WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Thursday, July 21, 2016

UFALME WA MUNGU UKO NDANI YAKO


July 21

Luka 17:20-21

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa ufalme wa Mungu uko ndani yako; mafarisaya walimuuliza Yesu je ufalme wa Mungu utakuja lini? Yesu aliwajibu kuwa ufalme wa Mungu hauji kwa kuangalia vitu na matukio yanayoonekana isopokuwa ufalme wa Mungu uko ndani yenu; hata pale Philipo alipomwuliza yesu awaonyeshe baba nasi tutaridhika; Yesu alimjibu kuwa nimekuwa nanyi muda huu wote na bado hamjemjua baba? Yeyote aliyeniona mimi amemwona Baba; mimi niko ndani ya baba na baba ndani yangu; na yeyote anayeamini katika neno langu ameamini kwa baba aliyenituma;

Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa jukumu letu inatakiwa tujiangalie zaidi undani wa matendo yetu na  sio matendo yetu au mwonekano wetu wan je katika maisha ya kumtumikia Mungu; Mwonekano wetu wa nje unalinganishwa na jinsi tunavyojiangalia katika kioo na kujiona kitaswira tuko vipi na daima tunachukua muda wa kujirekebisha ili tuweze kuonekana watanashati. Ni jambo nzuri hivyo kama tukiweza kuchukua juhudi hizo katika taathimini ya ndani itakuwa jambo nzuri sana; ni wazi kuwa katika mazingira ya maisha yetu leo hii; maisha yetu yametawaliwa na utitili wa mambo; maisha yetu yamekabiliwa na majukumu yetu ya kila siku, kazi ambazo lazima tuzimalize kwa wakati, mahitaji ambayo tunayaona ya lazima; na tama zetu za kila siku mabazo tunatamani kuzikamilisha; ni wazi kabisa na rahisi kabisa kama binadamu kupoteza mwelekeo katika utitili huu wa maisha; Luka 15:17  ni kama mtu ambaye ameshituka kutoka katika ndoto mbaya na kutisha pamoja na kutokwa na jasho lakini itamchukua muda ili akili yake iweze kurudi tena;

Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa  katika khali ya kupotea inapelekea mambo mawili  ulinzi wa uwongo ambao unakudhoofisha wewe mwenyewe; hatimaye unajipoteza mwenyewe kuna mambo mawili yatajitokeza mosi ni kujijua aina ya mtu uliyezoea kuwa na pili  na unajipoteza kabisa  katika uhalisia wako.  Je unakumbuka hadithi ya mwana mpotevu  alifika mahali akajitambua yeye mwenyewe kuwa amepotea; tabu zote ambazo alizipata ni matokeo ya tama ambazo alifikiri kuwa atapata maendeleo makubwa katika maisha yake matokeo yake kuwa aliishia kupotea na kurudi nyuma kimaendeleo na kimaisha. Utambuzi wa kwanza ambao humjia mtu mabaye amepotea anapojitambua kuwa alikuwa amepotea ni khali ya kujijutia kwa namna gani alianguka na kushinda kufika pale alipokuwa amekusudia kufika, ananza kujenga woga  kwa nini amefanya hivyo alivofanya. Je unakumbuka Samsoni alipoamka na kujikuta mikononi mwa maadui na sio mikononi mwa Mungu? Au unamkumbuka Yona alivyotapikwa na samaki ukingoni mwa pwani; ndio maana lazima tukubali kuwa kitu kikubwa hapa duniani sio wapi tunaposimama bali ni katika mwelekeo gani tunakwenda: na tutafurahi zaidi pale tukapofika mwisho wa safari yetu katika utukufu wa Mbinguni;

Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa kitu kikubwa na cha msingi sana katika maisha yetu ni  kuwa na furaha ambayo inatupa sisi nafasi ya kutenda; furaha ambayo inatupa sisi kitu cha kutumaini na ikumbukwe kuwa mtu yeyyote anaweza kupata furaha hasa pale ambap anapata kamba ya wokovu kutoka kwa Mwenyezi Mungu ya kumvusha. Tukumbuke jinsi Samsoni pamoja na kuwa kipofu baada ya kutekwa na maadui kwa sababu ya Delila lakini kwa kumtumaini na kujuta makosa yake Mungu alimrejeshea nguvu zake kwa dhumuni hasa la kuwaangamiza wafipipi ambao walikuwa wamemeteka na kumtesa. Yona pamoja kuwa alikuwa gizani kwenye tumbo la samaki kwa vile aligundua kosa lake wokovu wa Mungu na mwanga wa wokovu ulimrudia kwa mara ya pili na kuanza kuhubiri.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa mtu lazima aishi kwa malengo na madhumuni na kama lengo au dhumuni likipotea basi  maisha yake yanakuwa hayaeleweki ndipo tunapohitaji msaada wa Mungu katika kufanikisha dhumuni la maisha yetu. Pale ambapo tunashindwa kujitambua unakuwa umepotea kiroho, macho yako yanakuwa yamefungwa masikio yako yanakuwa yamezibwa, na ni Mungu pekee yake ambaye anaweza kuleta muujiza katika wakati kama huu. Ni wkati ambapo neema ya Mungu inahitajika. Tumkumbuke Daudi alipopotelea katika dhambi lakini ujio wa Mungu Katika maisha yake uliweza kumrudishia furaha na amani. Amani ya kweli upendo wa kweli na maisha ya neema ya kweli hayawezekani bila uwepo wa Mungu. Mungu ni kila kitu kwetu na katika maisha yetu ya kweli.
Ni ujumbe mzito ambao unahitaji utambuzi wa kweli. Hii ndio tafakari yetu ya leo. Amina

Emmanuel Turuka




No comments:

Post a Comment