Professor Mbelle akingurumisha vuvuzela
Uzuri wa kuwa na blogu yako ni kuwa hutawaliwi na mtu katika
kuamua nini cha kuandika. Uamuzi wote ni wako. Nimesema kabla kuwa katika blogu
yangu hii, masuala ambayo yanasemwa kuwa ni nyeti, kama dini, ni ruksa
kujadiliwa. Tena sio tu ruksa, bali muhimu kujadiliwa.
Leo napenda kutoa hoja kuwa Mungu ni mmoja: anaitwa Allah, Brahman, Chiuta, Ruwa, na kadhalika, kutokana na kuwepo kwa lugha nyingi hapa duniani. Huyu ndiye aliye juu ya yote, mwenye uwezo wote, kama inavyosemwa katika ki-Arabu, "Allahu akbar." Ni dhana ya msingi katika dini zetu.
Kama wewe ni mu-Islam, halafu unasema kuwa Allah ni tofauti na Mungu wanayemwabudu wa-Kristu, au Mungu wanayemwabudu wa-Hindu, jichunguze upya, kwani utakuwa unasema kuna miungu zaidi ya mmoja. Utakuwa unaongelea kuwepo kwa mungu mwingine zaidi ya Allah. U-Islam hautambui kuwepo kwa Mungu mwingine zaidi ya Allah.
Kama wewe ni m-Kristu, halafu unasema kuwa Mungu unayemwabudu ni tofauti na Allah, basi inabidi ujichunguze, kwa misingi hiyo hiyo. U-Kristu hautambui kuwepo kwa mungu zaidi ya huyu ambaye sisi wa-Kristu tunayemwabudu, ambaye kwa ki-Arabu huitwa Allah. Usishangazwe na jina Allah. Wa-Kristu ambao ni wa-Arabu nao hutumia jina Allah, wakimaanisha Mungu, kama nilivyowahi kusema katika blogu hii.
Huyu Mungu mmoja anatajwa kwa majina mbali mbali kufutana na lugha. Wa-Tumbuka wa Malawi na Zambia humwita Chiuta. Wa-Hindu humwita Brahman. Wa-Kamba na wa-Kikuyu humwita Ngai. Wachagga humwita Ruwa.
Hoja yangu ni kuwa majina yote hayo yanamtaja Mungu huyu huyu. Muumini anayeamini kuwa kuna Mungu mmoja tu, sherti akubali na azingatie hilo. Ni ushahidi kuwa Mungu alijitambulisha kwa wanadamu duniani kote tangu mwanzo kabisa.
Nimeona nitoe mawazo yangu, kwa uhuru kabisa, kwani ni haki yangu. Kama kuna anayetaka kuyajadili au kuyapinga, namkaribisha kwa mikono miwili kufanya hivyo.

Source: hapa
kwetu blog
Asante Prof. Mbele kwa mtazamo wako wa mapana. Tatizo linakuja kwa watu wanaodhania kuwa Mungu wao ni bora kuliko Miungu wa watu wengine. Pia labda na vitu vya ndani tunavyoamini, kuwa huweszi kupata uzima wa milele bila ya qualifieres fulani za kidini. Tukubali kuwa tofauti za ki imani zipo, lakini tusikubali kuleteana chuki eti kwa sababu mimi siamini unachamini wewe, tujifunze kuvumiliana. Nashukuru kuwa Dr. Mbele unaona umuhimu wa hilo tuombe kuwe na watu wengine wanaofikiri kama wewe.
ReplyDelete