WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Sunday, June 19, 2011

LEO NI SIKU YA AKINA BABA ( Father’s Day)

`
Mzee Alois Turuka
Sherehe ya akina Baba kihistoria ni siku ya kumshukuru Mungu kuwa hata baba amejaliwa uwezo mkubwa wamalezi kama kiongozi wa nyumba. Ni wakati shakinifu wa  kutafakari  na kusherekea wajibu wa baba ndani ya familia. Ni wakati wa kumshukuru Mungu  kwa kutujalia mzazi.
                             Mzee Alois


                            Babu Mlowe


Ni dhahiri kwamba Mungu ndiye aliyeleta wazo la familia. Basi, ni halali kutazamia kwamba atatupa maelekezo jinsi familia zinavyotakiwa kuishi na kutuonya juu ya matatizo yanayoweza kuangamiza au kuharibu familia.

                             Mzee Peter Myamba

Mungu amepanga mume awe kichwa cha familia. Mungu amewaita waume kupenda, kulinda, kutimiza mahitaji na kuongoza familia zao kama kichwa. Bibilia inatukumbusha kuwa; Enyi waume, wapendeni wake zetu kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake… Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe, maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake popote; bali huulisha na kuutunza kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa. Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake. Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe (Waefeso 5:25, 28-30, 33).
                    Baba Anna ( Joseph Turuka)

                         
Upendo huu una maana gani  na kwa nini ufanyike? Kama Baba atafanya hivyo atakuwa anatimizia mahitaji yake, atamtunza, atamheshimu, atamsaidia, atamtia moyo, na atatumia muda kuwa naye.
                    Baba Rose ( Mr. Emmanuel Turuka)
                          
Je katika siku hii ya leo watoto wajibu wake nini kwa baba; Enyi watoto, watiini wazazi  na Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia (Waefeso 6:1-3).
            Baba Grace ( Mr. Alex Rumanyika)
          
Baba anatakiwa  kutowachokoze watoto wao; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana (Waefeso 6:4). Kwa kweli baba wajibu wake ni wajibu kuwalea watoto wake katika adabu na maonyo ya Bwana

                    Baba Eneke ( Dr. Frank Mwakasisi)

Bibilia inatukumbusha kuwa mtoto asiyetiwa nidhamu atakapokuwa mtu mzima atakuwa na tabia usiyompendeza Mungu. Watoto wanapaswa kutiwa nidhamu wakati wowote wanapoacha kwa makusudi kutii sheria halali zilizowekwa na wazazi wao. Watoto wasiadhibiwe kwa makosa au kutowajibika kwa sababu ya utoto. Lakini, watakiwe kukabiliana na matokeo ya makosa yao na kutowajibika kwao, na kwa njia hiyo kuwasaidia kujiandaa kwa ajili ya uhalisi wa maisha ya utu uzima.
                     Baba Brian (Mr. George Kaabuka)

Watoto wadogo wanapaswa kuadhibiwa kwa kiboko, kama Neno la Mungu linavyofundisha.Kuchapa kiboko kusilete madhara kimwili, ila kusababishe maumivu ya kutosha kumfanya mtoto yule asiyetii kulia kwa muda kidogo. Kwa njia hiyo, mtoto atajifunza kuunganisha uchungu na kutokutii. Hata Biblia inaunga mkono hilo.
Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; bali yeye ampendaye humrudi mapema. … Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali. … Usimnyime mtoto wako mapigo; maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa. Utampiga kwa fimbo, na kumwokoa nafasi yake na Kuzimu. … Fimbo na maonyo hutia hekima; bali mwana aliyeachiliwa humwaibisha mamaye (Mithali 13:24; 22:15; 23:13-14; 29:15).
Lakini ikumbukwe kuwa ni wajibu wa baba, Baada ya kiboko, mtoto anapaswa kukumbatiwa na kuhakikishiwa upendo wa mzazi aliyemchapa. kama tunavyosoma katika Mithali 22:6, kwamba: “Mlee mtoto katika njia impasayo, naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee”
      Baba Vivian Wende (mr.Rogathe Sarwatt)

 Kwa hiyo leo tunavoshereke siku ya akina baba tunajifunza sifa kubwa moja kuwa Baba, “awe mwenye kuisimamia nyumba yake vema” (1Timo. 3:4). Mahusiano yake na familia yake ni kipimo cha uwezo wake kufanya huduma. Kwa kutekeleza hilo tutaweza kuungana hata na wale
     Mchungaji Myamba mmmm na wewe ni Baba?
watoto wengine ambao huwawia vigumu kuifanya siku hii kuwa ya furaha katika kusherekea,kwani wameshajenga chuki na baba kwa sababu yeyote ya kutoelewana kimalezi; kwahiyo Pengine cha kuwashauri tu wazazi wetu akina baba wajitaidi kuleta furaha ndani ya familia kwani baba ukiweza kuitumia furaha kama kielezo cha malezi ndani ya familia ni ukweli ambao haufichiki kuwa watoto watakuwa katika malezi ya upendo na heshima daima.
                               Mr. Kagumba
Nayarudia haya kwa msisitizo:
·        Je bibilia inatufundisha nini kuhusu umuhimu wa baba ndani ya familia Waefeso 6:1-3 

·        Tukifanikiwa kuisherekea sherehe hi inaonyesha wazi kuwa  kama   Kutoka; 20:12  kutambua wajibu wa baba inammainisha upendo wetu kwao na heshima kwao ndio wajibu ambao Mungu ametuagiza kuufanya sisi kama watoto ndani ya familia zetu na tutapata Baraka ya kuweza kuishi maisha marefu ambayo yatajaa furaha na amani.




   ·        Bibilia inawakumbusha wazazi wetu kuwa watufunze katika njia itupasayo kwenda nasi tukiwa wazee hatutaacha njia hiyo kamwe. 


                      Dr. Mwalimu Kassim



  • Akina Baba tunatakiwa tuwe wacheshi katika   familiazetukwani uchesi ni zawadi nzuri ya ukuaji wa familia bora 



No comments:

Post a Comment