WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Sunday, October 30, 2011

TAFAKARI YA JUMAPILI YA LEO




·        Biblia inatufundisha kuwa Walio na furaha ya kweli , ni hao walio masikini rohoni , yaani tegemeo lao haliko katika mambo ya kidunia ila wanamtegemea Mungu kwa kila kitu. Walio na huzuni au wanateseka kwa sababu yake Mungu, nao watafarijiwa .

·        Bibilia inatufundisha kuwa ili kuitwa wana wa Mungu yatupasa kuleta amani na upatanisho miongoni mwa watu na kati ya watu wa miongoni mwetu.

·        Biblia inatoa mfano wa kuwa Chumvi huwa nzuri iwapo tu na ladha, ikipoteza ladha yake, basi haifai kitu ila kutupwa. Rafiki, wewe ni chumvi na ili kuhifadhi ladha, unastahili kudumisha amani wakati wote. 

Je daima tunamshukuru Mungu kwa neema ya ya uzima ambayo tumejaliwa kwa wiki hii nzima iliyokwisha?

Je tunamshukuru Mungu kwa neema ya uzuri tunaoringia miongoni mwetu?


Wakati unafanya tafakari ya jumapili ya leo wewe uko kwenye kundi gani, kati ya makundi haya matatu hapo chini?

·   Watu wema wataendelea kudumu katika uaminifu na uokovu wa maisha  yao .

· Watu aliokuwa sio wema ambao wanakubali makosa waliyofanya na  wanapojirekebisha huwa thabiti katika msimamo wao, watu walio  katika kundi hili Mungu atazidi kuwabariki.


·        Watu wa kundi la tatu wanategemea hali ya jamii ilivyo, ikiwa jamii iko katika tamaduni nzuri na wao hufuata namna ya utamaduni wao ulivyo, na ikiwa jamii haiko katika tamaduni nzuri na wao vile vile hufuatanamna ya utamaduni wao ulivyo. Mungu hutukumbusha kuwa daiama tunatakiwa kuwa na msimamo na imani katika maisha na matendo yetu na sio kuishi bila msimamo kama mawimbi ya bahari ambayo yanasukumwa na upepo kwa mwelekeo wowote ule

Nawatakieni Jumapili Njema na mbarikiwe popote pale ulipo

1 comment:

  1. Ba mdogo ushaokoka nn? naona kama una kipaji cha kuhubiri. muungane na aunt Stella mfungue kanisa. Goodluck. Anna

    ReplyDelete