WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Thursday, July 14, 2016

KWA NINI UNAMWOGOPA MTU MWINGINE?



July 14

Tafakari ya leo tunaangalia tatizo la kumwogopa mtu mwingine katika maisha yetu kama wakristo; kama wewe ni mfuasi wa Yesu basi hutakiwi kumwogopa mtu mwingine yeyote ambaye hawezi kuua roho; kama katika maisha yako utakuwa unafanya maamuzi yako kwa kumwogopa mtu au watu wengine basi wewe unatatizo kubwa sana la kiimani. Kama tabia hiyo ikikutokea basi unatakiwa kucha kuwaangalia watu wengine katika kutimiza mahitaji yako; bali tunatakiwa tumtazame Mungu ndiye pekee mtoaji wa mahitaji yetu; kwa kufanya hivyo utajisikia vizuri mwenyewe bila kufuata maoni ya wengine.

Tafakari yetu leo inatukumbusha ili kujiridhisha katika maamuzi yako jambo la kwanza unatakiwa ujiulize kuwa wewe ni nani? Na ukumbuke kuwa wewe umepewa na mwenyezi Mungu neema ya kupendwa na yeye; tulivyoumbwa tuliumbwa watupu na Mungu kwa mapendo yake ametujaza na Baraka ya upendo. Kama wewe umejazwa na upendo wa Mungu kwa nini sasa unakubali kutawaliwa na watu wengine katika mawazo yako? Binadamu mwingine yeyote yule hana nguvu ya kutawala akili yako isipokuwa Mungu tu. Ndio maana Yesu alivyosema kuwa unapojiona kuwa unatabia ya aina hiyo yeye ana njia ya kutokea; basi tunatakiwa kumruhusu Yesu kujaza sisi na upendo wake ambao hauna mipaka lakini kama tutakuwa tayari kutekeleza mipango ya Mungu na sio mipango ya binadamu tunatakiwa kuwa tayari katika kutimiza utukufu wa mungu na sio matamanio yetu. Ili tuweze kujihakikishia kuwa tuko imara na hatumwogopi mtu yeyote lazima maisha yetu tuyaweke chini ya msingi wa uangalizi wa Yesu hapo hatutakuwa na sababu ya kumwogopa mtu yeyote na tutajihakikishia furaha ya kweli;

Tafakari yetu inatuonya kuwa hatutakiwi kabisa kutawaliwa na mawazo, woga ; mwonekano dhidi ya watu wengine kuwa watasemaje ; najua mara nyingi tatizo linakuwa pale wanapotaka kunufaika na kile ambacho wao wanancho na pengine mimi au wewe huna au sina na unatamani upate huko ukifikiri kuwa Mwenyezi Mungu hawezi kukupa wewe hiyo Baraka. Tunapo mwamini na kumtumaini mungu yeye Baraka zake anazitoa kwa namna ya ajabu na pekee kabisa. Hivyo hata pale tunaposoma bibilia katika msingi huu ndipo tunapoona jinsi gani tunavyowaogopa binadamu wengine. Tuangalie mifano kutoka Mwanzo 12:10-20 au Mwanzo 20: I-2 AU Hesabu 14:11 DEUt 1:17 Zaburi 56:3-4 Matahayo 10:28 1 petro 3:14

Lazima tutambue kuwa woga wa kweli wa kumwogopa Mungu ni kupitia maungamo; Mathayo 22:16 kwa kuungama dhambi zetu Mungu kupitia bwana wetu Yesu Krsito anaondoa woga kabisa; tunatakuwa kujitathimini wenyewe kwa kujiridhisha kuwa mungu ni wa ajabu katika maisha yetu na hatuna sababu ya kumwogopa yeyote isipokuwa yeye; woga kwa Mungu ni chanzo cha maarifa. Mungu lazima aogopwe kwa sababu yeye ni chanzo cha  haki; chanzo cha upendo; na mafanikio yetu. Zaburi ya 77: 13

 Ili tuweze fanikiwa lazima tuishi katika mafundisho ya Mungu; tujiepushe  kwa kikombe cha  ubinafsi  na baada yake tunatakiwa tujazwe na kikombe cha roho wake ili kitupe ujasiri wa kuweza kushinda woga na kuwa tayari kuungama dhambi zetu ili kujipatanisha na Mungu. Bibilia inatufundisha kuwa watu wamegawanyika katika makundi makubwa matatu; maadui, majirani na wafuasi wa kristo. Jambo kubwa katika makundi hayo yanayoleta tofauti ni upendo upendo huleta kila kitu; tunawahitaji watu ili tuweze kuwauliza maswali; je tunawahitaji watu ili kukamilisha haja zetu? Wafilipi 2:3 auwarumi 13:8. Tukumbuke kuwa woga ni tatizo la jumla kwa binadamu.

Hii ndio tafakari yetu ya leo

Emmanuel Turuka


No comments:

Post a Comment