WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Sunday, June 26, 2011

NAWATAKIENI JUMAPILI NJEMA



Ni siku nzuri kumshukuru Mungu kwa ukuu wake na tuendelee kumshukuru Mungu kila wakati bila kujali hali ya maisha yetu.  Wakati wa shida na wasiwasi mwingi, inanibidi tumsifu na kumshukuru Mungu;tukiwa na raha na wakati mzuri inanibidi tuendeleekumshukuru na kumsifu Mungu pia. Kumuamini Mungu ni kuamini kwamba hata niacha niteketee jambo ninaweza kuteseka na hata kuiacha dunia hii. Imani ni kuuchukua msalaba na kumfuata matendo mazuri ambayo tulifundishwa na Bwana wetu Yesu Kristo. kwa hiyo bwana tunajumuika na wenzetu katika kukusifu wewe jumapili hii ya leo; Bwana, tuongoze tuweze kutambua upendo na huruma yako. Ujaze moyo wangu shukrani na fadhila, utuepusehe na majivuno na ukosefu wa fadhila na shukrani. tusaidie kuziona Baraka zako kwa moyo wa shukrani wakati wowote na katika mazingira yoyote ya maisha yetu


Jumapili iwe ni jumapili yenye amani  upendo na ukarimu; na kwa wale wote ambao wako safarini Mwenyezi Mungu Awaongoze na awafikishe salama kwani Mungu wetu ni Rubani na Kiongozi Bora Kwa wasafiri Basi wewe Baba Wafikishe wasafiri wote salama salimini mpaka mwisho wa safari zao Amina.

No comments:

Post a Comment