WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Friday, October 19, 2012

TUOMBEE AMANI TANZANIA HALI HII TUSIIRUHUSU IENDELEE;



NINI SULUHISHO YA HAYA YANAYOENDELEA TANZANIA YETU, NA NINANI WA KUNYOOSHEWA KIDOLE?. MUNGU IBARIKI TANZANIA

Askari Kanzu akimsindikiza kwa teke mmoja kati ya watuhumiwa waliokamatwa wakati wa operesheni maalum iliyowekwa katika jiji la Dar es Salaam,leo mchana ili kuwadhibiti baadhi ya waliodaiwa kuwa ni waumini wa dini ya kiislam, waliokuwa wamepanga kufanya maandano mchana wa leo baada ya Swala ya Ijumaa kuelekea Ikulu kwa lengo la kushinikiza kiongozi wao, Katibu wa Jumuiya za Taasisi za Kiislam, Sheikh Ponda, aliyekamatwa majuzi,aachiwe. Hata hivyo jitihada za watu hao ziligonga ukuta baada ya wao kujipanga kutokea kila kona na kukutana maeneo ya Ikulu, lakini la Askari pia walijiandaa na kujipanga vyema kila kona ya jiji na kuwadhibiti watu hao. 
Vurugu kubwa ilikuwa katika maeneo ya Kariakoo ambako pia walijitokeza baadhi ya vijana waliojichanganya na makundi hayo na kuanza kuvamia maduka na kupora mali za watu na kuwatishia wenye maduka, jambo ambalo liliwafanya Polisi kuwatawanya kwa kupiga risasi hewani na waliokaidi amri hiyo walianza kushughulikiwa kama picha hizi zinavyoonyesha Pata Mkanda Kamili.
Twende garini.....
Akaaaa sio mimi jamaniiiiiii, Babu (kulia} akijitetea...
Askari wakimdhibiti babu...
Babu akishuhshwa garini kuingizwa kituoni.....
Mgambo wa kike akipambana na kijana kumburuta kumpeleka garini, baadaye mgambo huyu CHALIII
Mgambo chaliii, lakini wapi anaye tuuuu....
Watuhumiwa wakipandishwa garini....
Watuhumiwa wakipandishwa garini....
Watuhumiwa wakipandishwa garini....
Jamaa akijaribu kueskep ambapo alikula bonge la mtama na kutambaa kama hivi na kudakwa na mgambo wa kike....

Habari na picha kwa hisani ya Vijimambo

Hofu Ya Vurugu: Mjengwablog Imefika Kariakoo .... 


 Huu ni mtaa wa Kongo.hakuna watu hapa na wala hakuna hatari ya kuibiwa hela mfukoni


 Mitaa ikiwa wazi baada ya watu kuondoka







 Magari ya maaskari

 Wanafunzi wa Benjamin Mkapa wanaofanya mitihani.dhahiri vurugu hizi zimewaathiri

Maduka yamefungwa tangia mchana na watu wameondoka nyumbani.picha hizi zimepigwa saa 10 jioni.waislamu wamejificha msikitini,maaskari ni wengi sana,mikusanyiko hairuhusiwi,na mabomu yanarushwa mara kwa mara kutawanya vikundi vya watu

No comments:

Post a Comment