WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Sunday, September 18, 2011

JUMAPILI NJEMA NA MBARIKIWE SANA



“MWENYEZI MUNGU ANATUPENDA SANA”,

Ni jumapili Njema kuweza kutafakari mpango huu mzuri wa Mwenyezai Mungu juu ya maisha yetu;

Je kwa juma hili lote ambalo limekwisha je tunaweza kulipa upendo wa Mwenyezi Mungu katika maisha yetu? Tumeepushwa na mangapi mabaya? Tumepata Baraka ngapi nzuri?

Tujikumbushe kuwa Mungu wetu ni Mtakatifu na  hana ushirika na dhambi. Daima tunatenganishwa na Mungu kwa ufa mkubwa wa dhambi.

Faraja yetu kubwa ni hii kuwa Mungu anafahamu mioyo yetu.
Basi tutumie Jumapili hii ya leo popote tulipo kulitafakari hili na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa upendo wake kwetu na Msamaha ambao anaendelea kuutoka kwa sisi waja wake.


Tufurahie jumapili hii ambayo tumejaliwa kwa kumwabudu  na kutafakari haya yafuatayo:

·        Yesu aingia katika maisha yetu. (Ufunuo 3:20)
·        Tumesamehewa dhambi zetu. (Wakolosai 1:14)
·        Tumefanyika kuwa wana wa Mungu. (Yohana 1:12)
·        Tuzidi kujua makusudi ya Mungu kwa maisha yetu. (2 Wakorintho 5:14,15,17)


Amina; 

No comments:

Post a Comment