ASANTE MUNGU WETU KWA KUJIBU MAOMBI YETU;
Eh Baba kama
ulivyotufundisha kusali katika sala
kuu ya Bwana ambako tunautukuza ukuu
wako na pili tunaomba msamaa wa makosa yetu na hatiamye tunaomba Baraka ya
mahitaji yetu
Tunatakiwa kuhesabu furaha
tupu tunapopatwa na majaribu mbalimbali, kwa sababu tunajua ya kuwa kujaribiwa ndani
ya imani yetu huleta saburi. Saburi na iweze kufanya kazi yake inatakiwa
kuwa timilifu, ili tupate kuwa wakamilifu,
na hivyo tutakamilishwa, bila kupungukiwa na kitu cho chote.
Tunafahamu kuwa mara
nyingi miongoni mwetu tunapungukiwa na
hekima na ndio maana tunazidi kukuomba wewe Mfalme wa wafalme , wewe uliye Alfa
na Omega uzidi kuayasikiliza maombi yetu na utujalie kuupata msaada tuuombao,
tunafahamu kuwa wewe ni mwenye ukarimu na
wala huna kinyongo,.
Lakini umetufundisha
kuwa tuombapo inatupasa kuwa na imani na kuamini na
kutokuwa na shaka, kwa sababu mtu aliye na shaka ni kama wimbi la bahari, lililochukuliwa na upepo na kutupwa huku na huku. Mtu kama huyo
tusidhani ya kuwa atapata kitu cho chote kutoka Kwako. Yeye ni mtu mwenye nia mbili, mwenye kusitasita katika njia zake zote.
Basi na tukikaribie kiti
cha rehema kwa ujasiri, ili tupewe
rehema na kupata neema ya kutusaidia
wakati wa mahitaji na Maombi yetu, sisi sio wale wenye haki bali tunatamani
kuwa miongoni mwao kwani tunafahamu kuwa maombi ya wenye haki yana nguvu tena
yanafaa sana. Tunamkumbuka Eliya alikuwa
mwanadamu kama sisi. Akaomba kwa bidii
kwamba mvua isinyeshe nayo haikunyesha juu ya nchi kwa muda wa miaka mitatu na
miezi sita. Kisha akaomba tena, mbingu zikatoa mvua nayo ardhi ikatoa
mazao yake.
Tunajongea mbele ya kiti
chako kwa unyenyekevu tukiomba wingi wa huruma yako na utusikilize katika shida
zetu, na utupe majibu ya maombi;
Tunafahamu kuwa wewe ni
Mungu ambaye unasikiliza maombi na unatujibu kwa wakati muafaka kulingana na
neema yako;
Amina
No comments:
Post a Comment