelea na maisha yetu ya anasa za duniii hii. 

Tafakari yetu leo inaendelea kutukumbusha kuwa tuache dhambi ya kiburi ambayo ndio msingi wa dhambi nyingine zote; Tuwe wanyenyekevu tusikie sauti ya bwana na kutekeleza maagizo yake; tukumbuke kuwa utii ni sadaka ya juu sana, Yesu alituagiza kama tunampenda tutazishika amri zake; kutotii ni dhambi mbaya sana; Mungu anafurahishwa na utii wetu kwake na amri, mafundisho yake kwetu sisi kupitia Mwokozi wetu yesu kristo. Tunakumbushwa kuwa tusiwe kama Mke wa Lutu aliyeangalia nyuma kwa kufikiri kuwa dunia hii ndio zaidi kwetu kuliko Mungu. Tunatakiwa kuacha dhambi ya kiburi na kutekeleza utii kwa Mungu katika kuishi maisha yetu kama yeye anavyotaka sisi tuishi;

Tafakari yetu inatutadharisha na matendo yetu ya kuangalia Nyuma; Tumeagizwa tuangalie mbele ili tuweze kufuzu kuingia katika nyumba ya Mungu; lakini kwa kuangalia nyuma kama mke wa Lutu tunakuwa tumejiondoa wenyewe katika kushiriki utukufu wa Mungu; tukisoma Luka 9: 61-62 Mtu mwingine pia akamwambia, Bwana, nitakufuata; lakini, nipe ruhusa kwanza nikawaage watu wa nyumbani mwangu. Yesu akamwambia, Mtu aliyetia mkono wake kulima, kisha akaangalia nyuma, hafai kwa ufalme wa Mungu. Hatutakiwi kabisa kuangalia nyuma tunapoutafuta ufalme wa Mungu; Kuangalia nyuma hapa maana yake ni nini? Tunayaangalia maisha yale ya zamani, ya ulevi, uzinzi, uwongo, wizi, chuki, na kadhalika; tukumbuke kuwa hakuna maisha ya baadae bila mipango hiyo kupokea maelekezo ya Mungu ndani ya Nyoyo zetu. Agizo ambalo tunapata leo hatutakiw kugeuka nyuma na kuyarudia maisha yaliyojaa dhambi. Tumepata Baraka ya kukombolewa na damu ya Yesu jukumu letu sasa ni kusonga mbele na kamwe kuto geuka Nyuma.

Hii ndio tafakari yetu ya leo;

Emmanuel Turuka


 

TAZAMA ILIVYO NJEMA NDUGU WAKIKAA KATIKA UPENDO


May 2

1Peter 3:8

Tafakari ya leo inatukumbusha kuhusu umuhimu wa wa kuishi pamoja kwa upendo na maelewano; kama waraka wa 1 Petro 3:8 unavosema Neno la mwisho ni hili; mwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu;  kama Waraka wa Waefeso 4: 2-8 unavyoyukumbusha kuwa sote lazima tuishi kwa upendo na kuwa wamoja tukizingatia kuishi katika unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo; na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani.  Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu.  Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja.  Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.  Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo. Hivyo husema, Alipopaa juu aliteka mateka, Akawapa wanadamu vipawa. 

Tafakari yetu vile vile inasisitiza kuwa  bibilia inatukumbusha kuwa tunatakiwa kuishi kwa kupendana pamoja kama waraka wa Warumi 12: 15- 18 Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao. Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili.  Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote.  Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote. Tukumbuke kuwa pale penye amani na upendo furaha ya bwana utawala na watu wanakua katika neema ya Mungu na maarafa ya mungu; umoja wa kweli huzaliwa miongoni mwetu. Lakini pale ambapo pana chuki amani hutoweka neema ya Mungu na maarifa yake hutoweka pia; woga hutawala, uwazi hupotea shetani natawala na kuleta maangamizo ambayo mwisho wake humwangamiza mwanadamu na kumfanya kujenga kiburi na majivuno.

Tafakari ya leo neno la msingi katika kuishi kwa upendo na wezetu linatawalia na neno heshima; tukiweza kuwaheshimu wezetu na kuwapa haki wanayostahili upendo utatawala maisha yetu, na hakuna kiburi wala chuki kitapata nafasi katika maisha yetu; mwenyezi Mungu anatamani sana sisi tuwe tofauti katika dhana nzima ya kuishi pamoja kwa kupendana; Mungu anataka sisi tuwe chanzo cha Baraka kwa wenzetu; tuwe watu ambao hatutamani wenzetu wapate shida au tabu; na pale wanapofanikiwa tusiwe watu wa kwanza kuwaonea wivu na kuwachukia. Bali tushangilie pamoja katika mafanikio yao na tulie pamoja na kuwapa nguvu katika shida zao.

Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa ili tuweze kufanikiwa lazima tukubali na kujikataa wenyewe; tusiwe watu ambao tunajijali wenyewe na kuona vitu bora vyote ni vyako na wengine hawastahili; bali tunahitaji kuwa wenyenyekevu na kuweka matakwa ya wengine mbele zaidi katika kuleta maisha ya upendo wa kweli miongoni mwenu na kufanikisha amri ya upendo wa kuishi pamoja. Ni jambo gumu ambalo linasumbua katika utekelezaji wake. Maisha yetu yamejaa choyo, umimi, wivu na unafiki; ni neema tu itakayo tusaidia kutekeleza dhana ya kuishi kwa pamoja kama ndugu kama tutaweza kusoma na kuelewa nyakati za Mungu na maarifa yake, katika kutekeleza upendo wa kweli .

Hii ndio tafakari yetu ya leo; Amina

Emmanuel Turuka



Sunday, May 1, 2016

TUMSHUKURU BWANA KWANI NI MWEMA


mAY 1

ZABURI YA 107


Tafakari ya leo tunakila sababu ya kumshukuru Mungu kwa upendo wake na kwa Kutujalia kuweza kuanza Mwezi Mpya wa May tukiwa na tunaendelea kufunikwa na damu ya Mkombozi wetu, na kuendelea kuneemeka na baraka na neema zake katika maisha yetu ya kila siku. Mzaburi ametuonyesha njia zote ambazo Mungu anatusaidia kama alivyowasaidia wana wa Israeli  kutoka katika mikono ya Farao na kuwalisha na kuwannemesha wakati wote wa safari kwenda katika makazi mapaya. Je wewe na mimi tunaendelea kumshukuru Mungu kila siku?

1 Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele. 

Na waseme hivi waliokombolewa na Bwana, Wale aliowakomboa na mkono wa mtesi. 

Akawakusanya kutoka nchi zote, Mashariki na magharibi, kaskazini na kusini. 

Walitanga-tanga jangwani katika njia ya nyika; Hawakuona mji wa kukaa. 

Waliona njaa, waliona na kiu, Nafsi yao ilikuwa ikizimia ndani yao. 

Wakamlilia Bwana katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao. 

Akawaongoza kwa njia ya kunyoka, Wapate kwenda mpaka mji wa kukaa. 

Na wamshukuru Bwana, kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu. 

Maana hushibisha nafsi yenye shauku, Na nafsi yenye njaa huijaza mema. 

10 Waliokaa katika giza na uvuli wa mauti, Wamefungwa katika taabu na chuma, 

11 Kwa sababu waliyaasi maneno ya Mungu, Wakalidharau shauri lake Aliye juu. 

12 Hata akawadhili moyo kwa taabu, Wakajikwaa wala hakuna msaidizi. 

13 Wakamlilia Bwana katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao. 

14 Aliwatoa katika giza na uvuli wa mauti, Akayavunja mafungo yao. 

15 Na wamshukuru Bwana kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu. 

16 Maana ameivunja milango ya shaba, Ameyakata mapingo ya chuma. 

17 Wapumbavu, kwa sababu ya ukosaji wao, Na kwa sababu ya maovu yao, hujitesa. 

18 Nafsi zao zachukia kila namna ya chakula, Wameyakaribia malango ya mauti. 

19 Wakamlilia Bwana katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao. 

20 Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao. 

21 Na wamshukuru Bwana kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu. 

22 Na wamtolee dhabihu za kushukuru, Na kuyasimulia matendo yake kwa kuimba. 

23 Washukao baharini katika merikebu, Wafanyao kazi yao katika maji mengi, 

24 Hao huziona kazi za Bwana, Na maajabu yake vilindini. 

25 Maana husema, akavumisha upepo wa dhoruba, Ukayainua juu mawimbi yake. 

26 Wapanda mbinguni, watelemka vilindini, Nafsi yao yayeyuka kwa hali mbaya. 

27 Wayumba-yumba, wapepesuka kama mlevi, Akili zao zote zawapotea. 

28 Wakamlilia Bwana katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao. 

29 Huituliza dhoruba, ikawa shwari, Mawimbi yake yakanyamaza. 

30 Ndipo walipofurahi kwa kuwa yametulia Naye huwaleta mpaka bandari waliyoitamani. 

31 Na wamshukuru Bwana kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu. 

32 Na wamtukuze katika kusanyiko la watu, Na wamhimidi katika baraza ya wazee. 

33 Amegeuza mito ikawa jangwa, Na chemchemi za maji zikawa nchi ya kiu. 

34 Nchi ya matunda mengi ikawa uwanda wa chumvi, Kwa sababu ya ubaya wao walioikaa. 

35 Amegeuza jangwa ikawa ziwa la maji, Na nchi kavu ikawa chemchemi za maji. 

36 Maana amewakalisha huko wenye njaa, Nao wametengeneza mji wa kukaa. 

37 Wakapanda mbegu katika mashamba, Na kutia mizabibu iliyotoa matunda yake. 

38 Naye huwabariki wakaongezeka sana, Wala hayapunguzi makundi yao. 

39 Kisha wakapungua na kudhilika, Kwa kuonewa na mabaya na huzuni. 

40 Akawamwagia wakuu dharau, Na kuwazungusha katika nyika isiyo na njia. 

41 Akamweka mhitaji juu mbali na mateso, Akamfanyia jamaa kama kundi la kondoo. 

42 Wanyofu wa moyo wataona na kufurahi, Na uovu wa kila namna utajifumba kinywa. 

43 Aliye na hekima na ayaangalie hayo; Na wazitafakari fadhili za Bwana.
Hii ndio tafakari yetu ya leo; Amina
Emmanuel Turuka