·
Biblia inatufundisha
kuwa Walio na furaha ya kweli , ni hao walio masikini rohoni , yaani tegemeo
lao haliko katika mambo ya kidunia ila wanamtegemea Mungu kwa kila kitu. Walio
na huzuni au wanateseka kwa sababu yake Mungu, nao watafarijiwa .
·
Bibilia inatufundisha
kuwa ili kuitwa wana wa Mungu yatupasa kuleta amani na upatanisho miongoni mwa
watu na kati ya watu wa miongoni mwetu.
·
Biblia inatoa mfano wa
kuwa Chumvi huwa nzuri iwapo tu na ladha, ikipoteza ladha yake, basi haifai
kitu ila kutupwa. Rafiki, wewe ni chumvi na ili kuhifadhi ladha, unastahili
kudumisha amani wakati wote.
Je daima
tunamshukuru Mungu kwa neema ya ya uzima ambayo tumejaliwa kwa wiki hii nzima
iliyokwisha?
Je tunamshukuru Mungu
kwa neema ya uzuri tunaoringia miongoni mwetu?
Wakati unafanya tafakari ya jumapili ya leo wewe uko kwenye kundi gani, kati ya makundi haya matatu hapo chini?
· Watu wema wataendelea kudumu katika uaminifu na
uokovu wa maisha yao .
· Watu aliokuwa sio wema ambao wanakubali makosa
waliyofanya na wanapojirekebisha huwa
thabiti katika msimamo wao, watu walio katika kundi hili Mungu atazidi kuwabariki.
·
Watu wa kundi la tatu wanategemea hali ya jamii
ilivyo, ikiwa jamii iko katika tamaduni nzuri na wao hufuata namna ya utamaduni
wao ulivyo, na ikiwa jamii haiko katika tamaduni nzuri na wao vile vile
hufuatanamna ya utamaduni wao ulivyo. Mungu hutukumbusha kuwa daiama tunatakiwa
kuwa na msimamo na imani katika maisha na matendo yetu na sio kuishi bila
msimamo kama mawimbi ya bahari ambayo yanasukumwa na upepo kwa mwelekeo wowote
ule
Nawatakieni Jumapili Njema na mbarikiwe popote pale
ulipo