TUTAKUKUMBUKA DAIMA
Kuna msemo wa kale unaosema kuwa kifo kinatufungulia mlango na kutupeleka sehemu ambayo hatuifahamu; lakini Yesu katika mahubiri yake aliupinga mtanzamo huu pale aliposema katika John 11:25-26 “Mimi ndiye huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye Mimi, hata akifa atakuwa anaishi 26 na ye yote aishiye nakuniamini hatakufa kabisa hata milele”. Mtume Paulo yeye anatufundisha katika sura ya 14:8 kuwa 8 Kama tunaishi, tunaishi kwa Bwana, nasi pia tukifa twafa kwa Bwana. Kwa hiyo basi, kama tukiishi au kama tukifa, sisi ni mali ya Bwana.
Lakini pamoja na uthibitisho wote huu kifo sio rafiki mzuri hata kidogo katika maisha yetu kwani hata tukisoma kutoka katika kitabu cha Marko 14: 36 yesu aliwaambia wafuasi wake kuwa “Moyo wangu umejawa na huzuni kiasi cha kufa. Kaeni hapa na mkeshe.” 35 Akaenda mbele kidogo, akajitupa chini kifudifudi akaomba akisema, kama ikiwezekana saa hiyo ya mateso imwepuke. 36 Akasema, “Aba c Baba, mambo yote yawezekana Kwako. Niondolee kikombe hiki, lakini si kama nitakavyo Mimi, bali mapenzi Yako yatimizwe.’’
Kulingana na ubinadamu wetu tukio lolote la kifo halizoeleki hata kama utakuwa ni shupavu kiasi gani, kifo ni tendo ambalo halina kipimo kabisa,
Ni miaka kumi na sita (16) imepita toka Mwenyezi Mungu alipokuita katika makao yake ya milele; tulijiuliza maswali mengi lakini tuliishia tu kumshukuru Mungu kwa kumjalia maisha mema hapa dunia katika kipindi chote cha uhaki wake, kwani alifanikiwa kutimiza majuku yake kwa kiasi kikubwa na kulingana na neema na maagizo yake;
Je tunapowakumbuka wapendwa wetu yatupasa tufanye nini sasa?
- Tujitathimini uhalisia wa maisha yetu mbele yake kwa kujali zaidi matendo yetu na kuangalia mbele ili tuweze kusafiri katika mstari ulionyoka kama marko 8:62 62 Yesu akamwambia, “Mtu ye yote atiaye mkono wake kulima, kisha akatazama nyuma, hafai kwa Ufalme wa Mungu.”
Unakumbukwa sana na Mke wako mama yetu mpendwa Anna M. Kinunda na watoto wako wote, wakwe, wajukuu wako, vitukuu, marafiki na kila mtu.
Sisi tulikupenda daima lakini mwenyezi Mungu alikupenda zadi kwasni yeye ndiye aliye toa na yeye ndiye aliyetwaa kama anavyotufundisha kutoka Kitabu cha ufunuo 20:4 kinatukumbusha kuwa 4 Atafuta kila chozi, kutoka katika macho yao. Mauti haitakuwepo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu, kwa maana mambo ya kwanza yamekwisha kupita.’’
Amen
No comments:
Post a Comment